Rais Samia na Hayati Magufuli si kitu kimoja; Tutampima kama atafikia viwango vya Dkt. Magufuli

Rais Samia na Hayati Magufuli si kitu kimoja; Tutampima kama atafikia viwango vya Dkt. Magufuli

Kusema wewe ni tajiri wakati ni maskini ni sawa na teja au mvuta bangi.
Kweli Yoda. Mwendazake alikuwa anasema nchi ya Tanzania ni tajiri Sana, halafu siku ya 2 unamuona Dotto James na Philip Mpango wakisaini mkopo wa matrillioni kutoka Benki za nje.

Au unaona watu wa USAID wakizindua choo cha shule ya msingi walicho Jenga kwa msaada
 
Kama ni kitu kimoja kwanini asingeitwa Magufuli 😂
kila Raisi ni zama zake na kuendeleza mazuri na kuacha mabaya. Yeye angeshilia misimamo ya Corona ambayo imewaondoa hao huku juu itatusadia nini? Huwezi kuiga ubaya. Au yeye kuweka beef na Lissu wakati haimuhusu inasaidia nini taifa? Wale waliokuwa wananufaika na migongano ndiyo wana wasiwasi 😂 sasa ni matokeo tu sio chama, kabila, jinsia wala nini ni matokeo ya viongozi ndiyo muhimu
 
Kosa kubwa tunafanya nchi hii ni kujenga watu badala ya taasisi. Kama tungekuwa na taasisi imara zinazojitegemea leo tusingewaza sijui nani yupo au nani angekuwepo, tungekuwa na uhakika kuwa taasisi zetu zinasimamia maslahi ya nchi kwa uhakika.

Hizi habari tunampima sijui asije akafanya a,b,c ni uduni wa kuogopa kujenga taasisi imara.

Selikari ijenge taasisi na sio kutegema mtu mmoja. Kifo cha Magufuli iwe funzo kuwa nchi haipaswi kutegemea misimamo au maamuzi ya mtu mmoja. Lazima tuwe na dira na uhakika kuwa zipo taasisi zenye uwezo wa kusimamia na kutekeleza sera na mipango ya nchi kwa miaka 100 ijayo.
 
Mwaka 2018 Gazeti la Kenya la The East African liliripoti Sana uzinduzi wa Ukuta wa Mererani. Na katika kuripoti kwao walisema kua India wanauza tanzanite worth 300 mil dollars per year followed by kenya 100 million dollars and Tanzania only 38 million dollars per year.

Kwa hiyo kama tukiweza kudhibiti kabisa utoroshaji wa madini yetu pale Mererani, Tanzania inaweza kuuza Tanzanite yenye thamani ya 438 million dollars
Haya madini yanafaida gani kama uhuru wetu ulipokonywa na watu wachache,Sukuma-Gang?Thamani ya madini inakuwa na maana kama uhuru watu unakuwepo.Ninyi mnakazana na maendeleo ya vitu badala ya watu.Maendeleo yenyewe ya vitu mli hodhi ninyi na baba yenu MwenyeKwenda Zake.Utu kwanza mengine yatafuata!
 
Bro, sikujua maziwa ni bidhaa adimu Tanzania hadi mwaka jana.

Tulisafiri na gari across the country. Tukaondoka Dar 11 asubuhi bila breakfast, tukasema tutakunywa njiani.

Kikombe cha kwanza cha chai ya maziwa tumeenda kukipata Shinyanga. Ukiuliza chai ya maziwa njiani wanakwambia please, hakuna mwenye maziwa hapa.... Dar es Salaam kwenyewe viduka vyenye Tanga Fresh vichacheeeee.... itakuwa Manyoni jangwani huko au Igunga maporini ? Nilikoma kuringa.
 
Kwangu mimi naanza kumtazama atachukua hatua gani kwa mavuno ya pesa ya aibu TFF waliyopora mashabiki wa mpira mechi ya Yanga vs Simba hapo jana.
Je, serikali itapokea kodi inayotokana na mavuno ya aibu?
 
