Rais samia: Majeshi yataongezewa fedha katika bajeti ijayo ili wasijikite kwenye shughuli za uzalishaji

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 wameongeza fedha kwa majeshi ya Ulinzi na Usalama ili wapunguze muda wanaotumia kushughulika na shughuli za uzalishaji.

Rais amesema hayo alipokuwa Msalato, Dodoma akizindua Kiwanda cha Samani cha Jeshi la Magereza ambapo amesema shughuli za uzalishaji zinapunguza muda wa majeshi kujikita kwenye shughuli za medani.

Aidha amewataka Wakuu wa Majeshi Nchini kujifunza kutoka kwa majeshi mengine duniani namna ambavyo wanajihusha na shughuli za uzalishaji bila kuathiri shughuli zao za msing.
 
Ni kweli, bora majeshi yaunde "Suma JKT" zao ili wasipoteze focus. Uzalishaji kama kuna long term plan si jambo dogo na linaweza kumfanya hadi mkuu wa jeshi muda mwingi kutupia jicho huko.

Hapa mama ameupiga mwingi [emoji123]
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kwa bajeti yam waka wa fedha 2022/23 wameongeza fedha kwa majeshi ya Ulinzi na Usalama ili wapunguze muda wanaotumia kushughulika na shughuli za uzalishaji

Rais amesema hayo alipokuwa Msalato, Dodoma akizindua Kiwanda cha Samani cha Jeshi la Magereza ambapo amesema shughuli za uzalishaji zinapunguza muda wa majeshi kujikita kwenye shughuli za medani.

Aidha amewataka Wakuu wa Majeshi Nchini kujifunza kutoka kwa majeshi mengine duniani namna ambavyo wanajihusha na shughuli za uzalishaji bila kuathiri shughuli zao za msing.
Asilisahau na jeshi la mgambo, ili liongeze tija kwenye kuwaonea wamachinga kwa kuwapora mali zao
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kwa bajeti yam waka wa fedha 2022/23 wameongeza fedha kwa majeshi ya Ulinzi na Usalama ili wapunguze muda wanaotumia kushughulika na shughuli za uzalishaji

Rais amesema hayo alipokuwa Msalato, Dodoma akizindua Kiwanda cha Samani cha Jeshi la Magereza ambapo amesema shughuli za uzalishaji zinapunguza muda wa majeshi kujikita kwenye shughuli za medani.

Aidha amewataka Wakuu wa Majeshi Nchini kujifunza kutoka kwa majeshi mengine duniani namna ambavyo wanajihusha na shughuli za uzalishaji bila kuathiri shughuli zao za msing.
Hapa mama amekosea, au labda si msomaji au mfatiliaji...

Binadamu huendelea Kijamii au kiteknolojia kwa sababu ya vita ambayo husabisha maendeleo jeshini...

Kuna msemo unasema Enrich the Army Enrich the country.

Ukitaja nchi zote tajari Duniani kuanzia USA, Europe, Israel e.t.c maendeleo Yao yanaanzia Jeshini kuanzia tafiti Hadi implementation zote...

We need to give our armies such kinds of challenges and not to stop them. Mfano kipindi Cha Corona Hadi Sasa hakuna response ya kitaalam ya Majeshi yetu Kwa sababu hawana aina hii ya wataalaam au focus, Jeshi letu sidhani kama Ina Ina yoyote ya rapid response kama ikitokea Hatari ya kukosekana kwa hydrocarbons.

Samia ni mweupe sana kichwani
 
Ila akili zetu zinatofautiana sana, badala ya majeshi yetu yaongeze uzalishaji na kuwafanya waipunguzie serikali mzigo wa kuwalea ili hiyo pesa ipelekwe pengine, Samia ndio anawafanya wazidi kuwa wazembe.

Ningeielewa hiyo hoja ya Samia kama nchi yetu ingekuwa vitani wanajeshi hawana muda wa kuzalisha, lakini sio kwa hawa wanajeshi wetu wenye vitambi wasioweza hata kukimbia.

Muhimu hizo tenda wakizitoa wasitoe kwa upendeleo, vinginevyo itakuwa ni kazi bure mzunguko wa pesa utaendelea kubaki kwa watu walewale, hii itakuwa ni sawa na kuhamisha tatizo badala ya kulimaliza.

Tusipokuwa makini hili wazo alilotoa Samia leo litaturudisha kule kwa kina Manji kuliuzia jeshi letu sare, hiki ni kichaka cha upigaji toka kwa kikundi fulani na inawezekana hilo wazo kapenyezewa na mwanakikundi aliyeko kwenye serikali yake nae akalibeba tu.
 
