JERUSALEM 2006
JF-Expert Member
- Apr 23, 2012
- 527
- 596
Mhe, Rais, Mhe. Palagamamba M.A. Kabudi waziri mwandamizi katika serikali yako mwaka 2012/13 katika viunga vya Nkurumah Hall chuo kikuu cha Dar Es Salaam, alitoa ushauri huu juu ya katiba Mpya,
Mhe. Rais, Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, na kiongozi mwandamizi katika serikali yako na sasa ni Mbunge wa kuteuliwa na wewe, Mhe. Bashiru A. Kakurwa alipata kunena haya juu ya hitaji la katiba mpya.
Mhe. Rais sitaki kukupangia wala kukulazimisha. Kwa maneno yao wenyewe waliona hitaji la katiba mpya kabla hawajawa na madaraka, baada ya kuyapata midomo yao imefungwa.
Nipende kukuhakikishia Mhe. Rais umezungukwa na wanafiki wa kiwango cha Jupiter kwenye chama chako, hakuna kiongozi ndani ya CCM kwa sasa atakayeona umuhimu wa Katiba Mpya, lakini pindi mtakapomaliza madaraka yenu na mkarithiwa na viongozi sampuli ya Jiwe ndio mnakumbuka umuhimu wa katiba mpya.
Mama kwa sasa mpini uko kwako, wembe unao wewe mama na uchaguzi ni wako wengine tutabaki kukushauri tu.