BUCHANAGANDE
JF-Expert Member
- Sep 8, 2011
- 1,512
- 480
Salaam katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
Mheshimiwa Rais naomba nikujulishe kuwa ile pesa Milioni kumi na sita (16,000,000/=) ulizotoa kwa kila Wilaya Kwa Makatibu Tawala ili wanunue FANICHA katika Nyumba wanazoishi wengi wao hawajanunua Fanicha kama lengo la fedha hizo lilivyo na hivyo wamezitafuna kwa raha zao.
Cha kushangaza wengine umewatumbua na wameondoka vituoni walikokuwa pasipo kununua Fanicha hizo na kusababisha uliowateua kukuta Fanicha zilizochoka vibaya sana.
Kwa sababu Mh. Rais una vyombo vyako ni bora uvipatie kazi ya kuhakiki kama Fanicha zimenunuliwa maana hatuwezi kukaa kimya wakati watu wachache wanahujumu malengo ya pesa za Serikali.
Naomba wazitapike pesa hizo na kama ikiwezekana napendekeza wakatwe katika mishahara yao maana walishazila.
Naomba kuwasilisha.