Rais Samia kusaini EPA huko Brussels?

Rais Samia kusaini EPA huko Brussels?

Status
Not open for further replies.

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Ile Trade Agreement EPA iliyokuwa inapingwa kwa kila hali na CCM sasa kusainiwa na Raisi wa Tanzania Samia huko Brussels kwenye EU- Afrika Union summit.

EPA ni free trade Agreement Kati ya EU na Nchi za Afrika Mashariki zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.

Tanzania walipinga EPA kwa maana hawakuona manufaa yoyote kwa nchi yetu kwani hatuna cha kuuza EU wakati EU wana kila kitu cha kuuza kwetu.

Je, Viwanda vyetu juice ya Azam na umeme wa mgao vita compete na EU products? Kama hapo Kenya tu au Uganda ni ngumu kushindana tutaweza EU ?

Ikumbukwe sukari kutoka Brazili ni cheaper kuliko ya Tanzania sasa EU products tax free Tanzania, tutaweza?

Tunategemea kuuza nini EU ? Vipi natural resources zetu ?

Kweli ni Vita ya Kiuchumi RIP Magu

=====

UPDATES: TAARIFA HII IMEKANUSHWA NA SERIKALI

Serikali: Hatujasaini EPA, Msimamo wetu uko palepale

Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara imekanusha suala linaloendelea mtandaoni kuwa serikali imepitisha Economic Partnership Agreement(EPA) ambayo imetajwa na wasomi wengi kuwa itasababisha Tanzania kupoteza mapato yanayotokana na Importations kwa takribani 71% in the long run

Wizara imesema mijadala inayoendelea mitandaoni kuhusu suala hilo halina ukweli bali bado Tanzania inaendelea kuwa na msimamo wa kukataa makubaliano hayo ambayo yalipingwa vikali na Rais Mkapa mwaka 2015 katika moja ya andiko lake, ambapo pia rais Magufuli aliyakataa suala hilo.

Serikali imesema inaendelea kufanya mambo yenye manufaa kwa nchi na Jumuiya ya Afrika mashariki na kuwataka wananchi kupuuza taarifa zinazoenea mtandaoni.

Zaidi kuhusu kanusho hili soma: Serikali: Hatujasaini EPA. Msimamo wetu uko palepale
 
wenzio huku west africa juice zao nyingi za kutoka Europa. Wenye viwanda kazi kwao hili washindane na imported goods. Je mazao yetu yana kiwango cha kushindana na wakulima wa mabeberu au ndo tutauza tu kwa wenzetu hapa Africa?

Sasa utashindana na Mgao wa umeme wa masaa 12 ?
 
Hivi vitu vyengine kabla hawaja sign wawe wanatuelimisha kwanza sasa mtu nasikia tu EPA!,faida yake sijui,hasara pia sijui..! Haya vipi kama ni mpango mkakati wa siri ndani yake..?

Tunaambiwa tu nchi inafunguliwa,aisee kunakufunguliwa na kuliwa..😂
 
Nimesoma na kusema ilkabidi nicheke tuu! Kusema kweli Rais wetu si mwenye tabia ya kusoma vitu hata kidogo! Sitashangaa yeye akisaini kwakuwa kaambiwa! Rais wetu yeye huwa akikutana na mkataba ni kusaini tuu wala sina hakika kama anao muda wa kusoma hata kidogo.

Rais Samia ana udhaifu wa kutopenda kufatilia kujipa muda wa kujitafakari na kupitia mambo yeye huwa ni mtu wa kuanguka tuu sahihi hana muda kabisa.

Nakumbuka hata ule mkataba pale bandarini alishiriki utiwaji saini baadae akaja kugundua aliingizwa cha kike

Lakini Rais Samia anahitaji kushauriwa zaidi kabla ya kusaini mikataba ni lazima tuangalie mbele na tujiulize je viwanda vyetu na huo uchumi wa viwanda tutafika kweli?

Rais Samia lazima awe makini kwa watu wake wanao mshauri!
 
wenzio huku west africa juice zao nyingi za kutoka Europa. Wenye viwanda kazi kwao hili washindane na imported goods. Je mazao yetu yana kiwango cha kushindana na wakulima wa mabeberu au ndo tutauza tu kwa wenzetu hapa Africa?

Mtu umeme kuupata ni mbinde ashindane na nani atakayemmudu? Hawa watu wa viwanda wanapaswa kulindwa kwa nguvu zote.
 
Hivi vitu vyengine kabla hawaja sign wawe wanatuelimisha kwanza sasa mtu nasikia tu EPA!,faida yake sijui,hasara pia sijui..! Haya vipi kama ni mpango mkakati wa siri ndani yake..?
Tunaambiwa tu nchi inafunguliwa,aisee kunakufunguliwa na kuliwa..[emoji23]
Ungesema hivyo kuanzia wakati wa jiwe, sasa hivi unaonekana kanjanja tu mataga mwenye gubu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom