Yusufu R H Sabura
JF-Expert Member
- Jun 26, 2020
- 355
- 486
Your Excellency,
Nakusalimu kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Raisi, Ninaamini umzima wa afya na unaendelea kutekeleza majukumu yako kwa kadri Mwenyezimungu alivyokujaalia.
Mheshimiwa Raisi, hii itakuwa ni mara yangu ya pili kuzungumza na wewe kupitia maandiko haya ya majukwaani, bila shaka salamu zangu za awali zilikufikia na kama bado naamini zitafika tu. Nimechukua tena uamuzi wa kukuandikia hili kwa vile, kama Kijana na shabiki wako kisiasa, nimeona ipo haja ya wewe kulitekeleza hili ili twende kwa ulaini zaidi hapo kwenye kampeni za uchaguzi mkuu 2025.
Jina langu ni YUSUFU R H SABURA.
Mheshimiwa Raisi, kwa dhamana uliyopewa na wananchi, kuliongoza taifa hili la Tanzania, inakuwa ni wajibu kwako kwanza kama Raisi, lakini pia kama mzazi au mlezi au hata mama, kuhakikisha kwamba si Tanzania ya leo tu, bali hata ya miaka mia moja baadae inakuwa katika mpangilio mzuri wa kimaisha yaani kijamii, kiuchumi na kisiasa. Mheshimiwa Raisi kuna ufa mkubwa sana hapa kwenye jamii yetu ukijaribu kutizama maisha ya vijana. Naam ni Sheria ya ndoa ya mwaka 1971.
Mheshimiwa Raisi, hivi karibuni kumekuwa na vuguvugu la vijana kukataa ndoa, na vuguvugu hili nimeanza kulionea hapahapa jamii forums!, wakisindikizwa na maneno hasi kama vile NDOA NI UTUMWA, NDOA NI UTAPELI nk. Kwa namna nilivyojaribu kuwaelewa kwa nafasi yangu, moja ya sababu ya vuguvugu hili ni muundo wa sheria yetu ya ndoa ya 1971. kwa vile sio mtaalamu sana wa masuala ya kisheria sifahamu kama kuna ammendments zozote zilizowahi kufanyika, na kama zipo basi nikwambie tu bado haijatosha.
Mheshimiwa Raisi, nakushauri waagize wabunge wa chama cha mapinduzi wakapitie na kuunda upya sheria ya ndoa. Tena katika zoezi hilo wawe watulivu sana zaidi ya utulivu aliokuwa nao mheshimiwa waziri Hussein Bashe alipokuwa akijibu hoja ya sukari ya ziada iliyoibuliwa na mheshimiwa mbunge, Luhaga Mpina.
Mheshimiwa Raisi, ninafahamu kabisa kwamba, wakati sheria hii inatungwa, lengo lilikuwa ni kuondoa kama sio kupunguza unyanyasaji wa kina mama ama kwa lugha ya hapa jinsia ya kike wanapokuwa katika maisha ya ndoa. Lengo lilikuwa jema na tunaona hali ilivyo sasa sio kama zamani, sasa utu wa mwanamke unaonekana na wanaume wamegundua aaah kumbe mwanamke naye ni mtu.
Lakini changamoto ya moto kwelikweli iliyojitokeza hapa ni kwamba, wakemia waliochanganya mseto wa sheria hii sijui walikuwa wamefumba macho !, kiukweli sheria ya ndoa imevuka katika kurekebisha na sasa inaharibu ndoa, mheshimiwa Raisi hii dozi ni kali sana na imekuwa sumu kwani familia zinakufa kwa kasi ya ATCL.
Mheshimiwa Raisi, hivi sasa vijana wanaamua kukataa ndoa na kuanzisha mifumo mipya ya kimaisha ambayo ni ya hovyo ukilinganisha na utamaduni wetu, zimesikika sauti mitaani kwamba kupitia sheria hizi wanawake wamekuwa wajeuri kwelikweli na wamekuwa tishio hata kwa mali za familia, ndio kusema kwamba wakigombana kidogo tu silaha yao kubwa ni kuvunja ndoa ili wagawane mali. tafsiri ya hili ni kuwa, badala ya kufanya kazi wapo watu kila siku wanabuni ndoa ili wakapore vilivyotafutwa huko.
Mheshimiwa Raisi, ili ugundue kuwa kuna shida hapa, kwa vile wewe ni mwanamke nitakuomba uvae kimyakimya uhusika wa watu wawili hawa, wa kwanza ni mdada anaejidai kulindwa na sheria ya ndoa ya 1971, lakini uhusika wa pili ni kuwa mama mzazi wa mwanaume anaefanyiwa unyang'anyi wa kisheria na binti kupitia mwamvuli wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971. Sijakuchagulia uhusika wa kiume kwa vile huwezi kuwa na hisia za moja kwa moja za kianaume, wewe ni mtu mzima, ulianza kuwa binti, ukawa mama na hata bibi wa wajukuu zako, kwahio wahusika hawa wote wawili wapo ndani yako.
