Pre GE2025 Rais Samia: Serikali kupitia REA imeanza kutoa ruzuku kwenye miradi ya nishati ya gesi ya kupikia, majiko ya gesi na majiko ya umeme

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza kutoa ruzuku kwenye miradi ya nishati ya gesi ya kupikia, majiko ya gesi na majiko ya umeme ikiwa ni utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa kuhamasisha na kurahisisha upatikanaji wa nishati safi.

Rais Dkt. Samia ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi rasmi wa Mradi wa Usambazaji wa Mitungi ya Gesi ya Kupikia 551,795 nchi nzima kwa bei ya ruzuku iliyofanyika katika Wilaya ya Muheza ambapo Rais Dkt. Samia ametoa mitungi ya gesi asilia kwa wawakilishi wa wakazi wa Wilaya zote za Mkoa wa Tanga.

Mradi huo utahusisha usambazaji wa mitungi ya gesi ya kupikia, majiko banifu 205,000 na miundombinu ya gesi asilia katika Mikoa ya Lindi na Pwani.
IMG-20250227-WA0012.jpg
IMG-20250227-WA0013.jpg
 
Utekelezaji wa miradi mingine unakuwa na sura ya rushwa! Kwanini kwenye election year?
 
Back
Top Bottom