Rais Samia: Serikali kujenga Soko kubwa kama la Kariakoo eneo la Jangwani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Rais Samia amesema Serikali imejipanga kujenga Soko kubwa kama la Kariakoo eneo la Jangwani kupitia pesa za utekelezaji wa mradi ya DMDP ambapo baadhi ya wafanyabiashara (Machinga) watahamishiwa huko pindi litakapokamili.

Soma: Ninachokijua kuhusu Miradi ya DMDP na Ujenzi wa Miundombinu Mkoani Dar

"Dar es Salaam tuna mradi wa DMDP ambao kati ya fedha za DMDP tumejipanga kujenga Soko jingine kubwa na nzuri kama la Kariakoo maeneo ya Jangwani, kwahiyo ni maoni yetu kwamba baadhi ya Wafanyabishara, Wanangu Wamachinga tutawahamisha tuwapeleke kwenye Soko lile la Jangwani na wakafanye biashara zao kwa nafasi"


Your browser is not able to display this video.
 
Kabisa kabisa, nikashangaa eneo kubwa kama Jangwani tena katikati mwa mji linakaaje tupu muda wote huo?
 
Wakati wanajenga kituo cha kuweka mabasi walifikiria nini kwanza na kukiondoa.
 
Tusirudie makosa yaliyofanywa kwenye ujenzi wa kituo cha mwendokasi. Wataalamu walijiridhisha panafaa ila the rest is history.
 
Tutakua tunaingia sokoni na kutoka kwa kuogelea. Kama kawaida yetu "A lots of Plans with poor planning"
 
Bado tu wanataka kujaza mafoleni mjini? Kweli tunahitaji ukarabati mkubwa wa vichwa vyetu
Soko lijengwe mjin tu,

Dodoma walijifanya wamekarabat vichwa wamejenga soko nje kabisa ya mji ili kukwepa folen, umeona kilichotokea ? Njombe wamejenga mjini kabisa soko lao, umeona lilivyo ?
 
Kwenye hili tumekosea sana. tutaenda kukosea sana kuweka Soko Kubwa tena Jangwani just mkabala na Kariakoo. Hapo itakuwa foleni kubwa sana ya magari Mjini. Mimi kama ingekuwa soko kama la Kariakoo ningeshauri lijengwe Bunju, Mbezi-Kibamba, Mbagala-Kongowe hapo tungeenda sawa kudengonjest city center. Otherwise hapa itakuwa kama kituo cha mwendokasi. Jagwani wangechimba mifereji mikubwa .ya kuondoa mafuriko kwa kuunganisha na Bahari then Pembeni tupande miti kupendezesha jiji. Basi.
 
Soko lijengwe mjin tu,

Dodoma walijifanya wamekarabat vichwa wamejenga soko nje kabisa ya mji ili kukwepa folen, umeona kilichotokea ? Njombe wamejenga mjini kabisa soko lao, umeona lilivyo ?
Dodoma watu wakihamia Mtumba litaanza kuchangamka. Bado ofisi nyingi zipo mjini mpaka sasa
 
Soko lijengwe mjin tu,

Dodoma walijifanya wamekarabat vichwa wamejenga soko nje kabisa ya mji ili kukwepa folen, umeona kilichotokea ? Njombe wamejenga mjini kabisa soko lao, umeona lilivyo ?
Ukiona hivyo maana yake havikuwa vimekarabatiwa ilikua hivihvi, kichwa kilichokaa sawa hakiwezi kufanya investment ya ukubwa huo ikafeli! Yani wanapitwa akili na yule mchaga wa tegeta kibo? Alianza kukiwa porini kabisa na hajawahi kufeli. Huwezi kumlinganisha na viazi vilivyoweka kituo cha mwendokasi jangwani na leo wanakuja tena na jipya, watakua wamejifunza kukwepa mafuriko tu ila akili yao ni ileile km ya kuweka uwanja wa Mkapa na shamba la bibi sehemu moja! Pathetic
 
Hivi viongozi watapata lini akili?

Kiongozi mkubwa kama huyo haelewi nature ya eneo la jangwani?

Mradi mwingine wa kipigaji huo unaandaliwa!

Ni kichaa peke yake mwenye kuwaza kuweka mradi mkubwa kama huo kwenye mkondo wa bahari! Huku ni kuchezea kodi za wananchi!
 
Mambo Kama hayo yalipaswa kufanywa mikoa mingine Kama Moro goro itinga mbeya nk

Ili kilihusu mikoa mingine kukuwa

Badara ya kuangalia dar peke yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…