Rais Samia kutana na viongozi wa upinzani mapema zaidi

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Wanaomshauri Rais Samia wamshauri akutane na viongozi wa upinzani sasa na akisubiri zaidi ndiyo itakuwa ngumu zaidi.

Kwa sasa ni rahisi kukutana nao na kuwaambia umma ni kujadili corona, katiba, kujuana, amani ya nchi na miradi ya nchi.

Usisubiri ukafanya mkutano wakati upinzani wana nguvu zaidi maana kila siku madai yanaongezeka
 
Hakika tumpe mama mda huku makundi mengine ameshakutana nayo.
Upande wangu kundi No 1 ilitakiwa ni vyama vya siasa angekuwa amekata mzizi wa fitina.
Huko nje anakojenga bila kujenga ndani kwanza naiona kasoro,watu wa nje watamgeuka kesho tu asipojenga mahusiano na upinzani
 
bora akutane na walemavu kuliko ninyi wachumia tumbo.
JK aliwapa juisi mkaishia kumtukana tu
Walemavu ndio mtaji wako kisiasa?
Tumia katiba upate haki kwa makundi yote.
 
bora akutane na walemavu kuliko ninyi wachumia tumbo.
JK aliwapa juisi mkaishia kumtukana tu

..umetumia lugha kali dhidi ya walemavu.

..umewaweka ktk kundi lisilofaa kukutana na Raisi.
 
Wanao mshauri Rais Samia wamahauri akutane na viongozi wa upinzani sasa na akisubiri zaidi ndiyo itakuwa ngumu zaidi.

kwa sasa ni rahisi kukutana nao na kuwaambia umma ni kujadili corona, katiba, kujuana, amani ya nchi na miradi ya nchi. Usisubiri ukafanya mkutano wakati upinzani wana nguvu zaidi maana kila siku madai yanaongezeka
Na wapinzani wanazidi kupata credibility kwa wananchi huku yeye akipoteza mtaji wa kisiasa

Washauri wa Samia wamwambie tu kuwa
1. Hakubaliki sana na wafuasi wa Magufuli mpaka leo hii!

2. Alikuwa anakubalika na kundi lisilomkubali Magufuli lakini sasa nalo amelikorofisha kwa kutaka kuongoza nchi kinyume cha sheria kama Magufuli,Kundi hili lilidhani angekuwa mheshimu katiba, sheria, mheshimu kiapo chake, kumbe na yeye anataka kuendesha nchi kidikteta!

Kwa hiyo yupoyupo tu na umma unaelekea kutoridhishwa na utendaji wake kwa sababu haleti reform zozote za maana kisiasa na hata huko kwenye uchumi anawapa wananchi mikodi mikubwa na kuyafanya maisha yao kuwa Magumu!
 
Kwa tukio la Kwanza kuna dalili Mama katumika vibaya bila kauli yake.
Watu wakujipendekeza ndio wamefanya hivyo wakidhani wanampaisha mama kumbe wamemkorogea.
Kuna mchanganyiko Fulani wa maelezo hats ukiwa na akili ndogo huwezifanya vile.

RPC wa Mwanza sio size yake.
Singida,Shinyanga,Simiyu kutamfaa
 
Mwezi wa nne huu, Samia kakutana na makundi yaliyokuwa yanamkenulia tu lakini wapinzani na hasa Chadema anawahofia sana watamweka kwenye kiti moto na kuzidi kudhihirisha alivyo dikteta, mtupu kichwani na hatari kwa nchi yetu.

Wanao mshauri Rais Samia wamahauri akutane na viongozi wa upinzani sasa na akisubiri zaidi ndiyo itakuwa ngumu zaidi.

Kwa sasa ni rahisi kukutana nao na kuwaambia umma ni kujadili corona, katiba, kujuana, amani ya nchi na miradi ya nchi.

Usisubiri ukafanya mkutano wakati upinzani wana nguvu zaidi maana kila siku madai yanaongezeka
 
Wanaomshauri Rais Samia wamshauri akutane na viongozi wa upinzani sasa na akisubiri zaidi ndiyo itakuwa ngumu zaidi.

Kwa sasa ni rahisi kukutana nao na kuwaambia umma ni kujadili corona, katiba, kujuana, amani ya nchi na miradi ya nchi.

Usisubiri ukafanya mkutano wakati upinzani wana nguvu zaidi maana kila siku madai yanaongezeka

Narudia hili ni mihimu sana
 
Mama anaupiga mwingi.
 
Tulishauri sasa tunaona matokeo. Rais washauri wake wa siasa inabidi awafikirie upya
 
..Rais ameshakutana na viongozi wa ACT kuhusiana na tatizo lililotokea ktk uchaguzi mdogo wa jimbo la Konde Pemba.

..matokeo ya mkutano baina ya Rais SSH na ACT ni mbunge mteule wa Konde tiketi ya CCM kujiuzulu nafasi yake.

..Nadhani kwa huku Tanganyika Rais SSH hana watu wa kutosha wanaopendelea maridhiano baina ya vyama na wanasiasa walioko huku.

..Au labda pressure ya maridhiano toka kwa vyama vilivyoko Tanganyika haijawa kubwa vya kutosha kumfanya SSH kuona ulazima wa kukutana nao.

..Kabla ya Rais SSH kukutana na ACT Rais wa ZNZ na katibu mkuu wa CCM walikutana na viongozi wa ACT ili kujaribu kuzima mgogoro wa uchaguzi uliokuwa umetokea.
 
Yaani unamaanisha rais akutane na magaidi!
 
Back
Top Bottom