Walikuwa wakitizama tamasha na kumuona Mwana FA akizomewa ukumbini.
- Tunachokijua
- Julai 10, 2026 lilifanyika tamasha lilitambulika kama miaka 30 ya Bongo Flava katika ukumbi wa mlimani City, Dar es salaam na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali pamoja na viongozi akiwemo Naibu Waziri wa Sanaa, habari, utamaduni na michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA).
Wakati tamasha hilo likiendelea Naibu Waziri alipanda jukwaani na kuanza kuongea hali iliyopelekea kuzomewa alipokuwa akitoa baadhi ya hoja, ikiwemo alipoeleza kuwa serikali ya awamu ya sita itajenga ukumbi wa michezo (Arena).
Madai
Baaa ya tukio hilo, ikasambaa picha inayomuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri mkuu Mwigulu Nchemba wakitizama tamasha hilo kupitia televisheni Ikulu. AMbapo TV hiyo ilikuwa ikumunesha Mwana FA na kuhusishwa kuwa viongozi hao walikuwa wakifuatilia tamasha hilo pia.
Uhalisa wa madai hayo
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kwa kutumia zana za kididgitali umebaini kuwa picha hiyo ni Potoshi na imehahririrwa kutoka katika picha halisi ya tukio tofauti.
Picha halisi ilipigwa Desemba 13, 2023 Ikulu na kusambazwa na kurasa Rasmi ikiwemo ukurasa wa Msemaji mkuu wa serikali na kurasa za Ikulu Mawasiliano kwa kuambatanisha ujumbe;
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Changamoto za Millenia (MCC) Bi. Alice Albright kwa njia ya video, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 13 Desemba, 2023.
MCC imeichagua tena Tanzania kuingia katika mpango wa kupata msaada wa Fedha zitakazolenga kusaidia mabadiliko ya Sera na Kitaasisi nchini ili iweze kufanikiwa kupata mpango wa Compact.
Mara ya mwisho MCC iliwahi kutoa msaada wa Fedha wa Dola za Kimarekani milioni 698 mwaka 2008 ambazo zilitumika hadi 2013.
Hitimisho
Picha iliyosambazwa Julai 2026 imeharirirwa kutoka katika picha ya Desemba 13, 2023 wakati huo Mwigulu Nchemba akiwa Waziri wa Fedha, akiwa pamoja na Rais Samia walifanya mazungumzo na Alice Albright, Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Changamoto za Millenia (MCC) kwa njia ya video kutokea ikulu ya Chamwino Dodoma.