Ngaliwe
Senior Member
- Dec 30, 2015
- 164
- 374
Ukweli ni kitu gani? Swali hili limedumu kwa umri sawa na kalenda inayotumika sasa duniani, yaani karne 21 au miaka elfu mbili na ishirini na moja.
Tangu wakati huo ukweli umekuwa mhanga wa karibu kila jambo, hasa inapotokea ukweli huo haupendezi sana masikioni mwetu, watu hujikuta wakiushambulia au kumshambulia yule aliyeusema kana kwamba kwa kufanya hivyo kunaweza kuubadili.
Katika jamii zetu ukweli umekuwa tiba kubwa na muhimu ya matatizo mengi ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na hata kisiasa. Lakini jamii zetu zimejikuta zikiogelea katika tatizo ama matatizo waliyo nayo bila kupatikana suluhu hata kama miongoni mwa wana jamii hao wanaelewa vyema msingi wa matatizo hayo lakini kwa kuwa ukweli huo ama haupendwi au jamii hiyo haitaki kuukubali, basi kila mtu hatausema na kwa kukaa kimya kwao jamii huelekeza nguvu na rasilimali zingine katika kutatua tatizo lisilowakabili na kuliacha tatizo halisi likiendelea kushamiri.
Ndiyo maana wahenga wakatuasa kwa ukweli mchungu kwamba mficha maradhi kifo humuumbua, maana yake ni kwamba tatizo halitatuliki kwa kulificha au kujifanya hamlijui. Ukweli hubaki katika hali hiyo hiyo mpaka utakapotambuliwa na kupokelwa kwa rangi yake halisi.
Ukweli una sifa mbili muhimu ya pili ni kumuweka anayeukubali kuwa huru, lakini sifa ya kwanza kabla haujawekwa huru na ukweli lazima kwanza ulipe gharama zake, wenzetu wanasema the truth will set you free but if it doesn't kill you first.
Kwamba ili ukweli ukuweke huru lazima kwanza ukubali uchungu wake, katika jamii ambayo maslahi binafsi yametawala fikra za wanasiasa na wanaharakati, ni changamoto kubwa sana kueleweka unaposema ukweli mchungu ili hatimaye jamii iondokane na tatizo lililopo.
Ndivyo ilivyotokea kwa kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu umuhimu wa kusadia mistakabali wa maisha ya baada ya maisha ya soka kwa wanasoka wa kike nchini.
Kauli ya Rais imeuweka bayana mtazamo ulilopo katika jamii yetu, pengine ikiwemo miongoni mwa wanaomkosoa sasa. Ni mnafiki wa kiwango cha kimataifa tu ambaye hataelewa au hakutambua nia njema ya Rais Samia kwa wanasoka wa kike ambao wengi tunajua wanakutana na changamoto kiasi gani wakimaliza maisha yao ya soka.
Ni kwa vile tu baadhi ya wenzetu wamekengeuka kiasi kwamba kila kitu wanataka wafanye kiwe siasa, na kwa kuwa wengi wa wanasiasa na wanaharakati wamepoteza uhalali mbele ya jamii, wanafanya kila juhudi kuendelea kusikika kwa kila jambo. Na kwa kuwa wanatafuta, chambilecho vijana wa leo, kiki, wanaona ili waipate lazima waelekeze ukosoaji wao hata ule usiokuwa na mantiki kwa rais, ili tu wanasabishe hoja zao mufilisi na jina la rais.
Rais Samia angekuwa na nia mbaya kwa watoto wa kike wanaosakata kabumbu, hivi angekubali kuwa mdhamini wa michuano wa soka la wanawake katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)?
Uamuzi huu wa Rais Samia ni wa kipekee na wa kupongezwa na kila mtu anayethamini mabinti wanaocheza soka, siyo siri kwamba soka la wanawake ni kama lilikuwa limetekelezwa katika ukanda wetu huu. Hakuna kampuni wala nchi iliyojitokeza kudhamini michuano hiyo ili kuipa uhai na kuthamini mchango wa watoto wa kike wanaojitolea katikati ya changamoto kubwa za kijamii na kitamaduni na mila zinazowanyima watoto wa kike nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.
Rais Samia ameguswa na kuwiwa kama mama kuwasaidia mabinti hawa, siyo tu nchini Tanzania bali katika ukanda wote wa Afrika Mashariki na Kati, badala ya kupongezwa kwa jambo la maana na msingi kwa kuthamini watoto hawa, kauli yake iliyosema ukweli kuhusu jamii yetu imegeuzwa kuwa agenda badala ya majitoleo yake makubwa kwa soka la wanawake.
Kwamba hata wanaharakati wa haki za kijinsia na watoto nao pia wameingia katika mkumbo huo na wengine ndiyo wamekuwa viongozi wa kukosoa ni kielelezo cha kiwango cha juu cha unafiki uliofikiwa na baadhi ya wanajamii wenzetu tunaoishi na kila nao, wametuthibitishia kwamba kwao ukweli ni kile tu kinachowapa uhalali wa kuendeleza harakati zao, ukweli wowote kuhusu jamii na mustakabali wake, unaowakosesha guess ya kuendeleza harakati, siyo muhimu.
Tuepuke kuingia kwenye mtego huu, tumuunge Mkono Rais Samia katika juhudi zake za kuwakomboa wasichana hasa wanasoka.