Rais Samia: R4 si sababu ya Utovu wa Nidhamu, Serikali italinda Amani kwa gharama yoyote

Rais Samia: R4 si sababu ya Utovu wa Nidhamu, Serikali italinda Amani kwa gharama yoyote

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Rais Samia akifunga mkutano mkuu wa maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi kwa mwaka 2024 na maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Tanzania katika viwanja vya Jeshi la Polisi (CCP) Kilimanjaro, amesema;

R4 si sababu ya utovu wa nidhamu, si sababu ya kukiuka sheria za nchi sheria za nchi zipo pale pale, ni vizuri wasisahau mapito waliyopita. Serikali imejitahidi sana kurejesha uhuru wa vyama vya siasa,uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa raia.

Kwa ujumla wale waliokuwa uhamishoni walirejea nchini, waliokuwa na kesi za jinai na wengine tulizifumbia macho, waliokuwa jela tuliwatoa sasa wapo huru na wanaendelea na shughuli zao ikiwamo shughuli za kisisasa, lengo letu likiwa kuwaleta watu pamoja ili tuweze kujenga nchi yetu.

Sasa watu wale wale wanaposahau yote hayo na wanapofanya vitendo vya kutoa kauli zinazoharibu au kuturudisha nyuma sisi hatutokuwa tayari kuwaruhusu kufanya hivyo. Amani ya nchi yetu tatailinda kwa gharama yoyote ile.

 
Back
Top Bottom