Rais Samia najua mapato ya mwezi wa 4 umeyaona tayari. Kariakoo wanakuangusha

Rais Samia najua mapato ya mwezi wa 4 umeyaona tayari. Kariakoo wanakuangusha

Countrywide

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Posts
20,694
Reaction score
32,527
Naomba ku-declare interest.

Mimi binafsi nampenda na kumkubali Sana Mama Samia hivyo kwa nguvu na uwezo nilionao sitakubali hujuma yoyote kwake.
Nchi inaendeshwa kwa Kodi, hivyo kauli ya mama Samia kusema tutumie akili kukusanya hakumaanjsha tusilipe Kodi na badala yake mapato kupungua na kuonekana Kama ameshindwa.

Mama ni Mtu wa busara Sana, na hapa ndipo ninamkubali zaidi. Ila wafanyabiashara Sasa hivi wanatumia vibaya hizi busara zake.
Mfano mdogo na rahisi, Sasa hivi kariakoo ukinunua mzigo hupewi risiti, na ikitokea umepewa basi unaambiwa "chukua ya kutembelea na mzigo" hapo Kama mzigo ni wa milioni 2 basi unapewa risiti ya laki 2. Huu ni ukweli.

Mama najua huu mwezi wa 4 umeona mapato yalivyo na uhalisia ni kuwa Kuna watu ni Kama wamedhamiria kukukwamisha. Wafanyabiashara wote na Mimi nikiwemo tujitahidi kulipa Kodi na tutoe risiti mapato yapatikane mama yetu atuletee maendeleo.
 
Muuza mapera na wewe unatolea risiti wapi! Acha unaaa!!

Mlizoea kuumiza sana watu nyie, imawezekana wewe ulikuwa kwenye ile team ya kuumiza watu sasa kula yako ya unyanganyi imekoma inakuuma!

Fanya kazi kwa haki acha dhuluma!!
 
Mkuu kazana kutafuta hela, serikali inanjia nyingi za kuingiza mapato..

Duniani kote hakuna mfanyabiashara anaetaka kulipa kodi halali.
Mama kakwambia kama una vielelezo peleka wakusaidie halafu utakubalije upewe risiti feki inamaana na wewe ni feki 'kichwani empty'
 
Swala la risit ya bei ndogo halijaanza leo lipo kitambo mnoo.. Hasa zilipoanza hiz risit za efd ndio likawa kubwa zaid
 
Sisi yetu macho tu tukikosoa tunaambiwa hatujui tunachokitaka!

Sisi tunataka rais mwenye sifa zote sio dicteta wala goigoi aweze kufanya yote kodi ikusanywe, ufisadi apambane nao, Uhuru wa habari uwepo na katiba mpya ifanyiwe mchakato.

Bahati mbaya huyu rais ajazaliwa hivyo kama hayupo tutapiga kelele mpaka apatikane.
 
kwani mwezi uliopita TRA wamekusanya shingapi?
 
Naomba ku-declare interest.
Mimi binafsi nampenda na kumkubali Sana Mama Samia hivyo kwa nguvu na uwezo nilionao sitakubali hujuma yoyote kwake.
Nchi inaendeshwa kwa Kodi, hivyo kauli ya mama Samia kusema tutumie akili kukusanya hakumaanjsha tusilipe Kodi na badala yake mapato kupungua na kuonekana Kama ameshindwa.
Mama ni Mtu wa busara Sana, na hapa ndipo ninamkubali zaidi. Ila wafanyabiashara Sasa hivi wanatumia vibaya hizi busara zake.
Mfano mdogo na rahisi, Sasa hivi kariakoo ukinunua mzigo hupewi risiti, na ikitokea umepewa basi unaambiwa "chukua ya kutembelea na mzigo" hapo Kama mzigo ni wa milioni 2 basi unapewa risiti ya laki 2. Huu ni ukweli
Mama najua huu mwezi wa 4 umeona mapato yalivyo na uhalisia ni kuwa Kuna watu ni Kama wamedhamiria kukukwamisha.
Wafanyabiashara wote na Mimi nikiwemo tujitahidi kulipa Kodi na tutoe risiti mapato yapatikane mama yetu atuletee maendeleo.
Mama sio mda atakuja na mfumo mzuri,spendi watu kutolipa kodi,ila pia usiweke chumvi Sana k/ Koo ilisha kufa pia, sio kipindi Kuna kiongonzi alioneshwa sikitishwa na Hali ya k/ Koo kwamba hata watu waliokua wanakuja fungasha mizigo hapo TOKA nje hawaji, so mama anajua anafanya nini that's akisema kipindi kifupi makusanyo yatapungua, but ipo njia itakuja ya kufanya ulipaji wa kodi usimamiwe KWA taratibu ila sio zile, za unyanganyi Kama kipindi Cha mwendazake,
 
Kodi ya VAT ni kubwa we umeanza kununua bidhaa kariakoo lini kwa asilimia zaidi ya 70 machinga ndo wanunuzi wa hapo kariakoo wala huwa hawachukui risiti kwahiyo hao machinga ndo wanatumika kukwepa kodi
Machinga wangeendelea kukaa maeneo yao sababu hali iliyopo sasa machinga ananunua mamizigo ya kutosha anauzia hapo hapo nje ya duka mwisho wa siku inakuwa ngumu kuzibiti ukwepaji wa kodi
 
Kariakoo ilikufa kwa uamuzi wa kuhamia Dodoma. Spenders wengi ambao ni watumishi wa serikali wameondoka Dar.

