Rais Samia kwa sasa utakapoweka ruzuku kwenye bei ya mafuta utakuwa umewapa zawadi wafanyabiashara, sio kuwapunguzia Watanzania makali ya maisha

Rais Samia kwa sasa utakapoweka ruzuku kwenye bei ya mafuta utakuwa umewapa zawadi wafanyabiashara, sio kuwapunguzia Watanzania makali ya maisha

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Kutokana na hali kali za maisha zinazotokana na kupanda kwa bei ya mafuta, juzi hapa mama Samia aliondoa tozo ya Shs 100 kwenye bei ya mafuta, na baada ya Bunge kuitaka serikali kuchukua hatua zaidi kutoa nafuu ya bei ya mafuta, Mama Samia alimuagiza January Makamba kutangaza ruzuku ya shilingi bilioni kadhaa ili kupunguza bei ya mafuta. Hatua hii ya ruzuku itaanza hivi karubuni.

Lakini, japo ya nia njema ya mama Samia na serikali yake kuwapunguzia mzigo wa wananchi, hapa WAMEKOSEA SANA na huenda wamepotoshwa na watu wanaojua watanufaika na hi ruzuku. Nitaeleza kwa mfano rahisi sana.

Kwanza, ili ruzuku katika bei ya mafuta ifanye kazi, inatakiwa iwekwe KABLA bei hajizapanda, sio unaweka ruzuku baada ya bei kupanda. Kwa kifupi, ikiwa leo unanunua nyanya sokoni kwa fungu shs 200 badala ya Shs 1500 iliyokuwapo awali kabla ya bei ya mafuta kupanda, usitegemee siku ruzuku ikianza kutumika wafanya biashara watasema jamani eeh, sasa bei ya nyanya inashuka tena kuwa Shs 1500! Hilo halipo.

Hivyo basi, gharama za uchukuzi za mfanya biashara wa nyanya zitapungua kwa sababu bei ya mafuta itapungua, lakini mfanyabiashara huyo hatapunguza bei ya nyanya baada ya kupandisha kuwa Shs 2000 toka Shs 1500. Atakachokuwa amefanya Mama Samia ni kumpa faida mfanya biashara na sio mnunuaji.

Pili, ruzuku hufanya kazi vizuri katika market prices ambazo ziko regulated, yaani kuna taasisi ya kupanga bei. Sasa hili kwa upande wetu Tanzania tulishaliondoa. Bei inapangwa katika mambo machache sana kama nauli, na mengine yote serikali haina mamlaka ya kuzuia kupanda au kushuka bei. Kwa hiyo serikali inaweza kuweka ruzuku kwenye mafuta na bado isisaidie bei za vitu kushuka. Kwa sasa nina mradi wa ujenzi, nilikuwa nikinunua trip ya mchanga kwa Shs 100,000. Jamaa wamepandisha hadi shs 115,000 wakidai bei ya mafuta imepanda. Kukiwa na ruzuku, nani atawaambia hawa watu wa malori ya mchanga watelemshe bei ya trip ya mchanga?

Kwa hiyo Mama Samia, hili la kusema utaweka ruzuku kwenye bei ya mafuta ili kuwapa unafuu Watanzania wala halitasaidia kwa sababu kubwa mbili;

1. Bei za bidhaa zimeshapanda na hazitashuka kwa kuwa umeweka ruzuku katika bei ya mafuta
2. Bei katika sekta nyingi za biashara hazina usimamizi (price regulation or control)

Ruzuku unayotaka kuweka itawafaidisha wafanya biashara, hivyo tafuteni njia mbadala ya kupunguza makali ya maisha. Ruzuku itasaidia kupunguza sana sana bei ya nauli kwa kuwa kuna usimamizi wa viwango vya nauli, lakini sio mambo mengine. Kilio cha Watanzania sio katika nauli za mabasi na daladala tu.
 
Wkt makamba alitutangazi kutoa shilingi Mia kwa kila Lita na kusema kuwa serekali itakuwa Inapoteza shiling billion 30 kwa kila mwezi baadae mam kaja kutangazwa kuwa hiyo Mia irudi kwa kuwa tayari ilikuwa ktk bajeti

Kwa kifuli Sana kuwa Bei ya wese ndio hihi itakayo kuepo na kushuka haitaweza kushuka kamwe had urus asimamishe vita
 
Wkt makamba alitutangazi kutoa shilingi Mia kwa kila Lita na kusema kuwa serekali itakuwa Inapoteza shiling billion 30 kwa kila mwezi baadae mam kaja kutangazwa kuwa hiyo Mia irudi kwa kuwa tayari ilikuwa ktk bajeti

Kwa kifuli Sana kuwa Bei ya wese ndio hihi itakayo kuepo na kushuka haitaweza kushuka kamwe had urus asimamishe vita
Wala usijali hao urus kama ulivyowaita,wanakaribia kusitisha hiyo vita manaake Kichapo wanachokipata toka kwa majeshi shupavu ya Ukraine si cha kawaida,mpaka sasa mrusi ameishapoteza wanajeshi 25,000.
 
Kweli imetokea,Mafuta yameshuka but hakuna kilichoshuka,serikali Ina wanenaji tu,hakuna watendaji😄,serikali imetunishiwa msuli na wafanyabiashara.
 
Back
Top Bottom