Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza wananchi kwenye mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile yanayotarajiwa kufanyika Disemba pili, jimboni kwake Kigamboni Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu Dkt. Ndugulile unatarajiwa kuwasili nchini kesho Novemba 29, 2024 ukitokea India mauti yalipomfika wakati akipatiwa matibabu.

Dkt. Ndugulile alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumatano Novemba 27, 2024.

Soma: Dkt. Faustine Ndugulile aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni afariki Dunia
 
Khee! Tayari mmekwisha gawana majukumu! Basi na mimi nitakuwa mwandazi wa kugawa masinia ya pilau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…