Mama hongera Kwa kuliona Hilo Yani Sasa hivi majeshi yamebadirika kuwa kampuni za biashara Hadi ndani ya makambi Kuna miradi na biashara mbalimbali. Yani ni uozo
Dunia ya kwanza majeshi ndio hutumikaa kugundua na kuvumbua kila kitu.
 
Kwa hiyo hiyo Dunia ya kwanza hayo majeshi yanafanya hizo shughuli uraiani au ndani huko kwenye ishu zao?

Kazi ya majeshi sio kusomba korosho wala kuuza vitalu sijui kusogeza kokoto site.
 
Ila akili zetu zinatofautiana sana, badala ya majeshi yetu yaongeze uzalishaji na kuwafanya waipunguzie serikali mzigo wa kuwalea ili hiyo pesa ipelekwe pengine, Samia ndio anawafanya wazidi kuwa wazembe.

Ningeielewa hiyo hoja ya Samia kama nchi yetu ingekuwa vitani wanajeshi hawana muda wa kuzalisha, lakini sio kwa hawa wanajeshi wetu wenye vitambi wasioweza hata kukimbia.

Muhimu hizo tenda wakizitoa wasitoe kwa upendeleo, vinginevyo itakuwa ni kazi bure mzunguko wa pesa utaendelea kubaki kwa watu walewale, hii itakuwa ni sawa na kuhamisha tatizo badala ya kulimaliza.
Hiyo Kazi ni ya magereza na JKT sio hao wengine
 
Hapa mama amekosea, au labda si msomaji au mfatiliaji...

Binadamu huendelea Kijamii au kiteknolojia kwa sababu ya vita ambayo husabisha maendeleo jeshini...

Kuna msemo unasema Enrich the Army Enrich the country.

Ukitaja nchi zote tajari Duniani kuanzia USA, Europe, Israel e.t.c maendeleo Yao yanaanzia Jeshini kuanzia tafiti Hadi implementation zote...

We need to give our armies such kinds of challenges and not to stop them. Mfano kipindi Cha Corona Hadi Sasa hakuna response ya kitaalam ya Majeshi yetu Kwa sababu hawana aina hii ya wataalaam au focus, Jeshi letu sidhani kama Ina Ina yoyote ya rapid response kama ikitokea Hatari ya kukosekana kwa hydrocarbons.

Samia ni mweupe sana kichwani

Nakubaliana na wewe in a way
Kweli wanajeshi wana mambo mengi ya kuvumbua kwa kuendana na nchi na usalama wetu

Technology nyingi leo tuanzitumia wao wanajeshi nchi tajiri walizijua miaka hata 60 au zaidi nyuma
Mifano hata mobile phones, night vision na mengine

Ila sasa sisi wanajeshi wetu ni tofauti hawavumbui kitu bali wanatumikishwa tu, Kwa mfano Magereza wao utakuta askari anasimamia wafungwa wakilima mashamba binafsi au kukata miti wengine wakiwa wajenzi
Je kweli tunahitaji wajenzi jeshini?

Basi wajenge hata madaraja ya chuma na kuwauzia hata nchi za Jirani labda

Ni mfano tu maana hiyo iko karibu na uhitaji wa Jeshi

Huenda siko sahihi ila ni mtazamo tu
 
Nakubaliana na wewe in a way
Kweli wanajeshi wana mambo mengi ya kuvumbua kwa kuendana na nchi na usalama wetu

Technology nyingi leo tuanzitumia wao wanajeshi nchi tajiri walizijua miaka hata 60 au zaidi nyuma
Mifano hata mobile phones, night vision na mengine

Ila sasa sisi wanajeshi wetu ni tofauti hawavumbui kitu bali wanatumikishwa tu
Kwa mfano Magereza wao utakuta askari anasimamia wafungwa wakilima mashamba binafsi au kukata miti wengine wakiwa wajenzi
Je kweli tunahitaji wajenzi jeshini?

Basi wajenge hata madaraja ya chuma na kuwauzia hata nchi za Jirani labda
Ni mfano tu maana hiyo iko karibu na uhitaji wa Jeshi
Huenda siko sahihi ila ni mtazamo tu
Hizi unazosema ndio kazi za Uzalishaji, Serikali inatakiwa iwaongezee pesa wawe na uwezo wa kushindana na si kuwazuia
 
Akumbuke pia nyongeza mishahara kwa wafanyakazi Mei Mosi hii asiuchune tena.
 
Mama hongera Kwa kuliona Hilo Yani Sasa hivi majeshi yamebadirika kuwa kampuni za biashara Hadi ndani ya makambi Kuna miradi na biashara mbalimbali. Yani ni uozo
Hawa tunawalipa salary wanahangaika na ujasiriamali matokeo yake tukivamiwa wanaanza kututanguliza eti wanaume wote vitani wakati wenye kiapo na tunaowalisha kwa Kodi zetu wapo na tuliwafindisha.
 
Back
Top Bottom