Rais Samia Suluhu Hassan Serikali amesema Serikali ina mpango wa kuzifungamanisha huduma za Usafirishaji wa Treni za Reli ya TAZARA na za Reli ya Kisasa za SGR ili kuongeza ufanisi na kurahisha Usafirishaji nchini.
Rais Samia amesema hayo akiwa Mikumi mkoani Morogoro katika muendelezo wa ziara yake.
Rais Samia Suluhu Hassan Serikali amesema Serikali ina mpango wa kuzifungamanisha huduma za Usafirishaji wa Treni za Reli ya TAZARA na za Reli ya Kisasa za SGR ili kuongeza ufanisi na kurahisha Usafirishaji nchini.
Akizungumza katika ziara yake Mkoani humo amesema "Serikali tuna lengo la kufungamanisha Reli ya TAZARA na Reli ya SGR ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa na watu. Tunajua hapa Mikumi tuna mzigo mkubwa kwa hiyo itakuwa rahisi tukiunganisha hizi Reli kubeba mazao na kupeleka kwenye maeneo yanayotakiwa"