Kwa heshima kubwa nakusalimu mama yetu Mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania, nakupa pongezi kwa mambo makubwa unayoyafanya kwa maslahi ya taifa hili.
Mama mpira wa miguu sehemu nyingi duniani umefanikiwa kuleta maridhiano, upendo na umoja hata kama kulikuwa na vita mfano Liberia na Ivory Coast. Mahasimu wa kisiasa kwenye ufuasi wa mpira husahau tofauti zao na kuwa kitu kimoja.
Kitendo cha kuwaunga mkono kwa hamasa na pesa maarufu kwenye goli la mama imekuongezea upendo kuliko chuki kwa wapenzi wa mpira ambao ni wengi hapa nchini.
Ila nimepata wazo fikirishi baada ya kusikia kauli yako kuwa Yanga wasibishane na katoto, nikasubiri nione hatma ya kauli yako. Na sasa tumesikia tayari wamefuata ushauri wako na suluhu imepatikana, katoto kako njiani kutua azam.
Umejenga precedence gani mama yetu mpendwa? Ni kweli Yanga walikuwa wanashindana na katoto au katoto kalikuwa kanashindana na Yanga? Yanga kama taasisi na TFF kama wasimamizi wa mpira nchini hawakuwa makini kusimamia kanuni ili kuulinda mpira wetu?
Najiuliza mama vitokee vitoto vinne katikati ya msimu viamue miye sitaki kuchezea timu hii, tunavunja mkataba bila just cause wakati timu imewekeza kwa hawa wachezaji na waruhusiwe tu kuondoka haitoleta vurugu, hasira na chuki kwenye mpira wetu? Au what is so special kwa haka katoto ka kizanzibari?
Mama wewe ni amiri jeshi mkuu vyombo vya dola vyote viko chini yako, je mama yangu mpendwa ulitaka kujua sababu ya haka katoto kuamua kufanya aliyoyafanya ili kuulinda mpira wetu?
Kabla ya sakata hili kufikia hapa wapambe wa tajiri mmoja wa timu walisikika wakisema watakachukua hako katoto, msemaji wa Yanga akasema kwenye mitandao kuwa mchezaji wa Yanga hawezi kuchukuliwa kwa pesa za ukwaju. Haikupita muda mrefu baada ya hata wachambuzi waliokuwa wanashabikia suala hili kutangaza Katoto tu azam is a done deal.
Kulikuwa hakuna wasiwasi kwa upande wa Yanga kwa sababu inajulikana kanuni haziruhusu, lakini kwa mshangao wa wengi katoto kakatangaza kuvunja mkataba mtandaoni na kuingiza kwenye akaunti ya Yanga sh 112. Strange katoto kalikokuwa kanakula ugali na sukari kamepata hela ghafla?
Sheria za FIFA haziruhusu third party kuingilia masuala ya usajili bila kuzungumza na timu yenye mkataba na mchezaji, na kwa kujua hatari hii ya kuadhibiwa wakakaa mbali.
Hawa siyo waliokuwa wanamshawishi afanye maamuzi kinyume na kanuni za uendeshaji wa mpira? Tumekasikia katoto katika maongezi yaliyovuja akifundishwa uongo wa kuongea, pia akikataa hakuna timu inayomtaka, lakini siku tu baada ya kauli yako mama wamejitokeza kumalizana wamchukue. Coincidentally mwenye hii timu asili yake ni Zanzibar.
Mafanikio ya Yanga hadi kufika fainali ya shirikisho afrika na ubingwa wa ligi back to back huwezi kuyatenganisha na GSM na engineer Hersi, lakini katoto kwa kufundishwa kanamshambulia na kumharibia heshima yake, mama hukuliona hilo kwa katoto haka?
Mwisho najiuliza mama yangu mpendwa, kama kangekuwa katoto ka kiluguru kama Dickson Job au Kibwana Shomari ungeitumia hadhara tukufu kama ile kuwaambia Yanga wanashindana na katoto?
Au ingekuwa tajiri kutoka iramba mmiliki wa Singida Big stars angefanya umafia huu vyombo vya dola na ikulu ingemfumbia macho mama yangu?
Tuache hayo mama yangu maana naijua dhamira nzuri uliyonayo katika kuwapatia mema wanao na mimi nikiwemo, hii inawezekana kuwa uchungu wa mama kwa mtoto ila tunaweka angalizo tukifikiria mashabiki na wapenzi wa Yanga watalichukuliaje hili? Mama yangu umefikiria siku Yanga wakutane na Azam? Tena itokee Yanga ifungwe na katoto?
Mama yangu nakupenda na sijawahi kuwapenda marais wanaotokana na CCM, maana wengi CCM kwanza Tanzania baadae wewe ni tofauti kwani:
Tunafanya siasa kwa amani
Umehudhuria mkutano wa wamama wa CHADEMA na unakubaliana.
Wasiojulikana leo aidha wamejulikana wakajificha au umewakimbiza maana hatutekwi tena.
Viongozi wa calibre ya akina Makonda na Sabaya hakuna madarakani.
Na sasa tunaenda kwenye mchakato wa katiba mpya ni matunda ya busara zako.
Hayo ni mapenzi ya mama kwa mtoto yasitutoe kwenye reli.
Mwisho natamani niweke namba yangu nikitegemea naweza kulambishwa asali, maana wote waliokubali kukaa na mama kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu Mheshimiwa Rais wanaitwa walamba asali. Ila naogopa kabla ya kufikia kwenye asali naweza kutana na miiba ya nyuki nikatoka manundu.
Kazi njema ubarikiwe kwa makubwa unayotufanyia watanzania