Rais Samia na Demokrasia ya utawala kwa majadiliano na maafikiano

Rais Samia na Demokrasia ya utawala kwa majadiliano na maafikiano

rmajani

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
530
Reaction score
525
Utawala wa demokrasia ni utawala wa majadiliano na maafikiano, sio utawala wa amri.na sio utawala wa imla, sisi sote tunajua watu wamegawanyika au wametofautiana katika mawazo na fikira.hakuna kisima cha jumuiya cha kuchota mawazo na fikira za jumuiya.

Hwa hiyo mgawanyiko wa fikira ni lazima, lkn pia mgawanyiko haujengi maendeleo, mgawanyiko lazima uungane ili kuleta maendeleo ya pamoja,watu wasipoungana kwa mawazo na fikira, hawawezi kufanya kitu chochote kwa pamoja. Hawawezi kuwa taifa moja,sasa je muungano wa mawazo na fikira hufanywa kwa njia gani?

Hakika kabisa sio kwa bunduki na risasi, sio kwa amri na sio kwa imla, bali kwa MAJADILIANO,baada ya majadiliano hufuata uamuzi wa pamoja, uamuzi wa pamoja ndio muungano wa mawazo na fikira ambazo labda ziligawanyika kabla ya majadiliano.

Lazima binadamu wakae kitako kujadili na kuunganisha mgawanyiko wa mawazo na fikira, baada ya majadiliano na baada ya hoja kwa hoja, matokeo ndio uamuzi wa pamoja.

Ndiyo muungano. Majadiliano tu ndiyo tanuru la kuyeyusha na kuunganisha mawazo na fikira zilizotofautiana.

Inapotokea mtu ndani ya vyama vyetu vya siasa kwa lugha mama yetu Rais Samia wahafidhina wanataka kuzuia haya majadiliano ni kuzuia MUUNGANO, kwa kawaida demokrasia ni utawala wa watu wenyewe ambao hugawanyika katika mawazo na fikira lakini papo hapo wenye kuungana katika mawazo na fikira.

Mama Samia Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anataka kutuonyesha kama nchi kuwa demokrasia ina misingi yake na misimamo yake ambayo ni utawala wa wananchi wenyewe, utawala wa kushiriki, utawala wa uwakilishi, utawala wa uchaguzi, utawala wa haki sawa, utawala kwa majadiliano na maafanikio na utawala unaolinda uhuru wa mtu binafsi, lakini ndani ya vyama vyetu hawataki haya yanayoendelea, wanasema demokrasia inachelewesha maendeleo ya nchi, kwamba mambo muhimu ya nchi hayawezi kutendeka kwa haraka mpaka wengi wajadili, waamie na kukubali, tunataka Maendeleo ya maisha ya watu wote, na hili ndo linalokwenda kutokea ndani ya utawala huu wa awamu ya 6 chini mama Samia Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
 
Kabisa. Nami ni muumini wa democracy. Kwa umoja wa kitaifa ni muhimu sana. Kuliko kubagua watu na kutengeneza uaduhi ndani ya nchi moja kisa tofauti za mitazamo. Huo ni ushamba na ulozi kama kawaida. Tudumishe democrasia ndo upendo na umoja wa kitaifa.
 
Back
Top Bottom