Rais Samia Suluhu awasili Dar es Salaam akitokea Zanzibar

jitombashisho

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2020
Posts
651
Reaction score
2,246
Akiwa visiwani Zanzibar Samia alihudhuria swala ya kumswalia Hayati mzee Karume ambaye ni mpigania uhuru na mwasisi wa Taifa la Zanzibar.

Mheshimiwa Rais Samia mara baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius K Nyerere ameelekea Ikulu ndogo ya Magogoni iliyopo Dar es Salaam yalipo makazi yake.


Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi wakati akitokea Zanzibar. Amepokewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo, Abubakar Kunenge.​
 
Ikulu ndogo kwa vipi? au Kubwa iko DDM?
 
... hako kanguo alikovaa kamempendeza kweli Amiri Jeshi Mkuu. Very simple, no makeke, no makelele! Kiongozi mkuu ndivyo anavyotakiwa kuwa - SIMPLICITY!
 
Hivi Air Tanzania kazi Yale ni kubeba vigogo? How do you run an Airline like zat? Tsh 90 billion loss last year. RC job description yake, ni kupokea vigogo kila siku? Where is Polepole, Nona amepotea, anther confused young man! 2025 atagombea wapi? Musoma au dar?
 
Akiwa visiwani Zanzibar Samia alihudhuria swala ya kumswalia Hayati mzee Karume ambaye ni mpigania uhuru na mwasisi wa Taifa la Zanzibar.

Samahani Mkuu

Lakni hii ni fikira potofu kwamba Mzee Karume ndio mwanzilishi Taifa la Zanzibar. Katika historia ya ukweli na karibu tu Zanzibar imeanza kukaliwa na binadamu tangu wakati wa Persian Empire. Hassa Bin Ali na watoto wake saba walisafiri katika pwani za Africa Mashariki na walikuwa wakichukuwa maji hapo Zanzibar kwa ajili ya safari zao. Ndio wakafanya vituo na hatimae makaazi ya mapumziko na mji ukaanza kidogo kidogo na ndio maana Mzanzibari asilia anaitwa Mshirazi. Hassan Bin Ali alikuwa anatokea katika mji mkuu wa Iran sikuzile uitwao Shiraz.
 
Safi sana,
Sijaona wale askari na mitutu ya bunduki tayari tayari kama tuko vitani.
Huo ulinzi ni kiboko, wanapgopa nini Kama ni viongozi wazuri. Don’t they do a risk assessment ya eneo?
 
Rekebisha kwanza huu msemo wako kwani logic inagoma ukiachilia ukweli wake.

'MAENDELEO HAYANA VYAMA ILA MAENDELEO YA KWELI UTAYAPATA CCM'
Mkuu nimegoma, mimi ni mwana CCM na nina namba kabisaaa, mahaba yangu kwa hiki chama sio mchezo mchezo 🤣 🤣 🤣 🤣
 

Hasara ya Atcl inaenda ikipungua mwaka hadi mwaka. Uwekezaji wa mradi wa ndege is a long- run business project. Wapuuzi wa kutafuata chipu popularity wanazungumzia hasara tu. Hawasemi kwenye business plan ya Atcl projection yao BEP ilikuwa iwe baada ya kipindi cha muda gani? Hawa angalii Atcl ina impact gani kama kichocheo cha kurahisisha usafiri hivyo uchumi wa Taifa? Hawaoni faida kama hii ya kumfanya Mh Rais na viongozi wengine wajinome na kuharakisha utendaji wa majukumu yao.

Leo spika kawauliza wa Bunge Swali hili chonganishi kuhusu hasara ya ATCL ngoja utaona wale mawakala wa kushinda na marehemu watavyojitoa ufahamu.
 
Is Polepole young or dwarf?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…