Rais Samia, maisha ya vijana kwa sasa hayaridhishi. Nguvu kubwa itumike kubadili mfumo wao wa maisha

Tulikuwa watumwa kipindi cha mwendazake
 
Huyu bibi hafai tena.
Naona anapenda kujionyesha na watu wa nje. Akifikiri wanampenda. Labda kwa vile yeye ni Rais mwanamke.

Waingereza walimtoa Margret Thatcher, waziri wao mkuu mkuku mkuku, sembuse yeye.

Yeye atumie tu uwezo wake kwa maslahi mapana ya nchi yetu. Kupokea mawazo ya kutoka kwa hao caucasians ni kujipotezea mda. Hawana zuri la kufanya kwa nchi yetu. Hawana la maana tena. Huko kwao mambo yanawashinda, sembuse kwetu?
 
Tulikuwa watumwa kipindi cha mwendazake
Kama hujaelewa ulimwengu unakokwenda, endelea tu kumlaumu mwendazake. Mwisho wa siku utakumbuka dhamira yake.

Wayahudi walipiga "cheers" kusulubiwa kwa Yesu. Leo wanatamani angerudi awasamehe makosa yao.

Hivi sasa na rasilimali zetu tunashindwa je tukiwa hatunazo hali itakuwa vipi?
 
Maneno haya unayowaambia wapinzani, waambie pia na Ccm . Kumbuka ni 60 yrs now
 
Mwendazake hakuwa mzalendo mzuri labda kidogo Nyerere. Ingawa naye alituingiza kwenye vita vya ukombozi visizyo na return kwa taifa.
 
Maneno,
Kilimo umekiacha wapi? Yaani kilimo hatuwezi kabisa kukifanya kikawa mwajili mkuu nchi hii,?

binafsi nimeshajarubu kulima lakini ilibidi nitoke huko haraka sana! Kwanini nilitoka,

kwanza lazima uombe kudra ya Mwenyezi Mungu mvua inyeshe.

Pili uvunaji wetu wenyewe unapoteza mazao mengi sana,

tatu wizi, yaani kuibiwa shambani

Nne, hakuna watu wa kukutembelea kukupa ushauri, ni blabla tu, hawajitoi,

usafirishaji wa mazao kutoka shambani mpaka kwenye soko

Nne, namna ya kuyahifadhi hayo mazao baada ya kuvuna mpaka kutaka kuyauza.

Tano, kuibiwa na madalali, maana mnagawana nusu kwa nusu (watu wabaya sana hao),
Sita, pembejeo, bei aghari sana.

kuna mambo mengi sana huko.

lakini nina uhakika kama serikali ikiwa makini kuingiza mkono wake humo sidhani kama kuna kijana atahaingaika kutwa nzima kuuza tochi na sidiria mbili za mtumba huku mjini,

labda nikwsmbie kitu, vijana wa kitanzania ni rahisi sana kuchangamkia fulsa kama inalipa, sio wavivu kama tunavyofikilia ni kwamba hakuna watu wa kuwaongoza wafikie matarajio yao.

nini kifanyike,
NI SERIKALI TU KUINGIZA MKONO WAKO HUKO, kama inacyofanya kununua ndege na kujenga reli.

bila serikali kuingiza pesa huko hakuna mtu binafsi ambaye angewexa kununua ndege za kisasa au kujenga reli ya kisasa kama alivyoamua Baba yetu MAGUFULI
 
Mwendazake hakuwa mzalendo mzuri labda kidogo Nyerere. Ingawa naye alituingiza kwenye vita vya ukombozi visizyo na return kwa taifa.
[emoji23][emoji23][emoji23] Umenifurahisha sana na kunifariji kwa msemo wako " Ingawa naye alituingiza kwenye vita vya ukombozi visivyo na return kwa taifa".

Ni ukweli usiopingika. Lakini itoshe tu kusema zama zile zilikuwa zama za ideologies. Na kila mtu alijaribu to ge a good profile out of it. Lakini leo tuko kwenye era ya technology. Sidhani kama itatusaidia kitu.

Tunashindana kwa concepts nzuri za knowledge na technologies. Tengeneza kitu kinachoweza ku-compete vingevyo umeachwa nyuma.
 
Maneno haya unayowaambia wapinzani, waambie pia na Ccm . Kumbuka ni 60 yrs now
Mimi sina mpango wowote wa kiutikadi ya UCCM wala UCHADEMA. Na ndiyo maana kwenye mada yangu hujanisikia nikigusia au kutoa lawama aidha, kwa CCM wala CDM. Mimi nimemhusisha sana Rais na watendaji wake wa serikali na wataalam au wasomi wetu wenye infuence.

Wana CCM na CDM hawana mamlaka yoyote kwenye utendaji wa serikali na vile vile hawezi kabadili chochote kwenye awamu hii ya sita ambayo imeshaanza. Mamlaka yote yako mikononi mwa Rais mwenyewe na watendaji wake na wao ndiyo wenye uwezo wa kubadili mwelekeo wa maisha kwa utendaji wao in a short term.
 
