Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Hii ni Mwananchi ya leo
Naendelea na zile makala zangu za KMT, (Kwa Maslahi ya Taifa) za uelimishaji umma kuhusu katiba, sheria na haki, leo nikiendelea na ile mada ya wiki iliyopita ya jinsi haki ya Mtanzania kumchagua kiongozi anayemtaka na haki ya Mtanzania kuchaguliwa kuwa kiongozi, ilivyoporwa na kipengele batili cha katiba, kilichochomekewa kiubatili ndani ya Katiba yetu ya JMT ya Mwaka 1977, ambapo kumeifanya katiba ya JMT kuwa ni katiba batilifu yenye ubatili!, na sheria zilizotungwa kwa kipengele hicho, kuwa ni sheria batili kwa jicho la kisheria, na miongoni mwa sheria batili hizo, ni sheria yetu mpya ya uchaguzi, iliyotungwa na Bunge la JMT mwezi January mwaka 2024 na Rais Samia kuisaini ianze kutumika ambayo ndio itaendesha uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, 2025, kwasababu imetungwa kwa kujumuisha kipengele hicho hicho chenye ubatili.
Hapa naomba kutoa elimu kidogo kuhusu batili na batilifu. Batili ni kitu chenye ubatili tangu mwanzo, void ab initio, ambapo ubatili wake haurekebishiki kabisa.
Batilifu ni voidable, ni kitu chenye ubatili unaoweza kuondosheka na kurekebishwa kuwa halali. Katiba yetu ni voidable, ubatili wake unaweza kurekebishika.
Kitu cha ajabu zaidi katika siasa zetu za uchaguzi, tumetunga sheria mpya ya uchaguzi na sheria ya kuiunda upya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kuwa Tume Huru ya Uchaguzi, chaguzi zote zilipaswa kufanyika kwa sheria mpya na kusimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi, lakini tunakwenda kufanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa sheria ile ile ya zamani, na uchaguzi unasimiwa na Tamisemi, kwanini Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usifanyike siku moja na uchaguzi mkuu na usimamiwe na Tume moja huru na Shirikishi ya uchaguzi?!.
Swali kuu la msingi la kujiuliza ni Rais Samia ni mtaji wa haki na fursa ya haki kwa Watanzania, tangu ameingia madarakani, ameonyesha kwa kauli na matendo, yeye ni mpenda haki, ni muwaza haki, ni msema haki na mtenda haki, kwanini wasaidizi wake sheria, hawautumii mtaji huu tulionao na fursa hii ya Rais Samia kuwatendea haki Watanzania?!.
Na badala ya kumtungia sheria ya Uchaguzi ya haki, wao wamemtungia sheria batili ya uchaguzi, yenye vipengele batili, ambavyo viliisha batilishwa na Mahakama Kuu?!.
Haki Kuu ni zipi?.
Ni haki ya Kuchagua na Kuchaguliwa!.
Ibara ya 5 ya katiba, imetoa haki kwa kila Mtanzania anapofikisha umri wa miaka 18, ana haki ya kupiga kura kuchagua kiongozi anayemtaka bila sherti jingine lolote na Ibara ya 21 inatoa haki ya kila Mtanzania anapotimiza umri wa miaka 21, anakuwa huru kushiriki katika siasa na uongozi kuanzia serikali za mtaa hadi serikali kuu, bila ubaguzi wowote.
Hivyo ili Mtanzania awe huru kumchagua kiongozi yoyote anayemtaka kwa mujibu wa ibara ya 5, ni lazima huyo Mtanzania awe huru kushiriki kwa mujibu wa Ibara ya 21
Lakini kukatokea kikundi fulani cha watu, kwa maslahi yao, na kwa vile serikali ni yao, wakaipindua katiba kwa kuinyofoa haki hiyo ya kila mtu kushiriki siasa, iliyotolewa na katiba, na kupachika inara ya 37 na 69 zenye shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa, hivyo kujenga ubaguzi katika kushiriki shughuli za uongozi umma kwa watu kulazimishwa kwanza kujiunga na vyama vya siasa, ndipo upate haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma!. Huku sio kuwatendea haki Watanzania wengine wote, wasiotaka kujiunga na vyama vyovyote vya siasa, lakini wana uwezo wa uongozi. Hii ni haki muhimu iliyotolewa na katiba, kitendo cha kuingiza shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa ni kinyume cha katiba.
Ubatili ni Upi?
Ule uhuru uliotolewa na Katiba wa kila mtu kuwa huru kushiriki shughuli za uongozi, kupitia ibara ya 5 na ibara ya 21, umekuja kunyofolewa na ibara ya 39 na 67 (b)(c) kwa kuweka shurti, ili mtu kuweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma, nchini Tanzania, ni lazima uwe ni mwanachama wa chama cha siasa, na ili kugombea uongozi ni lazima upendekezwe na chama cha siasa hivyo kwa kudhaminiwa na chama cha siasa!, Haki zinatolewa na ibara moja katiba halafu zinaporwa na ibara nyingine ya katiba hiyo hiyo!.
Mchungaji Mtikila (Mungu amuweke mahala pema peponi), mwaka 1993, alifungua kesi No. 5 ya 1993, kupinga kifungu hiki na Mahakama Kuu chini kwa Jaji Kahwa Lugakingira, (Mungu amuweke mahala pema peponi), ikatamka wazi na bayana kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo kifutwe, na kutoa haki kwa kila Mtanzania ana haki ya kushiriki kugombea Uongozi.
