Rais Samia: Sitaki kusikia kesi za mimba shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, huku msituni mimba itatokea wapi?

Rais Samia: Sitaki kusikia kesi za mimba shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, huku msituni mimba itatokea wapi?

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyopo wilayani Namtumbo, mkoani Ruvuma, kuwajibika ipasavyo katika kutunza na kulea wanafunzi waliowekwa chini ya uangalizi wao.

Akizungumza mara baada ya kuzindua shule hiyo tarehe 27 Septemba, 2024, Rais Samia amesisitiza kuwa walimu wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanafunzi wanajifunza vizuri na wanatunzwa kiakili, kiafya, na kijamii.

"Hakikisheni mnalinda maadili ya watoto wetu. Sitaki kusikia kesi za mimba shuleni hapa, huku msituni mimba itatokea wapi? Ukitokea ujauzito, walimu tutakabana shingo kwa sababu huku msituni hakuna pa kutokea mimba," ameongeza kwa msisitizo.

Snapinsta.app_461332709_18253407100258462_5455079285437890558_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom