Rais Samia suala la Mikutano ya Kisiasa ni la Kisheria. Huwezi kuomba na kujipa mwenyewe ulichoomba, bila kukubaliwa na wale uliowaomba

Rais Samia suala la Mikutano ya Kisiasa ni la Kisheria. Huwezi kuomba na kujipa mwenyewe ulichoomba, bila kukubaliwa na wale uliowaomba

Chige

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2008
Posts
13,495
Reaction score
29,872
Kumbe Rais Samia alikuwa na mkutano na kundi fulani la watu! Sikufuatilia aliongea nini, kwa sababu huwa napata taabu sana kufuatilia mikutano ya Wanasiasa iwe wa chama tawala au upinzani.

Hata hivyo, kupitia mijadala mbalimbali nikagundua nikakutana na hoja za SSH "hataki" mikutano ya vyama vya siasa!! Mada hizi zikanilazimisha kutafuta video clip ili nisikie kwa masikio yangu alichosema SSH.

Baada ya kumsikiliza, mosi SSH anakiri hadharani kwamba uchumi umeporomoka, na mambo yanayohusiana na uchumi yapo shakala baghala! Kutokana na hilo, SSH ameweka wazi kwamba, priority yake ni kuweka sawa masuala ya uchumi na uwekezaji, na hayo mengine yatafuata baadae.

SSH hakutumia hard voice kupiga marufuku mikutano ya kisiasa bali ameomba sana, tena sana kwa sasa apewe muda ili aweke mambo sawa kwenye masuala ya kiuchumi na uwekezaji.

Nikiwa kama mdau wa masuala ya kiuchumi na uwekezaji, lazima nimpongeze SSH kwa kuona umuhimu wa kuweka mambo sawa kwenye eneo hilo.

HOWEVER, popote pale ulipo, Mheshimiwa SSH unatakiwa kufahamu ama kukumbuka kwamba suala la mikutano ya hadhara ya kisiasa ni suala la kisheria, na HAKUNA aliye juu ya sheria... HAKUNA.

Suala la kufanya mikutano ya kisiasa halitakiwi kuwa ni favor inayoweza kutolewa na Rais wa nchi, na asipotaka, anaitupia kabatini favor hiyo.

Kama unaomba uwekeze nguvu kwenye mambo uliyotaja na kutoa likizo kwa suala la mikutano ya kisiasa basi ombi hilo hukutakiwa kulitoa kwenye mkutano na Waandishi wa Habari bali ulitakiwa kukutana na vyama vya siasa kwanza, na kutoa ombi hilo kwao, na kuwashawishi ni kwanini unaona kwa sasa tusogeze mbele siasa za majukwaani zisizo na mipaka ya kimajimbo.

Ulichofanya kwenye mkutano wako na Waandishi wa Habari sio ombi hata kama umesisitiza mara kadhaa kwamba "unaomba"! Ulichofanya hapo ni kutoa conclusion ya mikutano kutofanyika.

Hilo halikubaliki kwa sababu kufanya hivyo inakuwa ni uvunjaji wa sheria za nchi moja kwa moja, tena mbele ya kadamnasi.

Kama hufahamu, au umesahau, nakukumbusha tu kwamba, Sheria ya Vyama vya Siasa kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019, Kifungu cha 11 (1) (a) kinasema:-

Every political party provisionally or fully registered shall be entitled to hold and address public meetings in any area in the United Republic after giving notification to the police officer in charge of the area concerned for purposes of publicising itself and soliciting for membership.

Utaona hapo sheria inatoa uhuru kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara popote pale ndani ya Jamhuri ili mradi tu wawe wametoa taarifa polisi, na sio kama ulivyosema wewe kwamba "...wanaweza kufanya mikutano ya hadhara" exclusively kwenye majimbo yao TU.

Hiyo ni haki ya kisheria ambayo inatambulika hadi kwenye mabadiliko ya sheria yaliyofanyika wewe ukiwa Makamu wa Rais.

Mheshimiwa SSH popote pale ulipo, hiyo ndiyo Sheria ya Vyama vya Siasa iliyofanyiwa mabadiliko mwaka 2019. Na hapa ningependa kurudia kwamba, kama unadhani unataka watu waelekeze nguvu kwenye masuala ya kiuchumi, na kupeleka likizo mikutano ya kisiasa basi unatakiwa kushauriana na vyama vya kisiasa.

