Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema amemuondoa aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata kwenye nafasi yake kwakuwa aliona atadata kwa jinsi anavyoandamwa lakini amekiri kuwa TRA chini ya Kidata imefanya vizuri na kuongeza mapato hadi kufikia Tsh. trilioni 27.64, ambayo ni sawa na ufanisi wa 97.67% ya lengo la kukusanya Tsh. trilioni 28.30 katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2023/24 ambalo ni ongezeko la 14.50% ikilinganishwa na makusanyo ya Tsh. trilioni 24.14 katika Mwaka wa Fedha uliopita, 2022/23.
Akiongea leo July 05,2024, Ikulu ya Tunguu, Zanzibar wakati akiwaapisha Viongozi Wateule, Rais Samia amesema โYusuph Mwenda kwanza hongera kwa kazi nzuri uliyofanya Zanzibar, tunakupeleka TRA (kuwa Kamishna mpya), TRA chini ya Kidata imefanya vizuri sana, mapato yamekua sana, sitegemei kama utashuka, kwanini nimemuondoa Kidata?, Kidata nimemuondoa niliona mwisho atadata, kazi kafanya nzuri sana lakini niliona atadata jinsi anavyoandamwa , sasa nakupeleka wewe Kijana wa Dar es salaam
Mtoto wa Mjini, uhuni wote ulioko TRA kule umefanywa na wewe ukiwa mulemule pengine uli-participateโ
โMipango yote mule ya kupenya, ya kufanyaje na Bandari mnatoa wapi mnapenyeza wapi unaijua Yusuph nenda kaizibe, nenda kaizibe, tunachohitaji ni mapato, tunachohitaji ni kupungua kukopa, tunakopa tunajichetua kila anayekuja akija European Bank yes yes, akija huyu Yes, World Bank wanatunyanyasa tumo tu, nini?, tuna miradi ya maendeleo inataka pesa, pesa hatuna tunakopa, tunakopa tunanyanyasika, je tukiwaomba itakuwaje?, kwahiyo twende tukanyanyue za kwetuโ
โSerikali imefanya yote, tumeweka mazingira mazuri ya kufanya biashara, mazingira mazuri ya kufanya uwekezaji, Wawekezaji wanakuja, biashara zinafanyika kodi hazilipwi, Kariakoo pale tatizo ni kulipa kodi ukienda leo wanakuambia hiki kesho wanakuambia hiki, Kariakoo pekee yake kuna mapato kama yatakusanywa vizuri kwa mwaka yanaendesha Wizara tatu lakini hamkusanyi kuingia Serikalini, inawezekana mnakusanya kuingia mfukoni lakini hamkusanyi kuingiza Serikalini nenda kazibe hiloโ
โMwenda unaijua vizuri TRA ulikuwa sijui Mkurugenzi wa kodi zipi lakini ulikuwa unajua mnaibia vipi na wenzio kwahiyo yale mliokuwa mkiiba vichochoro vile nenda kazibe tunahitaji fedha, nimekuamini na najua utakwenda kufanya kaziโ
#MillardAyoUPDATES
NB: Kiukweli 2025 tugangamale vingine tutakuja kuwa Zimbambwe iliyochangamka.