Rais Samia Kushiriki Mkutano wa Nishati ya Nyuklia, Rwanda

Rais Samia Kushiriki Mkutano wa Nishati ya Nyuklia, Rwanda

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo anaondoka nchini kuelekea Kigali, Rwanda, kushiriki Mkutano wa Uvumbuzi wa Nishati ya Nyuklia barani Afrika (NEISA 2026).

Mkutano huo utakutanisha viongozi wa Serikali, watunga sera, wawekezaji, wadhibiti na wadau wa sekta ya nishati kujadili nafasi ya nishati ya nyuklia katika kuimarisha usalama wa nishati, viwanda na maendeleo endelevu barani Afrika.

Mkutano wa NEISA 2026 unatoa nafasi kwa Tanzania kushiriki katika ajenda ya Afrika ya matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia katika nishati, afya, kilimo, viwanda na utafiti.

20260519_080538.jpg
 
Daktari Samia Suluhu Hassani ameondoka nchini kwenda kujadili na Viongozi wenzake wa Afrika mashariki kuhusu uvumbuzi wa Nishati ya Nyukilia.


Video Courtesy: State House instagram Account
 
Back
Top Bottom