Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua kiwanda cha uzalishaji vioo vya ujenzi cha Saphire Float Glass - Mkuranga Mkoa wa Pwani leo tarehe 20 Septemba, 2023.
Rais Samia amesema Kiwanda hiki kitakuwa kikubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati, na cha 4 kwa Ukubwa barani Afrika kwa uzalishaji wa vioo vya ujenzi. Pia, 75% ya bidhaa zake zitauzwa nje ya nchi hivyo kuongeza mapato kwa nchi na kutoa ajira 1650 kitakapokamilika kuanza kufanya uzalishaji kamili.
Uwekezaji huu nchini ni mapinduzi makubwa ya kuimarisha uchumi wa nchi.
Serikali imefanya maboresho mengi ya kisera, kisheria na kikanuni ili kufanya mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kuwa bora zaidi.
China na Tanzania zinafurahia urafiki wa kidiplomasia ambao unakaribia kufikia miaka 60, uwepo wa wawekezaji hawa ni mfano halisi wa mahusiano mema kati ya nchi hizi mbili. Nayahakikishia makapuni yote yaliyowekeza Tanzania kutoka ndani na nje ya nchi, mali zenu zipo salama, na serikali itaendelea kuwekeza au kuweka mazingira mazuri kwa biashara zenu kufanikiwa.