Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Akizungumzia kuhusu malalamiko yaliyopo kwenye kikokotoo katika ufunguzi wa Kikao kazi cha Maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi, Oysterbay, leo Septemba 4, 2023, Rais Samia amesema Serikali inafanyia kazi suala hilo na itaangalia njia nzuri ili kuondoa maneno mengi.
"Tupo tunakifanyia kazi na kuona jinsi tutakavyoenda vizuri kwa sababu masuala ya kikokotoo haya si tu matakwa ya Serikali kutaka kuja na kikokotoo, ni hali ya uchumi na hali ya mifuko yenu ilivyo. Ni hali ya mifuko ilivyo. Tukisema kila anayetoka boom lako hilo hapo, boom lako hilo hapo, miaka 2 tu mifuko ile imekauka." Amesema Rais Samia.
Ameongeza, "Tuliweka hivi ili kuweka sustainability ya mfuko, sasa kwa sababu imepigiwa kelele sana sio tu na jeshi la polisi lakini na wengine, tutakwenda kuangalia sababu tunasema siku zote Serikali yenu ni sikivu. Tutakwenda tuangalie njia nzuri tunayoweza kufanya ili kikokotoo kisilete maneno mengi"