Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwaapisha viongozi wateule Ikulu ya Tunguu, Zanzibar, leo Julai 5, 2024
Rais Samia amewapongeza wateule wote kwa kupata nafasi mpya. Amemtaka Jafo kurejea Ilani ya chama cha Mapinduzi kwa kuwezesha kukua kwa biashara za watanzania pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto za wafanyabiashara. Kariakoo ni eneo muhimu la biashara, akaifanye kariakoo kuwa kitovu cha biashara kwa masaa 24.
Amesema Kariakoo kuna siasa sana na wakati wa mgogoro alituma timu ya siri na amebaini hata huu mgomo baadhi ya wafanyabiashara walikuwa hata hawajui kwanini kuna mgomo zaidi ya kupewa maelezo na viongozi wao. Biashara sasa ni field, Jafo asikae Ofisini.
Akitolea mfano wa Video iliyosambaa mtandaoni ikihusisha mwanamke mtanzania na mwanaume raia wa China, Rais Samia amesema ipo pia migogoro inayotokea kati ya wageni na wenyeji sokoni Kariakoo, amemtaka Jafo kuangalia suala hili kwa undani kwanini inatokea.
Kuhusu uteuzi wa bosi mpya wa TRA, Yusuph Juma Mwenda Rais, Samia amesema chini ya Kidata mapato yalikua sana na amemuondoa hapo sababu aliona mwisho atadata maana kafanya kazi kubwa. Hivyo ameteua mtu mpya ili akapambane pia kuongeza mapato na kukusanya zaidi pamoja na kuziba mianya ya upigaji. Amesema Mwenda aisende kufanya kazi kwa kuridhisha watu bali amridhishe yeye aliyemteua.
Aidha, Rais Samia amesema ipo michezo mingi inafanywa na wafanyabiashara na wawekezaji ikiwemo mashine za EFD, msamaha wa kodi, VAT, PAYE n.k hivyo kamishna mpya anapaswa kufuatilia masuala haya kwa undani wake.