Rais Samia: Lengo letu ni maendeleo

Rais Samia: Lengo letu ni maendeleo

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Chuo Kikuu cha Dar es salaam kimemtunuku shahada ya heshima ya Udaktari Rais Samia Suluhu Moja Kati ya sababu iliyokifanya kumtunuku PhD Rais Samia ni juhudi zake za kukuza uchumi wa Tanzania na kuwawezesha wananchi kukuwa kiuchumi.

Lakini Rais Samia Suluhu alipohutubia amesema lengo la kila mtanzania ni maendeleo

"Ninaamini kabisa maendeleo hayawezi kuja bila wananchi kuungana na Taifa kuwa kitu kimoja. Tunaweza kutofautiana mitazamo, lakini sote ni Watanzania wenye lengo moja la maendeleo ya nchi yetu."

Lakini pia aliongeza kuwa Siasa isiwe kila kitu hii inaonyesha ni kwa kiasi gani mama ni mzalendo na siasa sio kipaumbele chake kipaumbele chake ni maendeleo tu "Kila kitu kikizidi kiwango huwa na kasoro na hivyo nikaona madhara ya kuzigeuza siasa kuwa kila kitu ikiwemo kuzifanya kuwa njia ya uchumi.

Hivyo nikahisi kuja na mambo haya manne (4R) tutaweza kulirudisha Taifa kuwa moja." Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu

Serikali ya awamu ya sita ina lengo kubwa la kufanya maendeleo na utekelezaji wa maendeleo unaendelea na ndio maana Rais Saia Suluhu anaimani ya kuwa watanzania tukiungana na tukawa kitu kimoja lazima maendeleo yaonekane kama ilivyo sasa
 
..Ssh hajiamini.

..title ya MAMA ina uzito kuliko PhD.

..nadhani ameona kujiita mama hakumsaidii.

.
 
Back
Top Bottom