Rais Samia: Nakwenda kufungua Nchi, mmekuwa mkinitukana sana mitandaoni

Rais Samia: Nakwenda kufungua Nchi, mmekuwa mkinitukana sana mitandaoni

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Rais Samia Suluhu Hassan amesema anakwenda kufungua Nchi akisema, "Mmekuwa mkinitukana sana kwenye mitandao! Unakwenda kubomoa yaliyojengwa kwa muda mrefu".

Akizungumza na Wafanyabiashara wa Tanzania Nchini Kenya Mei 05, 2021 Rais amesema anaamini hakuna Nchi inayoendelea ikiwa peke yake.

Ameeleza, anajiandaa kufanya mkutano na Sekta Binafsi kuzungumzia kero mbalimbali zikiwemo za Kodi, Vibali vya Kazi (Work Permits), kuchelewa kupata ardhi kwenye Uwekezaji ili kuona namna ya kuziondoa.

Rais amesema maeneo ya kujenga Uchumi yapo lakini mchakato umekuwa ukienda polepole, akitolea mfano eneo la "Industrial Parks" alilosema haoni sababu kwanini zinazuiwa.

Msikilize hapa:


 
Mama wacha achape kazi, hao watoto wa marehemu wanaosumbuliwa na jinamizi LA baba yao asiwasikilize awapuuze ajue sisi wanae tuna matumaini makubwa sana na yeye. Hao lengo lao wanataka kumtoa kwenye reli ili asitufikishe nchi ya ahadi.
 
Mama aachane na mitandao na asithubutu kuishi kwenye kivuli cha Jiwe mpuuzi.

Tumia vipawa vyako, simamia unachokiamini ila hao wa mitandaoni wakivuka mipaka watie adabu Rais ni wewe tuu hakuna wa kukupangia

Hata Jiwe tulitukana Sana
 
Kuboost uchumi kutoka 4.9% lazima afanye hivyo anavyofanya la sivyo hali itakuwa mbaya, watu watashindwa kufanya purchasing ya product zinazozalishwa na hivyo kuathiri viwanda na uchumi kwa ujumla

Sera za mwendazake zilikuwa ngumu sana kutoboa maana zilikuwa za kukusanya tu hii inaitwa Contractionary fiscal policy mama bila shaka atatembea na expansionary
 
Back
Top Bottom