Mkifanya majadiliano bila shaka mtafikia muafaka, ama wa kupeleka likizo mikutano ya hadhara isiyo na mipaka, au wanaweza kuamua kuweka idadi maalumu ya mikutano ya hadhara kwa muda fulani, na kama wataamua kuendelea na mikutano kama inavyoelekezwa na sheria, basi pia hiyo ni haki yao ya kisheria.

Aidha, kama wananchi wenyewe watataka kuwekeza nguvu zao kwenye masuala ya uchumi badala ya siasa, ni wao ndio watakaoamua kupuuzia mikutano hiyo.
 
Huyu Mama sijawahi kumuamini; JPM kafariki anaweza kusema lolote lile wajinga wakamuamini. Kawafanya wengi humu wamuone kuwa yeye ni tofauti na JPM, yaani JPM alikuwa katili yeye hakupenda. Miradi ya JPM yeye hakufurahishwa nayo. Na wengi wanaamini. CCM ni ukoo mmoja, anajua kabisa akijitofautisha yeye na JPM kwa yale Mambo mabaya wajinga wataamini. Wapinzani wengi mlimsifia ati huyu anafaa. Uongo mtupu; CCM tangu zama hizo ndivyo walivyo. Kishaangalia 2025 then 2030, minya katiba minya mikutano. Status quo.
 
Kimsingi huyo mama ni tofauti na JPM hata kama sio kwa kiwango cha kuridhisha. Tatizo ni namna alivyoingia madarakani kama msaidizi. Nilichokiona kwa huyu mama hataki kuudhi pande zote, kuanzia kwa wahafidhina wa chama chake, mpaka wengineo. Kwa maneno marahisi hajiamini, hivyo anachukua tahadhari kutokuudhi watu.
 
Sahihisho kidogo:

Neno 'Ibara' hutumika kwenye Katiba.

Neno 'Kifungu' hutumika kwenye Sheria nyinginezo zote.

As such, ondoa neno 'Ibara' na uweke neno 'kifungu'.

Hata hivyo, common mistake hiyo haibatilishi muktadha na logic ya bandiko lako.

Bandiko zuri, na lina mantiki. Naunga mkono hoja.

-Kaveli-
 
Hii nchi toka ipate uhuru chini ya CCM umasikini haujawahi kutuacha, sijui Samia amekuja na dawa gani ila nachojua anatumia kigezo cha uchumi kutuzubaisha tu.

Ukweli ni kwamba ni vigumu sana demokrasia ya upinzani kukua kwa kusubiri ruhusa toka kwa kiongozi wa CCM huku ni kujidanganya, hiyo ruhusa haiwezi kutoka wako tayari hata kuvunja sheria.

Ujinga kama huu ndio hufanya Chadema waitwe "wanaharakati" na wasiojielewa, kwasababu huamua kupigania haki zao wanazoporwa kwa makusudi na viongozi wa CCM, na mimi naona bora waendelee kuwa wanaharakati tu mpaka watawala watakapobadilika mentality zao.
 
Mkuu Chige ,kongole kwa andishi bora kabisa tuliloamka nalo leo.

Kama alivyoandika mkuu tindo hapo juu,Mh. Rais Samia ni tofauti na JPM, lakini tatizo ni kutaka kutowaudhi pande zote mbili za shilingi.

Tunapozungumzia katiba,lazima tujue kuwa hakuna aliye juu ya katiba.

Sheria pia ni hivyo hivyo.

Kazi ya wanasiasa na vyama vya siasa ni kutangaza sera na mitazamo yao ya uendeshaji wa nchi kwa wananchi. Shughuli za siasa kamwe haziwezi kuzuia shughuli za kiuchumi kusimama. Ni mikutano ya "watawala" pekee ndiyo husimamisha shughuli za kiuchumi.

JPM alipokuwa kwenye ziara/safari zake mahali popote pale,eneo husika shughuli nyingi za uzalishaji mali zilikuwa zinasimama kwa masaa kadhaa ili wananchi wapate kuhudhuria mikutano yake. Na hii ilikuwa ni lazima,sio hiari kama kwenye mikutano ya vyama vya siasa. Ndio maana nikaandika "watawala" na si viongozi.

