Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshangazwa na tabia ya baadhi ya Wananchi kutodai au kutoa risiti kisa yeye Rais hajawaambia wafanye hivyo akisema huo ni wajibu ambao hauhitaji hadi Rais aseme.
Akiongea leo October 04,2024 Ikulu Jijini Dar es salaam wakati akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi, Rais Samia amesema “Niwasahihi tuendelee na moyo huohuo wa kizalendo, kila tunapouza au kununua tudai risiti, na hapa ndio kwenye tatizo kubwa sana, nakumbuka Timu ya TRA ilitoka kwenda Nyanda za Juu Kusini mwaka jana, Watu hawatoi risiti hata kidogo, walipoulizwa wanasema Samia hajatuambia, mwenzie alikuwa anasema ukinunua dai risiti ukiuza toa risiti sasa huyu hasemi, sasa kama risiti zinatoka mpaka kwa kauli ya Rais hatupo vizuri, hatupo vizuri TRA naomba mjipange sana”
Katika hatua nyingine Rais Samia amesema ““Mwezi September tumekusanya mapato ya Tsh. trilioni 3 na hii inanikumbusha kitu, nilipokuwa Makamu wa Rais nadhani mwaka 2017, kuna Balozi kutoka Nchi moja ya Ulaya alikuwa anamaliza muda wake akaja kuniaga, na kipindi kile ndio Rafiki zetu wameondoa mradi wa MCC Tanzania, kwahiyo alipokuja kuniaga akaniambia sasa MCC imefutwa mtafanyaje, nikamwambia tutakusanya fedha za ndani akaniambia unafikiri mtakusanya mpaka ngapi?, wakati ule nadhani tulikuwa kwenye trilioni 1 na point, nikamwambia tutakusanya mpaka trilioni 2 lakini leo nafurahi tumefika trilioni 3”
“Hakuamini nilichomwambia lakini akisoma leo hata kama ameondoka, na hii trilioni 3 ni kwa mwezi, na hii September ni makusanyo ya kawaida tu, December ndio Watu wengi wanakwenda kulipa kodi kunakuwa na kiwango kikubwa, sasa kama September tumefika trilioni 3 kwa effort hii bila nguvu bila maneno, Kamishna wa TRA yuko wapi?, aah yupo, sasa hii katika mwezi sijasikia malalamiko wala misukamano ni hii September lakini wale Maaluwatani waliozea kupitisha mizigo bila kulipa walilipa mwezi September ndio maana tumefikia hapa, na lengo kila anayepaswa kulipa kodi alipe kodi stahiki hakuna aliye juu ya sheria na kama Mtu anapata msamaha wa kodi kuna njia za kupita asamehewe na sio kutolipa kisa Aluwatani”.
PIA SOMA
- Rais Samia: Wanaolipa kodi Tanzania ni milioni2 tu