Rais Samia Kuzindua Kitabu cha Maisha ya Edward Moringe Sokoine Jijini Dar es salaam

Rais Samia Kuzindua Kitabu cha Maisha ya Edward Moringe Sokoine Jijini Dar es salaam

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Baada ya Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kumaliza ziara yake kwa kishindoo kikuu kilicho itetemesha Nchi Nzima huko mkoani Ruvuma ,ziara ambayo leo ndio mwisho na ambayo ilikuwa ya mafanikio makubwa sana na ambayo ilishuhudia uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo na ambayo ilishuhudia ilihudhuriwa na wananchi wengi kuwahi kutokea katika Historia ya Taifa letu.

Screenshot_20240928-224331_1.jpg
IMG-20240929-WA0000.jpg


Sasa hapo kesho tena Rais wetu atakuwa na kazi nyingine katika jiji la Dar es salaam,jiji la Chalamila,jini la raha na akili,jiji lenye kila aina ya mbwembwe,jiji la burudani,jiji lenye makao makuu ya Yanga na Simba, jiji lenye kila aina ya uwekezaji, jiji linalokujitaji uende na akili tu na siyo nguvu, jiji ambalo ni ndoto ya kila mtanzania kufika na kuosha Macho,jiji ambalo kuishi kwake tu ni sawa na Elimu tosha.

Jiji ambalo wabunge wengine hupotelea huko na kurejea Majimboni wakati wa uchaguzi tu ,jiji ambalo lina kila aina ya stori, jiji ambalo limejaa manabii na watume Wa Mungu.jiji ambalo hakuna habari za kuulizana kabila lako ,jiji ambalo usiende kichwa kichwa kwamba unakwenda kumsalimia fulani maana unaweza kufika mlandizi halafu simu ya mwenyeji wako haipatikani tena hewani na huji kuipata tena hewani.

Ambapo sasa kesho Mama yetu Mpendwa , Mboni ya Taifa ,Mbeba Maono atakuwa na kazi ya kuzindua kitabu cha Maisha ya Hayati Edward Moringe Sokoine.Ambaye huyu alikuwa ni waziri Mkuu wetu aliyefariki kwa ajali ya Gari pale Mkoani Dodoma akitokea katika vikao vya Bunge.

Ambapo stori zinasema kuwa kuna gari liliingilia msafara wake na kwenda kugonga gari yake na hivyo kupelekea kifo chake.stori zinaendelea kusema kuwa Dereva wa gari hilo lililomgonga hayati Sokoine alikuwa ni Raia wa kwa madiba.yaani Afrika kusini.

Kwa hiyo kesho Mama atazindua kitabu hicho kinachoelezea Maisha yake Tangua makuzi yake katika jamii ya kimasai Mpaka pale aliposhika nafasi mbalimbali serikalini ikiwepo ya Uwaziri Mkuu. Pia kingine cha kuvutia ni kuwa eneo la waziri Mkuu huyu lilikuja kutoa Wazuri mkuu Mwingine ambaye naye ni hayati kwa sasa ,hayati Edward Ngoyai Lowassa aliyekuja na kauli mbiu yake ya safari ya Matumaini pamoja na kauli yake ya huwezi kuzuia mafuriko kwa Mkono.

Screenshot_20240929-131944_1.jpg


Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Hicho kitabu kitakuwa kimechakachuliwa na kimebandikwa mastori kabambe ya uongo yenye udanganyifu.

Tunataka zile hadithi za jikoni za ukweli na sio magarasa ya kutuhadaa watanganyika.

Samia tumechoka uongo. Naomba uniteue niwe mkuu wa mkoa wa dar nikunyooshee jiji, chalamila anakudanganya.

Najua chalamila ndio mtunzi wa hicho kitabu.
 
Sokoine alikuwa muadilifu, hakuwa fisadi,muuaji wala mbinafsi. Sasa huyu atazinduaje wakati sifa hizo hana?
Mama ni mtu safi, mzalendo,mcha Mungu, mchapakazi, muadilifu na mwenye kiu ya maendeleo kama aliyokuwa nayo Hayati Sokoine.ndio maana kaalikwa kama mgeni Rasmi.
 
Hicho kitabu kitakuwa kimechakachuliwa na kimebandikwa mastori kabambe ya uongo yenye udanganyifu.

Tunataka zile hadithi za jikoni za ukweli na sio magarasa ya kutuhadaa watanganyika.

Samia tumechoka uongo. Naomba uniteue niwe mkuu wa mkoa wa dar nikunyooshee jiji, chalamila anakudanganya.

Najua chalamila ndio mtunzi wa hicho kitabu.
Wewe njaa inakusumbua tu ndugu yangu😀😀😀
 
Mleta maada Wahamiaji haramu naona nnapambana sana wewe na Kafulila wahamiaji haramu mujaze nafasi ya mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu ambayo haijajazwa

Ile nafasi sio ya kampeni umwambie na Kafulila
 
Mleta maada Wahamiaji haramu naona nnapambana sana wewe na Kafulila wahamiaji haramu mujaze nafasi ya mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu ambayo haijajazwa

Ile nafasi sio ya kampeni unwambie na Kafulila
Unaumia na kuteseka ukiwa wapi huko ndugu yangu mtanzania.
 
Back
Top Bottom