johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Rais Samia ameliagiza jeshi la polisi kuhakikisha linakamilisha upelelezi kwa haraka na kuwaachia huru watuhumiwa ambao kesi zao hazina mashiko.
Rais amesema hivi sasa idadi ya wafungwa inakaribiana kuwa sawa na idadi ya mahabusu.
Kadhalika Rais Samia amemtaka IGP Sirro kuhakikisha hawatumii mabavu bila tija na tabia ya mahabusu kufia rumande hayatoi picha nzuri kwa jeshi hilo.
Chanzo: TBC
=======
Rais Samia Suluhu Hassan amelitaka Jeshi la Polisi kukaa na wadau wengine kuangalia uwezekano wa kurekebisha Sheria ya kuweka watu mahabusu, akisema kwenye Nchi nyingine mtu hakamatwi mpaka upelelezi utimie
Ameeleza Kesi nyingi zinakwama Mahakamani kutokana na kucheleweshwa kwa upelelezi au kukosekana ushahidi akisema, "Hizi tunaita kesi za kubambikiza"
Amesisitiza, "Kama kesi haina mwelekeo watu watolewe. Kwa kesi ambazo mna uhakika upelelezi utatimia basi uharakishwe"