Nigrastratatract nerve
JF-Expert Member
- Sep 4, 2019
- 1,521
- 4,381
Kuna mambo Mwendazake alituachia inabidi tuyaenzi kwa manufaa ya Taifa letu.
Kwa bahati mbaya Sana Siasa za ndani na nje ya CCM zinataka kutupofusha tusione mambo ya Msingi ambayo yanabeba maslahi makubwa Sana ya Taifa letu Tanzania.
Mwaka 2018 Gazeti la Kenya la The East African liliripoti Sana uzinduzi wa Ukuta wa Mererani. Na katika kuripoti kwao walisema kua India wanauza tanzanite worth 300 mil dollars per year followed by kenya 100 million dollars and Tanzania only 38 million dollars per year.
Kwa hiyo kama tukiweza kudhibiti kabisa utoroshaji wa madini yetu pale Mererani, Tanzania inaweza kuuza Tanzanite yenye thamani ya 438 million dollars.
Fedha hizi ni sawa na shilingi trillion moja za kitanzania. Chanzo hiki peke yake kinatosha kulipia bwawa la mwalimu Nyerere ndani ya miaka 6au 7 bila nchi kukopa nje ya nchi.
Ndani ya Miaka mingine mitano Chanzo hiki kingeweza kutujengea SGR nk. Hapa ndipo Mwendazake alipokuwa akisema nchi hii ni Tajiri lakini ilikuwa ngumu kueleweka na hata SASA inaweza kuwa ngumu kueleweka.
Taarifa ya The East African ikiripoti uzinduzi wa Ukuta wa Mererani hii hapa. MAGUFULI: Tanzanite firms ‘are not paying us enough tax’
Utafiti uliofanywa na Robert Grafen-Greaney, unaonyesha kuwa Kitalu C pekee pale Mererani kina akiba ya tani 1,759 ambazo zinaweza kuendelea kuchimbwa kwa miaka 27 Mbele. Usione watu Wanatununia bila sababu. Tukilegea tumekwisha. Hiki ni Kitalu C peke yake. Hapa tumeongelea Tanzanite tu achana na dhahabu, Almasi na madini mengine mengi ambayo nchi hii imebarikiwa.
Tusitoke kwenye kauli tuliyokuwa tunaimba kuwa Tunaweza kuwa donor county. Ni Kweli inawezekana kama tukiamua. Tusitoke kwenye kusema tunaweza kujitegemea ni Kweli tunaweza kama viongozi wetu wakifikiri vizuri Rasilimali tulizo Nazo zinatosha. Tuzilinde tuachane na Siasa majitaka.
Tupanue Mjadala.
Jarida la Xinhua 2019 liliripoti kuwa viwanda 15 vya Maziwa viliweza kufunguliwa nchini TANZANIA baada ya Serikali kuzuia uingizaji wa Bidhaa za Maziwa hovyo hovyo.
Kwenye habari hiyo inamtaja Sophia Mlote Msajili wa TDB (Tanzania Dairies Board) ambaye anasema viwanda hivi vipya 15 vina uwezo wa kuzalisha Lita za Maziwa 94, 400 kwa siku.
Yaani viwanda 15 vinazalisha Lita chini ya laki Moja kwa siku huku Bidhaa nyingi za Maziwa kama Milk powder Tanzania ikiwa haiwezi kuzalisha.
Fuata link kusoma habari hiyo 15 new dairy industries established in Tanzania: official - Xinhua | English.news.cn
Wakati viwanda 15 vikishindwa kufikisha Lita laki Moja kwa Tanzania wenzetu Kenya kiwanda kimoja Cha Brookside kwa mwaka Wana uwezo wa kuzalisha lita 1.5 million. Yaani kiwanda kimoja kinazalisha mara Tano zaidi ya viwanda 15 vya Tanzania.
Brookside ni Moja ya kiwanda kikubwa Cha Maziwa pale Kenya vipo vya Aina hiyo zaidi ya 15 ambavyo Maziwa yanayotokana na Ng'ombe wao hayatoshi hivyo hulazimika kuvuka Mipaka kutafuta Raw material ya Maziwa. Tuliwahi kuwazuia pale Arusha 2005 Brookside wasinunue Maziwa yetu lakini baada ya wao kuondoka Bei ya Maziwa ilishuka Sana watu wakaenda kwa Mh Pinda kuomba Wakenya waruhusiwe kununua Maziwa. Tanzania milk prices collapse after Brookside exit unaweza kupitia link hiyo kusoma sekeseke Hilo.
Brookside pekee inaweza kulisha Maziwa nchi nzima na kwa kuwa tunayapata toka kwao na kwa Bei rahisi basi kiwanda hiki pekee kinaweza kuua viwanda vyetu vyote vya Maziwa nchini.
Kwa wale ambao hawajui ni kwamba Tanzania ni nchi ya nne Africa kuwa na mifugo mingi nyuma ya Somali, Sudani na Ethiopia. Zaidi ya asilimia 50 ya wakazi wake wanajishughulisha na Ufugaji... Hivyo kama tutaweza kuwekeza hapa vizuri tutafungua kaya nyingi Sana Maskini na tunaweza kuzalisha ajira za kutosha za vijana wetu ambao hawana Ajira.
Dr Mayasa Simba Meneja wa TDB aliwahi kusema kuwa uwezo wa Tanzania kuzalisha Maziwa ni asilimia 40 tu. Asilimia nyingine 60 tunaagiza nje ya nchi. Tunashika nafasi ya nne kwa Mifugo mingi Ila tunaliashwa Maziwa na nchi ambazo hata kwenye kumi Bora ya kuwa na mifugo mingi hawapo.
Kinachofanyika kwa sasa ni Kuwa Tanzania inabakia kuwa hub ya Raw materials tu ambayo kimsingi haina faida yoyote kama hatutaongeza thamani ya mazao yetu. Hata haya mahindi tukiyasaga tu na kuyauza kama unga tutazalisha ajira za kutosha na tutapiga hela ya maana Sana. Kama kweli wanatupenda waturuhusi tuuze Unga wetu kwao badala ya mahindi. Kwanini tunashindwa bado sielewi.
Tuna kila kitu, Nishati, ardhi yenye rutuba, Mifugo ya kutosha, Tumezungukwa na maji kila Kona, hatuna Vita, hatujawahi kulumbwa na ukame lakini tunaogopa kusema nchi hii ni Tajiri.
Tunapotaka kufuta nyayo za Mwendazake tuwe makini nyayo nyingine zimebeba maslahi mapana ya nchi. Zimebeba Usalama wa Taifa Hili. Kuna Pande Mbili za maisha ya JPM Kuna upande umebeba maslahi mapana Sana ya Taifa Hili na upande mwingine Human Error kama walivyo binadamu wengine.
Tumuombe Mama Samia akaze haswa kwenye Rasilimali hizi za Taifa. Wanaotuhitaji watatufuata tu.
Kwa bahati mbaya Sina Lugha nzuri ya kidiplomasia Ila naweza kueleweka.
Nchi hii ni Tajiri