Rais Samia siyo wote walioachishwa kazi kipindi cha Magufuli walighushi vyeti, wasaidie

Habari Rais Samia,

Nianze kwa kukupongeza kwa uamuzi wako wa kuwalioa waliofukuzwa kazi kwa kughushi vyeti, ila napenda utambue kuna wengine hawaghushi vyeti bali waliachichwa kazi kwa sababu tofauti kabisa na hiyo.

Mimi nitazungumzia wale walioachishwa kazi kwakuwa tu walibadili kada zao baada ya kujiendeleza kisha wakafanya mchakato huo na kukubaliwa kubadili kada zao hasa baada ya kujiendeleza ila wanavyeti halali na wamesomea nafasi au ujuzi huo.

Mfano, ni walimu wa Voda Faster ambao kiuhalisia wao walimaliza kidato cha 6 na kupewa mafunzo ya muda mfupi ya ualimu kwa makubaliano ya kujiendeleza katika fani ya ualimu lakini kutoka na sababu na changamoto au nafasi mbalimbali zilizokuwepo walijiendeleza kwenye kada nyingine na kufanikiwa kubadilisha kada zao.

Ni wazi walimu hawa wengi wao hawakuwa na mapenzi na huo ualimu wa Voda Faster bali walitafuta njia ya kuingilia serikalini na ndicho kilichotokea.

Sasa kumekuwa na sintofahamu juu ya watumishi kama hawa nao kulipwa stahiki zao ambapo wanaambiwa kuwa hawawezi kulipwa kwani wao siyo wahanga wa vyeti feki.

Nikuombe kwa busara zako uwaangalie hawa watumishi pia kwa kuweka utaratibu wa wao pia kulipwa haki zao au kurejeshwa kazini kwenye kada walizojiendeleza na kubadilishwa.

Ni matumaini yangu kuwa utalifanyia kazi.

Nakala:

- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

- Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu.
Acha uwongo,hakuna alihetumbuliwa kwa kubadili kada,sababu ukiwa mtumishi ni haki yako inayolindwa kikatiba kujiendeleza,vyeti feki vilijikita form 4 na form 6,sema ulifoji vyeti tu kuwa mkweli,kakaangu aliingia na voda fasta na sasa hivi siyo mwalimu ni mtumishi serikalini idara tofauti na ualimu,kwann hajaguswa??
 
Ni ibala ipi ya katiba inayomlinda mtumishi kujiendeleza kama siyo uzezeta unaleta na ujuaji wako usiyo na maana?

Miongozo ya utumishi inayotoka kila leo juu ya watumishi unaijua au unaifuatilia hasa unaohusu kujiendeleza?
 
Huwezi ukaelewa kwa sababu uzi huu siyo wako,sasa usiwe unaropoka na kubisha kity ambachohuelewi au huna uhakika nacho
Punguza baasi uongo nani alifanyiwa recategorization halafu kafukuzwa bwana sio Kweli mi nawajua waliofanyiwa na wapo ktk vitengo vyao
Huyo hakufata taratibu au alienda kimagumashi brooo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Unaweza kufanya recategoeization kwa magumashi kweli?nimeweka barua yake yenye sababu za kuachishwa umezisoma?wapi wameandika amefanya magumashi,siyo kila mtu ni muongo kama ulivyo wewe na usilazimishe matukio yafanane na ya ndugu zako kenge wewe
 
Hehe....[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Mmmh em subiri, kwamba huyu huyu jpm wetu aliwatumbua na hao waliobadilisha kada kwa kujiendeleza kwa vyeti vyao halali?

Mbona mimi kuna mtu namjia alikuwa voda fasta akaenda chuo kusomea kitu kingine na JPM wetu hakumgusa yupo kazini kawaida?

Nachojua JPM wetu alidili na akina Makrina ila vyeti vinasoma frida. Anyway.......

Jina la——
 
Wenye vyeti feki wapo na ni wengi Tu na wanajijua kinachoendelea sasa HV ni usanii mtupu, kuna chuo cha mkskati kiko Tanga kimebeba vyeti feki balaan ila kina uhusiano na boss mataifa mmoja HV paka hayupo Acha panya walambe asali...
 
Mleta mada yupo sawa,kuna internal auditor wa SHINYANGA dc alikuwa mwalimu wa leseni akajiendeleza uhasibu kabla ya ualimu,alifukuzwa kazi,pia dada mmoja afisa kilimo SHINYANGA manispaa nae alikuwa mwalimu wa leseni akaenda kusoma SUA aliporudi akafanyiwa recategorization,alifukuzwa pia,wanaelezwa walitakiwa kujiendeleza ualimu kwanza wapate tsd namba,hawakuwa na vyeti feki
 
Nimeisoma hiyo barua (kwa shida maana picha ina low quality) na nimeielewa kwamba, ajira aliyopewa mleta mada ilikua na masharti kwamba akijiendeleza, ajiendeleze kwenye kada ya ualimu. Naomba mleta mada uweke nakala ya mkataba wa ajira hapa (wa mwaka 2006).

Kama mkataba ulikua una masharti na wewe umejiendeleza kwenye fani nyingine, wana haki ya kukula kichwa.

Kumbuka uliajiriwa kwa masharti.
 
Uko sahihi mkayana wao ulikuwa na masharti hayo sasa ninachota kushare humu ni kwanini wanaolipwa mafao ni wenyevyeti feki tu?

Je hawa kwanini hawalipwi na hizo hela zao walizokwishakatwa zinaenda wapi?

Karibu!!
 
Mleta mada yupo sawa,kuna internal auditor wa SHINYANGA dc alikuwa mwalimu wa leseni akajiendeleza uhasibu kabla ya ualimu,alifukuzwa kazi,pia dada mmoja afisa kilimo SHINYANGA manispaa nae alikuwa mwalimu wa leseni akaenda kusoma SUA aliporudi akafanyiwa recategorization,alifukuzwa pia,wanaelezwa walitakiwa kujiendeleza ualimu kwanza wapate tsd namba,hawakuwa na vyeti feki
Kuna mijitu humu kazi yao ni kubisha tu haichunguzi hata kidogo inakurupuka tu
 
Back
Top Bottom