Tanzania sasa imeshapata marais 6 - Mwalimu Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, John Magufuli na sasa Samia Suluhu Hassan. Mwinyi hatukusema tumpime kwa viwango vya Mwalimu, Mkapa hatukusema tumpime kwa viwango vya Mwinyi, Kikwete hatukusema tumpime kwa viwango vya Mkapa, Magufuli hatukusema tumpime kwa viwango vya Kikwete, je ni kwa nini unadhani Samia Suluhu Hassan ndiye inabidi tumpime kwa viwango vya mtangulizi wake?
Tatizo kuna baadhi ya watu wanadhani kwa vile Magufuli amefariki basi mama Samia ndiyo amekuwa Magufuli "mpya" kitu ambacho hakipo kama ambavyo hakikuwepo kwa Mwinyi na Nyerere, kwa Mkapa na Mwinyi na hata kwa Kikwete na Mkapa. Kila zama na kitabu chake. Hata kama yawezekana misingi ikawa ileile lakini kutokana na tofauti ya 'personalities' utendaji wa A kufikia lengo hilohilo unaweza kuwa tofauti na ule wa B na wa C na hata na wa D.
 
Hawa ndio wale waliotutangazia kuwa Wanakula raha kuliko wote Duniani

Hawakuona watu wakitekwa na kuuawa na watu wasiojukikana! Hawakuona mabilionea wetu walivyokufa ghafla ( Mzee Mengi, Ali Mufuruki,Subash Patel n.k).

Mimi nashauri wamwache Rais wetu Mhe.Samia Suluhu Hassan achape kazi wao waende Chato wakaendelee kula raha zao! Makonda ,Musiba n.k msituchoshe kwani ufalme wenu haramu Mwenyezi Mungu aliuhitimisha tarehe 17/03/2021!
 
Lini ulinyimwa huo uhuru wa kutoa mawazo?
Kwa kuwa ulikuwa usingizini au ulikuwa kwenye himaya ambayo kila kitu kwako kili kuwa burudani hukuweza kuona.Ulisha hata kusikia vilivyofungwa na yakatolewa maelekezo ya kuvifungua.Ama ni miongoni mwa mliokwamia awamu iliyopita.
 
Jomba jina lako Nani vile embu litamke...nimependa andiko lako sasa Ni PM ili tufanye mkakati endelevu..I wish JF ingekuwa na waandishi wengi kama wewe...ingesaidia sana nchi na Serikali na hasa Rais wetu katika kuongoza na kusimamia nchi kwa ujumla..tunahitaji think-tank nyingi kama hizi zizaliwe.

Watanzania baada ya Dr Magufuli mindset zao zaidi ya asilimia 80 sio zile za zamani..sio zile za lugha ya umaskini, noooooo way..sasa Ni za lugha ya utajiri ya kwamba Tanzania Ni Tajiri sana...na Ni kweli .

sasa basi kiongozi atakayeanza kuturudisha nyuma kwamba Tanzania ni maskini huyo HATUFAI. na HATUFAI wala hatutataka kumwona..suala Ni hata kama Bado tunahitaji support tufanye kwa kujua kwamba tuna resources zote za kutukinga..Ni LAZIMA TUTOKE UCHUMI WA KATI WA CHINI KWENDA WA JUU ZAIDI NA SIO KURUDI NYUMA TENA.

HII lugha hatutaki kuisikia tena kwetu sisi na vizazi vijavyo..AMINA
 
Nchi hii ni tajiri. Naunga mkono. Mimi nilikuwa activist wa kupinga ujangiri. Kabla ya JPM ujangiri nchi hii ulishamiri sana. Nakumbuka mpaka Bwana Mkubwa mmoja alienda Uingereza akahojiwa kuhusu Mauaji ya Tembo Tanzania, akaanza kujing'ata ng'ata.

Vijana wengi humu ndani hawalioni hata hilo. Tujifunze kuchukua mema na tusirudi nyuma kamwe kuwa nchi shagala bagala kama miaka ya nyuma.

Mawazo yangu, Mama anatakiwa azidi viwango vya JPM kwa kufanya kazi iliyotukuka kwa ajili ya nchi hii. Kwa bahati mbaya sioni kama atafikia hata 20% ya bossi wake wa zamani (mtazamo wangu) japo namtakia mema afanye zaidi. Akifanikiwa tumefanikiwa kama Nchi.

Ili nchi isonge mbele, tunahitaji kuji sacrifice kweli kweli na tuwe na Dira madhubuti ya taifa letu na watu wapambane kuhakikisha tunatimiza hilo. Kwa wale tulioishi ughaibuni kidogo - wengi (si wote) tumeona ukisema Unatoka Tanzania, Unaulizwa about Mount Kilimanjaro na Serengeti National Parks etc. Lini tutaulizwa why your country is so developed?

Nimependa uwasilishaji wa maada yako. Inaonesha wewe ni Msomi na Mwana hoja mzuri. Hongera sana.
 
Back
Top Bottom