MZEE CHAKA
Member
- May 27, 2021
- 87
- 141
Kama Raisi Samia anaona mikopo ya wahisani inaumiza kwa kuwa na riba kubwa, alinganishe riba wanazotoza wahisani na riba zinazotozwa na benki hapa nchini, labda hiyo itamfanya aelewe kwa nini Watanzania tunashindwa kuchukua mikopo toka benki zetu nchini.===
RAIS SAMIA: MIKOPO INA RIBA KUBWA
Rais Samia Suluhu Hassan amesema mikopo ina riba kubwa na misaada imepungua, hivyo ni lazima wananchi kujichanga ili kujenga nchi
Amesema ni heri kuchukua mikopo kidogo kufadhili miradi mikubwa kama ya reli na umeme.
Ameyasema hayo alipokuwa Zinga mkoani Pwani akielekea Bagamoyo
Na ni mikopo mingapi huwa wanatuambia wakiipokea? Na wanapoipangia matumizi wanatuonyesha mahesabu yake yamekwendaje? Mkuu ubarikiwe umeuliza swali fikirishi sana na lakugusa ndani kabisa.Kwani wale wa Danish ambao ni wahisani wakubwa kabisa wanaofunga ubalozi wao nchini walitoa sababu gani? Sidhani kama hii kauli ina ukweli. Waseme tu hawawezi kufuata demokrasia. Wahisani wana masharti ambayo wanahofia yatawapoka madaraka na hivyo kunyang’anywa tonge mdomoni.
Wanaona ni bora kuendelea kukamua ng’ombe aliyekonda na wao waendelee na ma viete yao wakitafuna keki ya Taifa kwa kupokezana.
Siyo kweli. Kwa mfano, Swaziland/Eswatini iko kwenye kundi la uchumi wa kati miaka kadhaa kabla ya Tanzania lakini imefaidika sana na mpango wa AGOA. Tukiri tu kwamba tuna viwanda vichache vinavyozalisha bidhaa zenye viwango vya kukubarika kwenye soko la Marekani na mataifa mengine ya Ulaya. Tukitambua udhaifu wetu ndipo tutakapoweza kubuni mikakati, mbinu na mipango ya kujinasua, siyo porojo.Halafu ndo ingekuwa kweli ni Uchumi wa kati walau inge make a sense.....lakini sio uchumi wa kati ya "Ripoti za Ki-Nadharia" za kubumba🙂....Ni viini macho na ndio maana WaTanzania wanateseka sasa.
Maana ukishaingia uchumi wa kati nchi inakuwa hai-qualify hata kufaidika na mipango kuinua uchumi kama vile AGOA na Millennium Challenge etc mfano mdogo tu kwa upande wa US
Nahisi kama vile Mama kavuta mkwanja.Kwani ile mkopo wa kipindi cha Corona usiokuwa na riba wenye kuanza kulipwa baada ya miaka 10 wenzetu walipata na sisi ikawaje vile?
Hilo la kujitegemea litawezekana vipi kwa utaratibu tulio nao? Nini haswa kitakuwa kimebadilika kama viongozi ni wa chama kile kile na mentality ile ile?Kwani kuna ubaya kama tukiacha kuwa tegemezi na kuwekeza zaidi kwenye biashara ya resources tulizonazo? Kazi ni kuweza kufanya watanzania wengi wawe wazalishaji wa vitu vya kibiashara na waweze kunufaika nazo.
Kwa hilo la lujitegemea Mama hana makosa. Yuko sahihi.
Ngoja asimamishe uchumi wake kwanzaNahisi kama vile Mama kavuta mkwanja.
alafu anasema eti anasimamaisha uchumi kwanza 🤣Hilo la kujitegemea litawezekana vipi kwa utaratibu tulio nao? Nini haswa kitakuwa kimebadilika kama viongozi ni wa chama kile kile na mentality ile ile?
Utofauti wa upatikanaji wa pesa bado siyo solution ya kuwa na vision. Wahisani hawasikilizwi, wananchi hawaikilizwi.
Amesema mkuu, mchana kweupe, video ipo humu ”siasa za CCM-Tanzania haziwezi kukubali kufuata mashariti ya WAFADHILI /MABEBERU.”Waseme tu hawawezi kufuata demokrasia. Wahisani wana masharti ambayo wanahofia yatawapoka madaraka na hivyo kunyang’anywa tonge mdomoni.
Kabisa kabisa,Ukisema uwafuatilie hawa watu waweza kuugua akili
Tena ni afadhali pesa za wahisani huwa wanabanwa kuhusu demokrasia nk. Za wananchi ndiyo hata hawatojali hata kidogo. Almuradi kuna polisi na wananchi hawaruhusiwi kuhoji lolote. Na pia kuwa na tume na katiba mbovu, vitu ambavyo ni nyenzo zao za kubakia madarakani. Hakuna lolote mwananchi analoweza kufanya hata wakitumia hizo pesa wanazotunyonya vibaya kiasi gani.Na ni mikopo mingapi huwa wanatuambia wakiipokea? Na wanapoipangia matumizi wanatuonyesha mahesabu yake yamekwendaje? Mkuu ubarikiwe umeuliza swali fikirishi sana na lakugusa ndani kabisa.
mambo kama haya unawaambia waendesha bodaboda watakuelewa kweli? waambie kuhusu kupunguza kuteswa na halmashauri, kupunguza ushuru ili wafanye shughuli zao bila kubughudhiwaRais Samia Suluhu Hassan amewaambia watanzania kwa sasa wahisani hawaleti misaada nchini, wanataka biashara ili kugawana faida
Amesema kwa sababu hiyo ni lazima tujinyang'anye wenyewe ili kufadhili miradi ya nchi hii
Ameyasema hayo alipokuwa Tegeta akisalimia wananchi akiwa katika safari ya kuelekea Bagamoyo kutengeneza filamu ya kuitangaza Tanzania
===
RAIS SAMIA: MIKOPO INA RIBA KUBWA
Rais Samia Suluhu Hassan amesema mikopo ina riba kubwa na misaada imepungua, hivyo ni lazima wananchi kujichanga ili kujenga nchi
Amesema ni heri kuchukua mikopo kidogo kufadhili miradi mikubwa kama ya reli na umeme
Ameyasema hayo alipokuwa Zinga mkoani Pwani akielekea Bagamoyo
Tungekuwa na viongozi makini, tayari ungekuta tumeshaacha kuwategemea wahisani. Tatizo la kusema hatutaki kuwategemea wahisani ni kwasababu wanajuwa kuwa wameshindwa kuondoa umasikini na kufuta ujinga. Wanaogopa Demokrasia itasababisha washindwe kujibu maswali magumu na hivyo uwezekano wa kuondolewa madarakani unakuwa mkubwa.Mkuu unataka tuendelee kuwategemea wahisani mpaka lini?