Rais Samia: Mikopo ya Wahisani ina Riba kubwa

Wangekuwa na akili wangezeuza rasilimali zetu kuwa pesa na miradi yote ingefanyika bila hata ya kuwaibia wananchi.
lakini kwakuwa hawana akili basi njia rahisi ya kupata pesa ni kuzichukua pesa zilizo kwenye mzunguko ili ufukara uenee zaidi kwa wananchi
 
Halafu utasikia baadhi ya watu humu hawataki kukiri kuwa Samia ni kiongozi wa ajabu, wanataka makosa ya Samia yabebwe na watu wengine licha ya yeye mwenyewe kujipambanua kila mara

Utasikia " Tatizo kuna watu fulani serikali (Sukuma gang) ndo wanamharibia mama kwa wananchi"

Ukweli ni kwamba,hakuna cha kundi wala nini , ni yeye mwenyewe ndo master plan wa yote yanayoendelea.

Ifike mahalo watu tutoke kwenye denial mode, tukubali tu kuwa tuna miaka minne au tisa ya kuchakarika kwelikweli.
 
kuliko waliochukua benki za biashara?
 
Kwahiyo mkopo wa Trillion 2 ni mdogo?
 
Unajua hata kipindi cha mwanzo cha utawala wa Magufuli watu walikuwa wanasema JK anaongoza nchi kutokea Msoga kwamba et Magufuli alikuwa kama remote tu, ila baadaye wajaachana hizo story hivyo na sasa itafika muda wataacha hizi story za sukuma gang.
 
WaTanzania tuache tabia ya kupenda kuwa Tegemezi. Hakuna mtu anayemthamini masikini, hasa masikini asiyekuwa na ndoto ya kujikomboa katika hali yake. Wenyewe mmesikia mahela yaliyokusanywa kipindi hiki kifupi cha tozo za miamala ya simu. Tukijipanga tunaweza sio kusubiri hela za wafadhili tu, ambazo zinatolewa na masharti mengi - kama vile haki za mashoga nakadhalika. Marehemu JPM alisema mara nyingi - nchi hii siyo maskini. Serikali ikijipanga vizuri , matumizi mazuri ya pesa za serikali na kila mtanzania kulipa kodi- tutafika mbali. Nchi kama Denmark- wananchi wao wanalipa kodi kwa asilimia kubwa sana. Hapa kwetu ni asilimia ndogo sana ambao wanalipa kodi stahiki.
 
Mkuu unataka tuendelee kuwategemea wahisani mpaka lini?
 
Kasi ya kuwaaminisha watanzania kuwa tozo zao ndio zinazojenga nchi ingeenda sambamba na kuwakemea watendaji wa serikali ambao ni wabadhirifu wa pesa za uma basi ingekuwa vyema sana.
 

Lazima tunyang'anyane? Je na vigogo kwenye kunyang'anywa?
 
Ni bora kuwa honest na kuzungumza ukweli kama huu kuliko kutupiga sound

Tunataka kuona na wewe rais ukifanya marekebisho ya sheria na katiba ili mshahara wako ukatwe kodi. Haikubaliki kuwa sisi tuwe ndo wakatwa kodi halafu wewe ni mtumiaji tu, huo ni unyonyaji
 
Mkuu unataka tuendelee kuwategemea wahisani mpaka lini?

Kwani ile mkopo wa kipindi cha Corona usiokuwa na riba wenye kuanza kulipwa baada ya miaka 10 wenzetu walipata na sisi ikawaje vile?
 
Kasi ya kuwaaminisha watanzania kuwa tozo zao ndio zinazojenga nchi ingeenda sambamba na kuwakemea watendaji wa serikali ambao ni wabadhirifu wa pesa za uma basi ingekuwa vyema sana.

Pia ingekuwa across the board na pia kupunguza gharama za serikali
 
Kwani kuna ubaya kama tukiacha kuwa tegemezi na kuwekeza zaidi kwenye biashara ya resources tulizonazo? Kazi ni kuweza kufanya watanzania wengi wawe wazalishaji wa vitu vya kibiashara na waweze kunufaika nazo.
Kwa hilo la lujitegemea Mama hana makosa. Yuko sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…