Rais Samia kuunda tume mbili kushughulikia suala la Ngorongoro

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema ataunda tume mbili, moja itachunguza na kutoa mapendakezo kuhusu masuala ya ardhi yanayolalamikiwa na wakazi wa Ngorongoro na nyingine itaangalia utekelezaji wa uhamaji kwa hiari kutoka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Rais Samia amesema hayo leo Jumapili, Desemba mosi, 2024 Ikulu ndogo ya Arusha alipozungumza na viongozi wa kimila wa jamii ya kimasai (Malaigwanani) wanaoishi eneo la Ngorongoro.

Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kuwasikiliza viongozi hao kutokana na kuwepo malalamiko kuhusu baadhi ya uamuzi wa Serikali kuhusu eneo la Ngorongoro.

Soma Pia: Sakata la Ngorongoro Rais anadanganywa', afike awasikilize Wananchi atabaini uhalisia - Olengurumwa

Pia, amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuimarisha utendaji kazi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya Serikali na jamii hiyo.

Katika hatua nyingine, Rais Samia ameitaka Ofisi ya Rais-Tamisemi kushughulikia changamoto zinazojitokeza, ikiwemo kukosekana kwa baadhi ya huduma za msingi za kijamii katika eneo la Ngorongoro.
 
Gazeti la serikali, la kufuta Kata ya Ngorongoro,tunaomba liandikwe Tena gazeti la kutokufutwa kwa kata hiyo.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema ataunda tume mbili, moja itachunguza na kutoa mapendakezo kuhusu masuala ya ardhi yanayolalamikiwa na wakazi wa Ngorongoro na nyingine itaangalia utekelezaji wa uhamaji kwa hiari kutoka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Rais Samia amesema hayo leo Jumapili, Desemba mosi, 2024 Ikulu ndogo ya Arusha alipozungumza na viongozi wa kimila wa jamii ya kimasai (Malaigwanani) wanaoishi eneo la Ngorongoro.

Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kuwasikiliza viongozi hao kutokana na kuwepo malalamiko kuhusu baadhi ya uamuzi wa Serikali kuhusu eneo la Ngorongoro.

Soma Pia: Sakata la Ngorongoro Rais anadanganywa', afike awasikilize Wananchi atabaini uhalisia - Olengurumwa

Pia, amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuimarisha utendaji kazi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya Serikali na jamii hiyo.

Katika hatua nyingine, Rais Samia ameitaka Ofisi ya Rais-Tamisemi kushughulikia changamoto zinazojitokeza, ikiwemo kukosekana kwa baadhi ya huduma za msingi za kijamii katika eneo la Ngorongoro.
Mkaza mwana amegeuka na kuingia kwenye orodha ya watu wasio julikana
 
Back
Top Bottom