DOKEZO Rais Samia na Serikali fuatilieni udhalilishaji wa Kingono unaofanyika kambi ya JKT Makutupora

DOKEZO Rais Samia na Serikali fuatilieni udhalilishaji wa Kingono unaofanyika kambi ya JKT Makutupora

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

STINGER

Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
41
Reaction score
11
Wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya JKT ulituambia kuwa jeshi hilo ni muhimu katika kukuza vijana kuwa wazalendo na kuipenda nchi yao.

Kauli hiyo inatofautiana na kile kinachoendelea kambi ya JKT Makutupora maana kuna afande mmoja amefikia pabaya kwa tabia yake ya kudhalilisha watoto wa kike walio kwenye kambi hiyo.

Afande huyo amewadhalilisha vijana wengi wa kike kingono kiasi cha wengine kukimbia kambi hiyo.

Amekuwa akiwatisha na kuwafanyia vituko ambavyo vimewafanya vijana hao kukata tamaa na wengine kujiliuliza iwapo uzalendo uliozungumzia ni pamoja na kukubali kudhalilishwa kiasi hicho.

Afande huyo amewadhalilisha wasichana wengi wao ni watoto wa kimaskini ambao hawana watetezi maana hautuamini kama watoto wa vigogo wanafanyiwa visa kama hivyo.

Kikubwa zaidi ni hivi majuzi alipoanza kuonyesha tabia hiyo kwa vijana wa kiume na alipoulizwa na mmoja wao kuhusu tabia hiyo chafu alijibu kiurahisi tu kwamba kama wewe kwenu ni dhambi kwetu ni suna, hayo ni majibu ya afande anayetegemewa kuwafundisha watoto maadili mazuri na uzalendo kwa nchi yao

Sasa kama anafikia kuwatamani watoto wa kiume tena kipindi ambapo nchi inapambana na janga hili tunajiuliza maana ya JKT ni nini.

Cha ajabu malalamiko yalishapelekwa kwa RC wa Dodoma kwa maandishi na vijana husika waliambiwa barua itamfikia RC, kama imemfikia kaipuuza hatujui kama haijamfikia hatujui. Fuatilia waliokimbia Makutupora utapata taarifa za kusikitisha

Rais wewe ndiye Mama wa vijana wote walioko JKT ndiyo Amiri Jeshi Mkuu fuatilia hili, tayari zaidi ya vijana 10 wamekimbia jeshi kambi ya Makutupora Dodoma tena makao ya nchi.

Haya ni machache mengi utayasikia baada ya baadhi ya vijana waliotoroka Makutupora kutoa taarifa yao kama walivyopanga kukutana na waandishi wa habari wiki ijayo.
 
Halafu tukisema hili jeshi ni jeshi la kisiasa linalotumiwa na maccm mnakataa !Kwa nini huyu hachukuliwi hatua ,nasema hivi JWTZ limekuwa jeshi la chama CCM ,nimewadharau sana hasa kwenye suala la DPWORLD ni wahuniiiii wanaoshirikiana na CCM kuwanyanyasa watanzania
 
Jeshi! jeshi! Jeshi!. Jeshi ni sehemu pekee ambapo hakuna haki za binadamu. Kinachoangaliwa ni cheo. Nikiwa na cheo kikubwa naweza tumikisha waliochini yangu kama nipendavyo. Huyu afande anatumia kigezo hicho.
 
Mbona hujasema kawadhalilisha vipi? Anawatongoza? Anawagonga kinguvu? Anawashika makalio au nyeti? Eleza vizur mtu mwenye akili timamu ataona ni majungu tu umeleta humu btw ana cheo Gani huyo afande?
 
Jiukizeni ni nani aliyewatuma huko? Je ni nini faida zake? Ukimaliza unarlekea wapi?
Maza mwenyewe hajawahi kupotia huko leo mnamlalamikia nani?
 
Mkuu wa kambi na mashushushu wake watakuwa wamefeli sana. Makosa ya namna hiyo kama ushaidi ukiwepo wa kutosha mtu anapelekwa mahakama ya kijeshi na kufukuzwa kazi.
 
Dunia ya sasa jkt ni ujinga .mnaenda kufanya nini? Si bora uende gereji au kujifunza kitu cha kukuwezesha kujiajili katika huo muda wa kusubiri majibu yenu
Well said
 
Eti jeshi. Jeshi la konyo! Mdogo wangu hatakaa aingie kwenye huo upuuzi.

