denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,509
- 68,228
Haya mambo mnayafikiria kwa upeo mdogo sana, jeshi kwa nafasi yake wana uwezo mkubwa wa kuzalisha kwa wingi na bidhaa zao zikawa bei nafuu kwasababu wana man power ya kutosha, na skilled personnel, hawa watalipwa kwa mishahara yao ile ile wanayolipwa wakiwa kama waajiriwa wa jeshi.Hatua gani tunarudi hapa? Hivi Kazi ya jeshi ni kubeba korosho na kushona viatu?
Bora wawe busy na mambo yao ya ndani ikiwemo kuzalisha zana zao wenyewe.
Lakini unapopeleka shughuli kama hizi kwa watu wa nje, kwanza kuna ukiritimba, hizo tenda huko CCM watatoa kwa upendeleo mpaka wahusika wahongwe.
Hawa wahongaji nao lazima watakuja kufidia gharama hizo kwenye mauzo ya bidhaa zao, lakini pia issue ya man power, kuwaajiri wafanyakazi lazima mishahara yao itoke kwenye mfuko wa muajiri, hili nalo litachangia kuongeza bei ya bidhaa.