Aisee kama kuna kipindi watu wamedhulumiwa ardhi yao ni kipindi hiki. Huku Kinondoni sehemu za mabwe, malolo, mji mpya, kinondo, mbopo na maeneo ya jirani kuna migogoro inatengenezwa na wakubwa kupitia diwani wa mabwepande na wenyeviti wa serikali za mitaa halafu wanatumia watu wao wanawadhulumu masikini viwanja vyao na wengine nyumba zao zinavunjwa. Kahamishwa mkuu wilaya Gondwe lakini bado hayo mambo yanaendelea.
Ila bado washirika wawili wakihamishwa hao mwenye mkoa wake na mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni nadhani hii migogoro itapungua sana kama sio kuisha kabisa. Haiwezekani mtu eneo la kwake na analimiliki kihalali lakini kwa kuwa tu hana hati eti anapimiwa anauziwa tena kiwanja chake mwenyewe square meter 1 kwa TZS 6,500 wakati inajulikana gharama za serikali kupima kiwanja kimoja (na sio square meter) ni kati ya TZS 150,000 - 250,000 bei elekezi ya serikali iliyotangazwa na aliyekuwa waziri wa ardhi ndugu Lukuvi. Masikini gani atakuwa na hizo hela kama sio kunyanga'nywa kijanjajanja. Hizi pesa mamilioni kwa mabilioni zinaenda wapi na ni mradi wa nani? Na kama huna pesa za kulipa unanyanganywa kwa gia kuwa eneo hilo unaambiwa mali ya NSSF au DDC. Kama ni mali ya NSSF au DDC vipi anyanganywe masikini halafu auziwe mwenye pesa?
Na ni kwanini wanakataa wakaazi wa huko wasitumie kampuni binafsi kupima ardhi yao kuna ni nini nyuma ya pazia? Na waziri wa ardhi yupo wapi au mpaka raisi atembelee mwenyewe kuzungumza na na wanachi ndio atajifanya kushtuka. Mbunge Gwajima suala hili analijua na amepambana sana kuwapigania wananchi lakini inaonekana kuna genge kubwa linamzunguka na linataka kumzidi nguvu. Makubaliano yakifanyika kwenye mikutano ya hadhara na mbunge akiwepo akiondoka tu huku nyuma viongozi wenzake na wenyeviti wa mitaa wanakuja na maazimio tofauti kabisa.
Mwisho mhemshimiwa raisi tunaomba utume wasaidizi wako waje kwa siri maeneo hayo kwa kweli taarifa watakazokusanya hautoamini kujua kile ambacho watanzania wanapitia kwenye nchi yao tena hapa hapa mjini na wala sio mikoani huko.