Rais Samia, na sisi wana michezo tuna ombi letu. Na tunaomba ulifanyie kazi, ikikupendeza

Rais Samia, na sisi wana michezo tuna ombi letu. Na tunaomba ulifanyie kazi, ikikupendeza

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2019
Posts
33,092
Reaction score
96,127
Lengo kuu la hili bandiko langu humu jukwaani, ni kukuomba tu kwa heshima na taadhima! Mheshimiwa Rais kuangalia namna ya kuvirejesha kwenye Halmashauri zetu baadhi ya viwanja vya michezo nchini mfano Sokoine Mbeya, Samora Iringa, Nelson Mandela Rukwa, Ali Hassan Mwinyi Tabora, Jamhuri Morogoro na Dodoma, Mkwakwani Tanga, na vinginevyo vingi kutoka kwenye umiliki wa chama chako cha CCM, ili viboreshwe kama ule uwanja wa Kaitaba Kagera! na hivyo kuendelea kutumika kwenye ligi yetu, lakini pia kwenye uibuaji wa vipaji vya wana michezo nchini, (na ukichukulia michezo ni moja ya vyanzo vizuri sana vya ajira kwa vijana), hivyo jambo hili halikwepeki.

Natambua fika siyo jambo jepesi kihivyo, ukichukulia kwamba hivi viwanja pia ni moja ya vyanzo vya mapato ya chama chako, na makada wachache. Lakini ifikie wakati tutangulize kwanza maslahi ya Taifa, na yale ya mtu binafsi/chama yafuate baadaye. Maana hivi viwanja vilijengwa enzi za mfumo wa chama kimoja kupitia kodi za Watanzania wote. Hivyo sioni sababu ya CCM kuvimiliki! Na huku ikishindwa kabisa kuviendeleza kwa miaka 30 sasa! Yaani karibia viwanja vyote viko mahututi kwa kukosa matunzo! Na badala yake imevigeuza tu kuwa chanzo chake kimojawapo cha mapato.

Ni matarajio yangu kuwa hili ombi litafanyiwa kazi kwa wakati.
Kwa niaba ya wapenda michezo wote nchini. Naomba kuwasilisha. ✍️
 
Mimi nilifikiri ungeomba kufanyika ujenzi wa viwanja viwili vipya vya kisasa vyenye hadhi ya kimataifa kwny moja wapo ya majiji yetu ili na sisi tuandae Afcon..kwnn mnapenda vitu vidogovdgo!
 
Ni matarajio yangu kuwa hili ombi litafanyiwa kazi kwa wakati.
mkumbushe na ombi hili tulilopeleka siku kadhaa baada ya kurudi kutoka Ulaya

1647231574319.png
 
Back
Top Bottom