Na siyo Kariakoo tu, bali hata mahoteli mengi ya mwambao wa bahari ya hindi nayo yana hali mbaya, nayo sababu mojawapo ni kuhamia Dodoma!
 
Biashara nyingi kutokana na utandawazi zinawafuata wateja waliko
 
Kawa pokonye kwangu kama baba yako alivyo kuwa ana fanya!
Kariakoo ilisha kufa ilikuwa ina subiri kuzikwa tu
 
Aliyekudanganya nani kwani haya wakati wa jiwe Magufuli hayakuwepo?

Unazungumzia 2mill upewe risit ya 200K,January mwaka huu kuna jamaa nilimfungia mzigo hapo Kkoo wa karibia mil3 jamaa akaandika risit ya 170,000/= tu tena baada ya kuvutana sana akidai siku hizi hakuna noma.
 
Unless unazungumzia maduka makubwaa yenye VAT, ila maduka yetu haya ya Risiti za kawaida utoe risiti usitoe makadirio ni yake yale, unafkiri Tra Hawajui?
 
Mama sio mda atakuja na mfumo mzuri,spendi watu kutolipa kodi,ila pia usiweke chumvi Sana k/ Koo ilisha kufa pia, sio kipindi Kuna kiongonzi alioneshwa sikitishwa na Hali ya k/ Koo kwamba hata watu waliokua wanakuja fungasha mizigo hapo TOKA nje hawaji, so mama anajua anafanya nini that's akisema kipindi kifupi makusanyo yatapungua, but ipo njia itakuja ya kufanya ulipaji wa kodi usimamiwe KWA taratibu ila sio zile, za unyanganyi Kama kipindi Cha mwendazake,
Kuna kipindi kkoo ilikuwa inajaa wafanyabiashara kutoka nchi za jirani,yani ukipita madukani wapo wanafungasha maroba yale na kuandaa oda,hoteli za kariakoo walijaa,lakini wote walipotea.Nafikiri sasa watarudi tena,magari ya transit yatabeba mizigo kama yote maana wameruhusiwa kubeba bidhaa watakazonunua kwetu kwenda nazo kwao.
 
Mama kakwambia kama una vielelezo peleka wakusaidie halafu utakubalije upewe risiti feki inamaana na wewe ni feki 'kichwani empty'
Inawezekana mtu asiwe feki. Umepitia maduka kadhaa kariakoo ukapata bei ya kitu ni shilingi laki 2 au zaidi kidogo. Huyu mwenye duka fulani akakuambia nipe laki na sabini ila nitakuandikia risiti ya 140,000. HII DILI UTAIKATAA? HEBU TUJIPIME NDIVYO INAVYOTOKEA? SASA HIYO RISITI YA 140000 NDIYO YENYE KODI. KIASILI TUJIULIZE HIYO KODI SERIKALI SI IMEPATA? PIA HAIELEWI HUYO MFANYABIASHARA AMEPATA NINI HAPO. MARA NYINGI SI FAIDA KUBWA SANA. ANATAKA MALI IISHE HARAKA AKACHUKUE NYINGINE BADALA YA KUNGANGANIA BEI KUBWA. NDIO kisa cha kuteremsha bei afuatilie mzigo mwingine.YAANI UNAWEZA KUTA FAIDA NI SAWASAWA NA YULE ANAYEUZA BEI KUBWA ila huyu kaitafuta kwa kutumia ujanja zaidi. SASA AKIFUATA MWINGINE AKAUZA HIVO HIVO SI SERIKALI ITAKUWA IMEPATA KODI MAPEMA NA PENGINE KUBWA KULIKO HUYO WA BEI KUBWA NA MZIGO HAUISHI
 
Swala la risit ya bei ndogo halijaanza leo lipo kitambo mnoo.. Hasa zilipoanza hiz risit za efd ndio likawa kubwa zaid
Hilo lipo miaka na miaka, hata TRA wanajua hilo.

Na halitakuja kuisha labda kama TRA ndio waanze kuuza maduka.
 
Swala la compliance ni la buyer na seller. Wote wawili wanatakiwa ku comply , sasa kama mmoja hataki basi chukua hatua . Acha mzigo. TRA hawawezi kuwepo kila mahali . Ni jukumu letu kutimiza wajibu watu badala ya kulalamika kwenye media
 
Back
Top Bottom