Wanajamvi, kama sote tujuavyo, nchini kwetu Jana palifanyika uzinduzi rasmi wa reli ya viwango vya kimataifa (SGR) sambamba na mabehewa na train za umeme za kisasa. Mgeni rasmi katika shughuli hiyo adhimu alikuwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tukio lile lilirushwa live na baadhi ya vyombo vya habari sambamba na akaunti rasmi za mitandao ya ikulu pamoja na chama Cha mapinduzi.
Rais Samia alifanya mahojiano maalum na alihojiwa na mwanahabari Babe Kabae aliembatana na WENZAKE kutoka kituo kipya cha radio mahsus cha wanawake kiitwacho malkia radio. Kwanza nampongeza sana kwa kukubali kufanya mahojiano yale, na kuonyesha support kwa wanawake.
Katika mahojiano yale, mh. Rais amejipambanua wazi kama kiongozi mwenye nia ya dhati na wivu mkubwa wa kuleta maendeleo na mabadiliko makubwa sana iwapo atapata ushirikiano pia kama atapewa nafasi na muda.
Alichonifurahisha sana kwanza ni kutokuwa mbinafsi...amekiri MRADI ule ulianzishwa na mtangulizi wake alie mbele za haki, nae ameusimamia mpaka ameufikisha mwisho..aliendelea mbele na kusema anatamani kuunganjsha reli mpaka Burundi na DRC Congo, Ili kuleta ufanisi katika bandari yetu pamoja na biashara ya kimataifa.
Ameongelea pia miradi alioachiwa na mtangulizi wake kama ya umeme tayari ameshauwasha, madaraja kama lile la tanzanite na mingine mingi. Nilipenda alivyokuwa anaongea kwa kujiamini, kwa utulivu, huku akijenga hoja na hakika nilimtizama na kumsikiliza kwa makini sana na hakika nimejenga Imani kwake.
Kingine kilichonifurahisha ni kuwatambua viongozi wastaafu, hii inaonyesha kwamba anatambua nao walichangia kwa namna moja ama nyingine katika kuleta maoni na mapendekezo ya mradi kabla mh. JPM hajaanza utekelezaji wa mradi ule.
Maoni yangu ni kwamba Rais anakwenda vizuri.
Katika maongezi yake nilimsikia anasema alimpa muda maalum Kadogosa na kama angefeli basi angemtumbua.. namwomba mama sasa hii nguvu ahamishie kwenye elimu yetu hapa Tanzania. Ampe muda maalum waziri wa elimu Ili tuone mabadiliko chanya katika elimu yetu.
Mambo ambayo mheshimiwa ana mpango nayo yanahitaji wasomi wazuri Ili waweze kuyafafanua na kuyaelewa, kwa hali ilivyo sasa sometimes wananchi wanadanganywa na wanasiasa ambao kimsingi wanatafuta "political mileage" na wanafanikiwa ktk upotoshaji sababu wananchi hawana elimu sahihi.
Makazini napo huko kwenye utumishi wa uma, watumishi wapandishwe vyeo kwa kuzingatia uwezo wao na sio makaratasi(VYETI) sababu wengine wanaiba mitihani, hawatumii akili zao.. Kuna ofisi unafika unakuta mtumishi hajielewi mpaka unaogopa...Sasa mtumishi kama huyu atawezaje kuelezea miradi ya serikali kwa wananchi wamuelewe?
Mwisho ahakikishe ubunifu na umahiri kutoka kwa viongozi wa serikali, haswa hawa wadogo ambao ndo wapo karibu sana na wananchi. Watendaji wa kata na mitaa wanasema sana na hatuoni mkeka wao nini kazi ya maafsa tarafa?
Ngaiwoye