Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Rais Samia kuwaongoza waombolezaji kuaga mwili wa William Lukuvi, Viwanja vya Karimjee, leo Machi 28, 2026. Hadi mauti yanamkuta Lukuvi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani.View: https://www.youtube.com/live/y_iXq1YH0ag?is=DwDqptaqYbLwT_3I
=================
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaongoza Watanzania kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Hayati William Vangimembe Lukuvi, huku akisisitiza kuwa taifa limepoteza kiongozi mzalendo na mwalimu wa wengi.
Akizungumza leo, Machi 28, 2026, katika viwanja vya Karimjee mkoani Dar es Salaam, Rais Samia Rais amemwelezea Hayati Lukuvi kama kiongozi aliyekuwa tayari kushirikisha uzoefu wake na wengine. Amesema Lukuvi hakuwa mchoyo wa maarifa, na viongozi wengi waliobahatika kufanya naye kazi wamejifunza mambo makubwa kutoka kwake.
Amesisitiza kuwa katika nafasi zote alizohudumu ndani ya CCM, Serikali, na Bunge, Lukuvi ameacha alama ya utendaji bora ambayo itabaki kuwa darasa kwa viongozi waliobaki.
“Ndugu zangu msiba huu si wa familia pekee bali ni wetu sote Watanzania kwani wengi tulimfahamu, wengine tulibahatika kufanya kazi naye na muhimu zaidi wengi waliguswa na mchango wake kwa namna moja au nyingine kupitia uongozi na utumishi wake wa muda mrefu kwa umma na wa kisiasa”, ameeleza Rais Samia.
Ameongeza kuwa uzoefu na busara za Lukuvi zingekuwa muhimu zaidi katika kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na migongano ya kisiasa na vita, hali iliyochangia kupanda kwa gharama za maisha katika nchi mbalimbali, ikiwemo bei za mafuta.
Amesema busara za Lukuvi zingeweza kusaidia kutoa mwelekeo na mawazo mbadala katika kukabiliana na changamoto hizo, huku akiwataka Watanzania kuendelea kumwomba Mungu ili hali ya amani na usalama irejee katika maeneo yenye migogoro.