Hapa ndipo mwanasheria mimi, ninapotofautiana na wanasheria wa serikali, na wanasheria wa Bunge, kuwa anayebatilisha sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba sio Mahakama Kuu, ni Ibara ya 64 ya katiba yenyewe, jukumu la Mahakama ni kuuthibitisha tuu huo ubatili na kuutamka ni batili, na tangu ulipotamkwa ni batili, tangu wakati huo ubatili huo unakuwa umebatilika.
Baada tuu ya Mtikila kushinda kesi serikali ikafanya mambo mawili makubwa ya ajabu!, kwanza ilikata rufaa kuupinga uamuzi huo, Pili serikali ilipeleka bungeni kwa hati ya dharura, sheria No. 34 ya mwaka 1994, kufanya marekebisho ya 8 ya Katiba ya JMT kwa hati ya dharura na kukichomeka kipengele hicho ndani ya katiba, hivyo kuibatilisha ile hukumu ya Jaji Lugakingira!. Hapa ndipo katiba yetu ilipochomekewa ubatili kiubatili.
Baada ya kufanywa marekebisho hayo batili ya katiba, sasa ibara hiyo ya 21 ya katiba, inasomeka hivi,
21. “ Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 39, ya 47 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchaguwa na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi”
Mchungaji Mtikila, licha ya kuwa ni mwanasiasa, Mwenyekiti wa chama cha siasa cha DP, (Democratic Party), lakini alikuwa ni mtu wa Mungu kiukweli kweli kabisa, hakukubali katiba yetu inajisiwe!, hivyo akafungua kesi nyingine No. 10 ya mwaka 2009 kupinga marekebisho hayo ya 8 ya katiba yaliyofanywa na Bunge.
Katika kesi hiyo, Mchungaji Mtikila aliomba mambo mawili makuu
(a) Mahakama itamke ibara 39 na 67 za katiba zilizorekebishwa na marekebisho ya 8 kwa sheria No. 34 ya mwaka 1994, ni batili na kinyume cha katiba.
(b) Kutamka wazi kuwa Kila Mtanzania ana haki ya kugombea kwa mujibu wa ibara ya 21 ya Katiba, bila kulazimishwa kudhaminiwa na chama cha siasa, hivyo mtu anaweza kugombea kama mgombea binafsi.
Mahakama Kuu chini ya majaji watatu, (majaji watatu kisheria inaitwa Half Bench), Amiri Manento, Salim Masati na Thomas Mihayo, wakayakubali mambo yote ya Mchungaji Mtikila na kumpa ushindi tena kwa kutamka marekebisho hayo ya 8 ya katiba ni batili!. Hivyo aliyetamka katiba yetu ni batili sio mimi bali ni Mahakama Kuu ya Tanzania.
Japo serikali yetu ilikakata tena rufaa, na safari hii Mahakama ya Rufaa ikakaa Full Bench ya majaji 7, chini ya Jaji Mkuu Mwenyewe, Agustino Ramadhani, akisaidiwa na Jaji Eusebio Munuo, Jaji January Msoffe, Jaji Natalia Kimaro, Jaji Salim Mbarouk, Jaji Benard Luanda, na Jaji Sauda Mjasir. Tena Mahakama haikuwa peke yake, bali iliwaita mabingwa wabobezi wa sheria na katiba kuisaidia, hawa ni wanaitwa marafiki wa mahakama, kwa kiingereza ni friends of the Court, kisheria wanaitwa Amicus Curiae, hivyo ma Amicus Curiae hawa, Mr. Othman Masoud Othman, Prof. Palamagamba Kabudi, na Prof. Jwan Mwaikusa(Mungu Aiweke Roho yake Mahala Pema Peponi)
Ambapo tarehe 17 mwezi June, mwaka 2010 ikatoa hukumu ya mwaka, inayoitwa landmark judgement, Mahakama ya Rufaa ikaamua kuwa Mahakama haina mamlaka ya kuliingilia Bunge, katika vipengele vya katiba, kumaanisha kwa vile marekebisho hayo ya 8 yamefanywa na Bunge, hivyo ni Bunge ndio lirekebishe kipengele hicho!, mpaka hii leo, Bunge halikuwahi kuubadilisha ubatili huo ndani ya katiba yetu, hivyo katiba yetu ni batilifu na sheria ya uchaguzi ni batilifu kwa jicho la kisheria.
Kwa vile Rais Samia ni fursa ya kurekebisha katiba na kuuondoa ubatili huu ndani ya katiba yetu, wasaidizi wa Rais Samia sheria, kwanini hawakuitumia fursa hii na badala yake kumtungia sheria batili na kumsainisha sheria batili ya uchaguzi?.
Kwa vile Rais Samia, sio Mwanasheria, hivyo haitarajiwi lazima aujue ubatili wa katiba na ubatili wa sheria, lakini wasaidizi wake sheria, ni wanasheria manguli wabobezi na wabobevu ambao wanaujua ubatili huo, kwanini wamemtungia sheria batili na kumsainisha huku wanajua fika kuwa sheria hiyo ni batili?.
Naamini kabisa Rais Samia wakati anasaini sheria mpya ya uchaguzi, yeye hakujua kuwa anasaini sheria batili, hivyo naamini watu kama akina sisi , tunapojitokeza
Kama hivi kumweleza kuhusu ubatili huu, na kwamba amesainishwa sheria batili, anaweza kusikia, and something might be done kurekebisha ubatili huu kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025.
Mungu Mbariki Rais Samia, kutuondolea ubatili huu.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali