Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
RAIS SAMIA KUZINDUA RASMI ZOEZI LA KUANDIKISHA WAPIGA KURA WA SERIKALI ZA MITAA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atazindua rasmi Zoezi la Kuandikisha Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa mnamo tarehe 11.10.2024 Kijiji cha Chamwino mkoani Dodoma.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohammed Mchengerwa
Bado siku nne (4), Kuelekea Zoezi la Kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.