Jeshi la Kungonoka Tu (JKT)
 
Bongo hakuna ajira, unampeleka mtoto jkt kutafuta nin!? Hakuna uzalendo unafundishwa kule,niambie wajukuu wa me into, kikwete, kama, wapo huko jkt!!
Mpe mtoto elimu, Bora, anzisha shughuri ya kiuchumi, hiyo ndio utamuachia mwanao!
Elimu Bora, aweze kuajirika Afrika nzima,
Huko duniani wanaangalia skills nyingine sio hiyo jkt ya kulima malando, migomba, na kufyeka, nyasi,
Wa Toto wanatakiwa wa we na ujuzi wa sayansi, na AI,na lugha,sio kuwapereka jeshini, kukutana na mizee yenye ngoma, itaishia kuwashika makalio tu, na vijana hawa wasiku hz, waliolelewa kwa unga wa lishe, pampasi, serelaki, na maziwa ya kopo,ni walaini kama maini!! Mtoto wa kiume amejazia hatari, sasa huyo wa kike!
Kwa, ufupi kwa, mzazi kama unapereka mtoto wako jkt, kuwa makini,sana, huko sio njia pekee ya kupata ajira, serikali haina ajira, fulsa,ni chache, muda wa, kwenda jkt, ni Bora kijana akaenda veta kujifunza skills, tofauti, za, ufundi,Sanaa, kilimo nk.
Lengo LA jkt ni zuri,tatizo kuna upuuzi, mwingi sana, hata Hao viongozi wao, ukiwasikia wanahutubia kwenye kuhitimisha mafunzo, kuna maneno wameyakalili kama kasuku, utawasikia, "nendeni mjitengenezee fulsa, mjiajiri" Wakati hayo mazee yapo jeshini kwa miaka 30+hayajaweza, hata kujenga genge na kutoa ajira kwa MTU mmoja,
Richa ya kukaa kwenye utumishi kwa miaka 30+, ukiyafukuza Leo, hayawezi, kusimama yenye we, tutazika kesho, tu!! Harafu unamuambia kijana wa kidato cha nne na Sita, akajiajiri.
 
IO Dept ya chuoni hapo imefeli sana hadi taarifa kupelekwa nje kwa barua hii itamla mkuu wa chuo
 
Dunia ya sasa jkt ni ujinga .mnaenda kufanya nini? Si bora uende gereji au kujifunza kitu cha kukuwezesha kujiajili katika huo muda wa kusubiri majibu yenu
Eti wanaenda kufundishwa uzalendo

Ova
 
Hii habari sio nzuri hasa kwa chombo kikubwa kama jeshi. Binafsi kama kuna chombo ninachokikubali basi ni jeshi habari hii iwe ni ya kweli au sio ila imetia doa JKT.

My take.
Lengo la JKT ni kuwajengea vijana uzalendo, kuwafundisha kazi, kuwajengea ujasiri na kuwapa mafunzo ya ulinzi na usalama na kubwa zaidi ni kuwafundisha nidhamu.
Mimi niongelee hili moja tu la nidhamu, Kwa bahati mbaya sana majeshi yetu yamekuwa yakijisifu kwa kufundisha nidhamu ambapo kiukweli nidhamu inayofundishwa hapo ni nidhamu ya utii tu.
Naposema nidhamu ya utii namaanisha nidhamu ni dhana pana ila utii ni katika nidhamu sasa jeshi lenyewe linafundisha nidhamu ya utii tu hili ndio kosa ambalo JKT na majeshi mengine yanafanya.
Kwani nidhamu ya utii ime base kutoka kwa mdogo kwenda kwa mkubwa kwa maana mdogo ata mtii mkubwa bila kuhoji ndio maana itawaona watu wengi wakiwasifu wanajeshi kwa nidhamu ila hawajui kuwa ni nidhamu ya utii ndio wanayo, kitu hichi kimepelekea baadhi ya wakubwa kukitumia kama kichochoro cha kuwaonea wadogo, kuwa harass na ku wa abuse hasa ishu ya ngono ni tatizo sana.
Niseme kuwa sio JKT tu bali majeshi yote yanatakiwa kuwa reformed kuanzia kiuongozi, uwajibikaji, nidhamu, muundo mpaka utendaji.
Kufumbia macho mambo haya ndiyo kinapeleka idadi ya wanajeshi wenye UKIMWI kuongezeka jambo ambalo ni hasara kwa jeshi kwani mtaji wa mwanajeshi ni afya yake, Lakini pia wanawake wengi wanakuwa wanatumika kama bidhaa tu mpaka baadhi ya wazazi wamekuwa waoga kuwaruhusu vijana wao wakike kujiunga na majeshi naposema hivi najua kama kuna mwanajeshi humu atakuwa anaelewa, Wapo wanajeshi wanaojielewa hawaruhusu watoto wao wakike kuingia jeshini kwasababu wanajua what is going on kwenye makambi.
Ni hitimishe kwa kusema majeshi yanatakiwa kuwa reformed, Sheria kali ziwekwe na zitekelezwe kwa wanao vunja maadili. Kwa sasa nimeongea upande wa nidhamu tu ila kuna mengi kuhusu mabadiliko katika majeshi yetu
 
Dunia ya sasa jkt ni ujinga .mnaenda kufanya nini? Si bora uende gereji au kujifunza kitu cha kukuwezesha kujiajili katika huo muda wa kusubiri majibu yenu
Muundo wa jkt ni mzuri sana ila viongozi wa sasa wamefail kulifanya kuwa jeshi la kuwakwamua vijana kwa maarifa mpya.

Mbinu na namna ya ufundishaji ni uleule wa kipindi cha chama kimoja wakati hata namna tu ya maisha ya Tanzania yameshabadilika.
 
Back
Top Bottom