Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema mafanikio yaliyopatikana katika sekta mbalimbali nchini yametokana na usimamizi imara wa mapato ya serikali yanayotokana na kodi za wananchi na mikopo kutoka vyanzo mbalimbali.
Akizungumza leo, Septemba 10, 2025, mbele ya umati wa wananchi wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Dkt. Samia amesema matumizi bora ya fedha hizo yamewezesha miradi mingi ya maendeleo kuonekana na kutekelezwa kwa ufanisi, sambamba na kudhibiti vitendo vya rushwa.
“Tumesimamia matumizi mazuri, na watumishi wetu tumeweza kuwaweka kwenye mstari wa kusimamia matumizi na kuepuka rushwa, ndugu zangu,” amesema Dkt. Samia.
Amefafanua kuwa bila usimamizi huo madhubuti, mafanikio yaliyoshuhudiwa hivi sasa yasingekuwepo, huku akibainisha kuwa serikali imefanya kazi kubwa kuhakikisha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma inalindwa.
Dkt. Samia pia ametaja tafiti za mashirika mbalimbali zinazohusiana na hali ya rushwa nchini, zikionesha kuwa viwango vya rushwa vimeendelea kupungua kutokana na jitihada za serikali ya awamu ya sita.
Aidha, amewaasa wananchi wa Nzega na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura, kama wanavyojitokeza kwenye mikutano ya kampeni, ili kutumia haki yao ya kikatiba na kuchagua viongozi wanaowataka