Mheshimiwa Raisi, ni furaha sana kwa mabinti kujitwalia mali kwa urahisi kabisa na kwa kweli hata ningekuwa mimi ningefurahi maana ni upendeleo wa kipekee, sina maana ya kudhoofisha juhudi za sera ya jinsia ya hamsini kwa hamsini lakini fikiria wanandoa wanapopelekwa madawatini halafu akasikilizwe mwanamke tu na mwanaume akapewe karipio, akaonekana hana akili na jitihada zake zote kuijenga familia zisionekane na ikibidi anyang'anywe bila kujali muda alioutumia. Fikiria kuwa ungekuwa wewe ni mama mzazi wa mwanaume huyu ungepata furaha kama aliyoipata mwanamke mwenzako (mkweo)? kwa kuzingatia tu kwamba sheria imempendelea sana mwanamke na kumuacha nyuma mwanaume badala ya kuleta usawa! .
Mheshimiwa Raisi, nakuomba rudisha imani ya serikali kwa vijana kwa kubadilisha sheria hii iendane na sera ya hamsini kwa hamsini, ili vijana waache uoga wa kunyanyaswa na wake zao na wakimbilie ndoa haraka sana iwezekanavyo kwa maslahi ya taifa. Kama utafanya hivi nakuhakikishia vijana na wakina mama wengi ambao kimsingi ni wote watakukumbatia kwa furaha ambayo hawajawahi kuisikia tangu sheria hiyo ilipoundwa.
Mheshimiwa Raisi nimeandika hili kwa experience kubwa sana, familia yangu sasa (mimi ni mtoto) ipo katika hali ya kusambaratika kwa muda wa miaka karibia kumi chanzo kikiwa ni sheria ya ndoa ya mwaka 1971, Nilikuwa form three, nikaenda high school, nikaenda chuo, nikamaliza na sasa nipo kitaa.
Mheshimiwa Raisi, nimekusikia mara kadhaa ukiimba wimbo wa Political Stability, sisi wataalamu wa sayansi ya siasa tunaamini kuwa familia ndio the smallest political unit in a state. kama huku chini hakutakuwa na stability ya kiutawala nakuhakikishia huko juu mtasumbuka sana, anza na ngazi ya familia, sisi wawakilishi wako katika ngazi ya familia(wanaume) sheria inatunyanyasa mno.
Mheshimiwa Raisi, jambo la pili ambalo binafsi nafikiri litakuwa fyekeo kali sana kuelekea 2025 ni MSAMAHA WA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU KUANZIA MWAKA 2014-2024.
Najua kuna wakosoaji watasema nafanya jitihada za kufutiwa deni langu lakini nakuhakikishia hili ni sahihi na ikibidi samehe wote nchi nzima la kwangu nitalilipa mwenyewe, ni takribani kama millioni kumi na tatu na ushee hivi.
Mheshimiwa Raisi, nimeamua kuchagua miaka tajwa hapo hapo juu kwa vile wewe ni shahidi kwamba, tangu mwaka 2014 serikali iliacha kutoa ajira kwa kada nyingi, hadi wewe ulipoingia madarakani mwaka 2021, hata hivyo pamoja na jitihada zako za angalau kupunguzapunguza aibu hii bado kidonda kilichopo ni kikubwa sana na lawama hazitakuwa upande wako hata kidogo.
Isipokuwa ningekushauri, ili upunguze fukuto la hasira na kuvunjikwa mioyo ya wengi waliohitimu, wasamehe mikopo yao na ikibidi watakapopata ajira badala ya kuanza kulipa deni hilo kubwa basi waanze maisha kwa wepesi. wamekaa sana mtaani, Mheshimiwa Raisi kete iliyobaki ni kujenga familia zao hivyo wapunguzieni (sisi) mzigo kwani halikuwa kosa lao(letu).
Mheshimiwa Raisi, ninaamini msamaha kwa mikopo ya elimu ya juu kuanzia mwaka 2014-2024 inawezekana kwa vile, hebu tumia logic hii tu ndogo, mmetupatia mikopo kwa miaka kumi na hatujarudisha na bado nchi unaijenga, na kila mwaka bajeti ya HESLB inapanda hii ni ishara na dalili kwamba elimu bure vyuo vikuu inawezekana lakini anza kwanza na hili la msamaha wa mikopo, NAJUA UNAWEZA MHESHIMIWA RAISI.
Mheshimiwa Raisi, Nakuona ukishinda kwa ushindi wa kimbunga, kura ni za kuokota, tufanyie hayo vijana wako ili waseme umeturoga. hakika utakuwa umewakomboa vijana na ukiwakomboa vijana utakuwa umelikomboa taifa.
Sitapenda kumaliza uzi huu bila kukupongeza kwa mambo makubwa unayolifanyia taifa letu, sisi tunaona kuwa ilivyokuwa jana siyo leo, hivyo wewe chapa kazi, wakikunanga sana wewe niite mimi nitazungumza nao taratibu na wataelewa tu.
Asante na kazi iendelee.
YUSUFU R H SABURA
0750883466/0717934194.