Maneno haya unayowaambia wapinzani, waambie pia na Ccm . Kumbuka ni 60 yrs now
60 years of what? JK Nyerere alipochukua nchi kulikuwa hakuna wasomi wa Kitanzania, walikuwa wanahesabika. Mlaumuni Mwinyi, Mkapa na Kikwete, walifanya nini wakati wao. Mwinyi mzee rukhsa, Mkapa aliuza viwanda vyote alivyoanzisha Nyerere, Kikwete alifilisi kwa miradi fake na wauza unga walishamiri etc. Wahukumuni waliotufikisha hapa bila kumung'unya maneno. SSH Kikwete part 2.
 
Nyerere lazima alaumiwe. Kwa maneno yake mwenyewe (mwl) alinukuliwa baada ya kustaafu kuwa "KATIBA YETU NI MBAYA INAWEZA KUMFANYA KIONGOZI KUWA DICTATOR" Je alifanya juhudi zipi kuhakikisha anaiacha katiba nzuri kwa watu wote ?! Tunajua amekufa akiwa bado na nguvu serikalini na chamani. Ameacha leo ma dictators wanaitumia kuumiza walio tofauti nao kimawazo.

Kuhusu mambo ya viwanda na uchumi alijitahidi, lakini kosa lake likawa kuingiza nchi katika vita visivyo na return . Lazima uchumi uporomoke . (Kusini mwa Africa , Seashell, Uganda nk)
 
Elimu ya uzazi wa mpango ipewe kipaumbele tena. Watu wasizae kupitiliza hata kama elimu ni bure.
 
Atalaumiwa mpaka mwisho wa Dunia aliyoyaleta Tanzania kwa kichwa chake yeye hayakuwahi kuwapo tangu zama za ukoloni,labda enzi za Utumwa wa Waarabu.
 
Kubishana na wewe ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.
 
Kwangu ninaamini Jana Ni njema kadhalika na leo, lakini kesho ni Bora zaidi. Lakini pia kesho Bora huundwa na leo.
Aisee, mkuu imebidi nisome tena mchango wako wa hoja. Unahekima kubwa sana. Sentesi yako ya mwisho nimeipenda sana!👍
 
Mkuu uwezi kusema jambo lolote linaloikumba nchi hii kwa sasa ukawasahau CCM na siasa kwa ujumla kwasababu ata Rais uliyempa hizo nondo apo juu anafata ilani ya chama......
 
Aisee, mkuu imebidi nisome tena mchango wako wa hoja. Unahekima kubwa sana. Sentesi yako ya mwisho nimeipenda sana!👍
Motivational speaker nimepitia bandiko lako namba moja lote kwa uzuri. Nilichokiona kwako ni kuandika mambo mengi ya kila unachokiwaza, ndio maana umechanganya mambo mengi kwa wakati mmoja. Nilitarajia kama ni ajira kwa vijana ndio lilikuwa lengo lako utaje njia halisi ya kuzipata, lakini umeishia kutaja data sijui za deni ama hata idadi ya watu ambazo sio sahihi.

Mwisho umeishia kumsifia Magufuli, lakini Magufuli alitengeneza ajira kiasi gani kwa vijana wala hujataja! Na hata ukiangalia kiwango cha ajira kwenye utawala wake kilishuka zaidi, na yeye amechangia sana uwepo wa hizi ajira za uchuuzi, kuliko uzalishaji kwa kuruhusu biashara holela ya uchuuzi. Pitia miji ilivyochafuka sasa hivi kwa uchuuzi, huku akiwa ameweka karibu 2t kwenye ndege zisizo na tija. Amewekeza 6.5t kwenye umeme wa maji, wakati kuna bomba la gas hapa Dar, na uzalishaji umeshaanza. Kwanini hakuongeza 2t kwenye gas iliyo tayari, na hizo 4.5t akawekeza kwenye kilimo na viwanda? Kajenga daraja la Busisi litakalokula 700b, kwanini asingenunua vivuko vinne vya 50b@, kisha 500b akajenga viwanda hata kumi vya 40b@ vya kuchakata pamba huko kanda ya Ziwa, kisha hela inayobakia kama 100b itumike kuinua zao la pamba, vijana waondoke mjini maana kilimo cha pamba kingekuwa. Huyo Magufuli kapora 200b za mfuko wa korosho kwenda kununua ndege isiyo na tija, sasa hivi kilimo cha korosho kimezubaa, halafu unampa sifa za kijinga mtu aliyeua ajira za vijana, na kuruhusu biashara holela za uchuuzi hapa mjini!

Kama unazungumzia ajira za vijana taja njia halisi, na sio hizo nadharia zako za kutaja vitu vingi vya mara sijui chuma, sijui majina ya wazungu na blabla kibao. Solution ya kweli kwa ajira za vijana hapa nchini ni kilimo kwanza, kisha viwanda kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa. Hii ni iwapo unazungumzia ajira za vijana. Kilimo pekee ndio kitaondoa vijana mjini kama serikali itawekeza nguvu huko, kisha uzalishaji ukikua automatically viwanda vitafuata malighafi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…