Rais Samia kuongoza Vikao vya Kamati kuu na Halmshauri kuu ya CCM Taifa June 29-30

Rais Samia kuongoza Vikao vya Kamati kuu na Halmshauri kuu ya CCM Taifa June 29-30

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Habari ni kuwa Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hasssan Mwenyekiti wa CCM Taifa, ambaye pia ndiye Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama, ataongoza vikao vya Kamati kuu na Halmshauri kuu ya CCM Taifa Tarehe 29 na 30 Mwezi huu jijini Dar.

Vikao hivyo vitatanguliwa na vikao vya Secretarieti ya CCM vitakavyoketi na kufanyika Tarehe 27 na 28 Mwezi huu jijini.

Chama ni vikao, huko ndiko masuala mbalimbali huzungumzwa na mipango na mikakati mbalimbali kuwekwa katika kukiimarisha chama na kukipa nguvu kuanzia ngazi ya shina, Tawi, kata, wilaya, mkoa mpaka Taifa ndio maana CCM Inaendelea kuimarika na kuwa na nguvu kila uchwao.

Tofauti na vyama kama CHADEMA vinavyoendelea kudumaa kila uchwao na kupoteza muelekeo,vinakwenda tu utafikiri gari lililokatika breki pamoja na usukani.hakuna cha utaratibu wala mfumo unaoeleweka ,ndio maana unakuta kila mtu anajadili na kuweka msimamo wake juu ya jambo fulani kupitia ukurasa wake wa kijamii Kabla hata ya vikao rasmi vya chama.

Utaona kiongozi huyu anatoka hadharani mbele ya camera anaongea mambo yaliyotakiwa kuzungumzwa na kujadiliwa kwenye vikao vya ndani vya chama,anaita waandishi wa habari na kuanza kuzungumza yanayomjia kichwani mwake tu bila breki ya mdomo.

utoto wa namna hiyo huwezi kuukuta ndani ya CCM wala kuona au kusikia ukifanyika..ndio maana CCM kinaitwa chama kiongozi na tumaini la watanzania.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Screenshot_20240627-164908_1.jpg
 
Kwenye vikao vyenu hivyo ,kumbukeni kujadili habari za GEN Z.

Msijidanganye kuwa uraiani Hali Iko shwari.

Pitieni hii attachment, ili mjue mko na kizazi kipi
 

Attachments

  • IMG-20240627-WA0012.jpg
    IMG-20240627-WA0012.jpg
    71.5 KB · Views: 3
Dah! Naona mtoa mada anashambuliwa na makombora makali kila upande. Nahisi mpaka muda huu atakuwa amejificha sehemu salama ili tu kuyanusuru maisha yake.
 
Katika hali ya sasa na tension zote hizi nchini utashangaa kusikia agenda za hicho kikao......

1. Kufungua kikao

2. Kupokea ripoti ya utendaji wa ziara ya Rais Korea

3. Kukemea chokochoko za kumzuia rais znz kuongeza muda

4. Chama kumpongeza Rais

5. Kufunga kikao
Kaa kwa kutulia maana nimeona umeanza kutetemeka na kupata presha kabla hata ya kikao hakijaanza.
 
Dah! Naona mtoa mada anashambuliwa na makombora makali kila upande. Nahisi mpaka muda huu atakuwa amejificha sehemu salama ili tu kuyanusuru maisha yake.
Makombora yapi ndugu yangu mtanzania uliyejaa msongo wa mawazo.mimi ni Mwamba kwelikweli na hakuna wa kuweza kunitikisa wala kuniyumbisha.
 
Back
Top Bottom