Rais Samia: Mikopo ya Wahisani ina Riba kubwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais Samia Suluhu Hassan amewaambia watanzania kwa sasa wahisani hawaleti misaada nchini, wanataka biashara ili kugawana faida

Amesema kwa sababu hiyo ni lazima tujinyang'anye wenyewe ili kufadhili miradi ya nchi hii

Ameyasema hayo alipokuwa Tegeta akisalimia wananchi akiwa katika safari ya kuelekea Bagamoyo kutengeneza filamu ya kuitangaza Tanzania

======

RAIS SAMIA: MIKOPO INA RIBA KUBWA

Rais Samia Suluhu Hassan amesema mikopo ina riba kubwa na misaada imepungua, hivyo ni lazima wananchi kujichanga ili kujenga nchi

Amesema ni heri kuchukua mikopo kidogo kufadhili miradi mikubwa kama ya reli na umeme

Ameyasema hayo alipokuwa Zinga mkoani Pwani akielekea Bagamoyo
 
Rais Samia Suluhu Hassan amewaambia watanzania kwa sasa wahisani hawaleti misaada nchini, wanataka biashara ili kugawana faida

Amesema kwa sababu hiyo ni lazima tujinyang'anye wenyewe ili kufadhili miradi ya nchi hii

Ameyasema hayo alipokuwa Tegeta akisalimia wananchi akiwa katika safari ya kuelekea Bagamoyo kutengeneza filamu ya kuitangaza Tanzania
Kwani wale wa Danish ambao ni wahisani wakubwa kabisa wanaofunga ubalozi wao nchini walitoa sababu gani? Sidhani kama hii kauli ina ukweli. Waseme tu hawawezi kufuata demokrasia. Wahisani wana masharti ambayo wanahofia yatawapoka madaraka na hivyo kunyang’anywa tonge mdomoni.

Wanaona ni bora kuendelea kukamua ng’ombe aliyekonda na wao waendelee na ma viete yao wakitafuna keki ya Taifa kwa kupokezana.
 
Kwani wale wa Danish waliofunga ubalozi walitoa sababu gani? Sidhani kama hii kauli ina ukweli. Waseme tu hawawezi kufuata demokrasia. Wahisani wana masharti ambayo wanahofia uatawapoka madaraka na hivyo kunyanh’anywa tonge mdomoni. Bora kuendelea kukamua ng’ombe aliyekonda na wao waendelee ma viete yao wakitafuna keki ya Taifa kwa kupoteza a.
Well said ndiyo hiki kinatutafuna
 
Kumbe siyo tozo tena ni unyang'anyi, anyway lazima maviieite ya waheshimiwa yatembee yakiwemo ya kile chama chakavu ambao hawatumii gari zaidi ya VIIEITE............
 
Hayo ndo madhara ya uchumi wa Kati.
Halafu ndo ingekuwa kweli ni Uchumi wa kati walau inge make a sense.....lakini sio uchumi wa kati ya "Ripoti za Ki-Nadharia" za kubumba🙂....Ni viini macho na ndio maana WaTanzania wanateseka sasa.

Maana ukishaingia uchumi wa kati nchi inakuwa hai-qualify hata kufaidika na mipango kuinua uchumi kama vile AGOA na Millennium Challenge etc mfano mdogo tu kwa upande wa US
 
Tuliaminishwa sifa za kijinga kabisa
 
Shida siyo uchumi wa kati, shida ni democrasia ambayo CCM hawataki kufuata masharti ya wahisani
 
Kwani wale wa Danish ambao ni wahisani wakubwa kabisa wanaofunga ubalozi wao nchini walitoa sababu gani? Sidhani kama hii kauli ina ukweli. Waseme tu hawawezi kufuata demokrasia. Wahisani wana masharti ambayo wanahofia yatawapoka madaraka na hivyo kunyang’anywa tonge mdomoni.

Wanaona ni bora kuendelea kukamua ng’ombe aliyekonda na wao waendelee na ma viete yao wakitafuna keki ya Taifa kwa kupokezana.
Walisema wanannagalia nchi fukara zaidi acha upitoshaji eti demokrasia ,hivi nyie bavicha akili zenu huwa ziko rikizo

USSR
 
Back
Top Bottom