Kiongozi kamwe hawezi kushurutisha wananchi kuhudhuria mkutano wake.

Ni mwanasiasa gani anaweza kushurutisha wananchi kuhudhuria mkutano wake!!?

Kuna siku tumesimamishwa masaa matatu kupisha msafara wa JPM,masaa matatu!!! Hapo tunajenga uchumi au tunabomoa!!??
 
Huyu Mama sijawahi kumuamini; JPM kafariki anaweza kusema lolote lile wajinga wakamuamini. Kawafanya wengi humu wamuone kuwa yeye ni tofauti na JPM, yaani JPM alikuwa katili yeye hakupenda. Miradi ya JPM yeye hakufurahishwa nayo. Na wengi wanaamini. CCM ni ukoo mmoja, anajua kabisa akijitofautisha yeye na JPM kwa yale Mambo mabaya wajinga wataamini. Wapinzani wengi mlimsifia ati huyu anafaa. Uongo mtupu; CCM tangu zama hizo ndivyo walivyo. Kishaangalia 2025 then 2030, minya katiba minya mikutano. Status quo.
Huyu ni kiongozi mbovu sn kuwahi kutokea
 
Mkuu residentura,

Nakubaliana na wewe moja kwa moja, na pia nakubaliana na hoja ya tindo kuhusu mama! Ni kweli anao utofauti na JPM kwa kiasi fulani... lakini kama alivyosema tindo, SSH anahangaika sana kutaka kufurahisha pande zote, huku akichelea kuonesha anapinga sera za Magu, ingawaje matendo yake yanaonesha tofauti hiyo!!

Kuhusu mikutano ya kisiasa, pia nakubaliana na wewe kwa 100%!! Sijui hawa wenzetu wanapata wapi hisia kwamba mikutano ya kisiasa, hususani ile ya vyama vya upinzani ni chanzo cha vurugu, kuondoa utulivu, na kubwa zaidi kuonekana kama ni chanzo cha kudhoofisha shughuli za serikali kwenye kutekeleza wajibu wao!!

Yaani wanajisahaulisha kwamba, popote pale ambapo zilipata kutokea vurugu basi vurugu hizo zilianzishwa na polisi wao wenyewe, baada ya kupokea maagizo kutoka kwao wenyewe!

Hadi Magu anatutoka bado nimeshindwa kuona tofauti ya matokeo ya "kukwama kwa shughuli za kiuchumi wakati wa JK " kutokana na mikutano ya kisiasa, na "kuboreka kwa shughuli za kiuchumi" wakati wa Magu ambao vyama vilipigwa marufuku!

Miaka 5 ya kwanza iliisha huku rate ya ukuaji wa uchumi ikiwa ile ile, tena miaka mingine ikiwa chini ya wakati kulinganisha na enzi ambazo "vyama vya upinzani walikuwa wanakwamisha shughuli"!
 
Anachukua tahadhari ama ni unafiki tu?,madaraka ni yake ,afanye yote mema bila woga
 
Kimsingi huyo mama ni tofauti na JPM hata kama sio kwa kiwango cha kuridhisha. Tatizo ni namna alivyoingia madarakani kama msaidizi. Nilichokiona kwa huyu mama hataki kuudhi pande zote, kuanzia kwa wahafidhina wa chama chake, mpaka wengineo. Kwa maneno marahisi hajiamini, hivyo anachukua tahadhari kutokuudhi watu.
Mwenda zake kafariki

Mambo ni super! Si uonaona sheria zinatekelezwa kila kona?

Mi 10 kwa mama
 
Rais haombi mtu, rais anatoa tamko tu.

Maagizo ndio hayo sasa chague kusuka au kunyoa
 
Rais haombi mtu, rais anatoa tamko tu.

Maagizo ndio hayo sasa chague kusuka au kunyoa
Kwahiyo rais anaweza kutoa tamko la kuvunja sheria, sio?! Hayo mamlaka anayotolea wapi?!
 
Nilichokiona kwa huyu mama hataki kuudhi pande zote, kuanzia kwa wahafidhina wa chama chake, mpaka wengineo.
Kama ana mtazamo huu wa kupendezesha kila kundi hata kwa kuikanyaga katiba, atazua timbwili litakalo mharibia kabisa.
 
Back
Top Bottom