Rais Samia: Nimewatia wadhamini timu za Simba SC na Yanga SC

Rais Samia: Nimewatia wadhamini timu za Simba SC na Yanga SC

Inside10

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
29,909
Reaction score
32,414
Najua wadhamini au washika vilabu vile wanafanya jitihada kubwa sana, lakini pamoja nao nimeongea na wadau wawekezaji wetu wakubwa hapa, mmoja nimempa Yanga mmoja nimempa Simba awasaidie, kwahiyo litakapokamilika tutaitana vilabu tuambizane" - Rais Samia akizungumza katika uwekaji wa Jiwe la Msingi Suluhu Sports Academy Mkunguni- Kizimkazi Zanzibar

Nb. Hatua nzuri na vilabu vingine pia vitazamwe kidogo kidogo.
Je, nini kimekufurahisha? Nkni kimekushangaza?
 
hao tayari wana wadhamini angewaweka kwenye vilabu vingine ili ushindani uongezeke zaidi. sijui kwanini tanzania huwa tunataka kuwa na washindani wachache tu.
 
Cha ajabu utakuja kusikia wale viongozi wa vilabu ambavyo havijatafutiwa udhamini vinakwambia " HAKUNA KAMA MAMA, ANAUPIGA MWINGI"
 
Inatakiwa Academy kama ile ya Zanzibar tuachane na udhamini wa vilabu ambavyo pesa huishia pigwa bila manufaa
 
Siasa michezoni. Eti Rais kazitafutia wadhamini Yanga na Simba, kivipi? Olympics tunatia aibu miaka nenda rudi na hakuna anayeshtuka. Unaleta mdhamini mpya kwa klabu kama Simba wakati mchakato wa mabadiliko umekwama, si kuleta mvurugano zaidi ndani ya Klabu?
 
Angewatafutia wadhamini kina jku na mwenzake ambao mechi zote wanacheza ugenini, Simba na yanga ni brand zinazojiuza.
 
Hayo ni maandalizi tu. Kuja kushituka DPWORLD huyu hapa kasepa na vilabu vya simba na yanga🤣
 
Aisee wanasiasa nuksi sana ...hapo ni simba na yanga sababu wana wapiga kura wa kutosha kina lmc na pamba jiji mtatusubiri kwanza.
 
Mohamidin Riyadh El makhtur Oman - Yanga
Jalmin Hussein Jamil khasmin Dubei- simba
 
Back
Top Bottom