Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya

Hakuna mapendekezo zaidi ya kurejea katika rasimu ya Katiba ya Warioba. Hiyo ndiyo itakuwa msingi wa taasisi Imara na kuondoa mrundikano wa madaraka kwa mtu mmoja.
Ooh, katiba ya warioba. Hivi ipo kweli maana hii nchi kubwa na wajanja wengi.
 
Ila hivi vyeo vya kuteuliwa navyo vinawadhalilisha baadhi ya wasomi. Unakuta waziri na katibu mkuu wana vidiplona au bachela halafu msaidizi wao ni Profesa. Yaani Prof anapokea maelekezo kutoka kwa Diploma au Bachelor degree holders. Kuna mokoa unakuta DAS au RAS ni Prof halafu RC na DC ni F4 au diploma!

Kuna wakati mkoa mmoja mkubwa ulikuwa na RC division 0 lakini akisimamia na kutoa amri kwa Masters, Phd na Profs
 
Kama ni hivyo sawa, basi ni sahihi kwa picha hii na maelezo yako haya mkuu.......
 
Basi kama huwafahamu usiwataje kwenye tuhuma kwa umoja wao. Hupotezi chochote kuiheshimu kanda.
Tuhuma zipi au wewe ndio unaona wana tuhuma? Unaweza nionyesha nilipoweka tuhuma dhidi yao?
 
Huyo Mchembe (Mchamba) anabeba mzigo mzito sana kichwanini mwake.

Kamsababishia kifo mtu aliyetakiwa kumpa ushauri makini.

Maisha yake yote atakuwa analijutia sana hili.
mmh...mkuu huyo c shujaa kweli au?
 
Watu wamekuwa hawamsomi vizuri.
Alisema Lawrence Mafuru na Nehemiah Mchechu watateuliwa...Ameangukia pua!!
Naona sasa hivi ana hasira na mama! Majina yote toka VP amekuwa amekosea!!
Kigogo ni boya tu....natembea na upepo.

Niamini......ukiwa mfuatiliaji sana wa jambo au mambo fulani....ukajipa muda wa kutosha kufuatilia mambo....you can predict na ikawa.
Na watu wakakuona wewe ni mtu wa tofauti. Kumbe ni ile kufuatilia tu mambo kwa ukaribu.

Ndicho anachofanya Kigogo....anajuwa kabisa kwa move hii....hiki kinaweza kuwa.....anabashiri inatokea watu wanamtukuza.
 
Katibu Mkuu Ikulu na Katibu Mkuu wizara nani senior kimamlaka? Ukipata jibu basi elewa kwamba boss wa Mkurugenzi MAELEZO ni KM Wizara ya Habari while Msemaji wa Ikulu bosi wake ni KM Ikulu.
 
Katibu Mkuu Ikulu na Katibu Mkuu wizara nani senior kimamlaka? Ukipata jibu basi elewa kwamba boss wa Mkurugenzi MAELEZO ni KM Wizara ya Habari while Msemaji wa Ikulu bosi wake ni KM Ikulu.
Huyo nae suala dogo hilo linamshinda kuelewa.

JF siku hizi sijui imekuwaje!.
 
Msemaji Mkuu wa Ikulu anatakiwa kuwa mtu mkubwa sana. Kwa bahati mbaya kwa nyumbani anakuwa mtu wa kusaini Press releases tu. Cheo cha Msemaji Mkuu wa Serikali hata sikielewi maana inatakiwa kila wizara iwe na msemaji wake.

Hii ni kwa sababu msemaji wa taasisi anatakiwa kuwa na uelewa wa ndani wa shughuli za taasisi yake na hivyo kuweza kuiwakilisha kikamilifu. Hakuna mtu ambae anaweza kuelewa shughuli za wizara na taasisi zake kwa undani kiasi cha kuweza kuzisemea zote. Hii ndio inamfanya nae awe mtu wa releases na kupiga watu viemme.

Amandla...
 
MAMA SAMIA AMETUMIA VIGEZO GANI KUMRUDISHA KIDATA TRA WAKATI ALIKUWA NDO FAILURE PALE.

JE HUYU THOBIAS RICHARD MWENYE UZOEFU WA SALES NDO UMEMPA TPA-SERIOUS?

NADANHI SIKU YAKUAPISHA TUNATAKA MAELEZO.

ASANTE
 
Msemaji Mkuu wa Ikulu anatakiwa kuwa mtu mkubwa sana. Kwa bahati mbaya kwa nyumbani anakuwa mtu wa kusaini Press releases tu. Cheo cha Msemaji Mkuu wa Serikali hata sikielewi maana inatakiwa kila wizara iwe na msemaji wake...
Msemaji wa serikali sio post yenye majukumu yanayoeleweka. Na ndio maana utaona mara nyingu ana-copy/paste habari zile zile za ofisi ya Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu. Hana kipya!

Ila sababu hasa ya kuundwa ile ofisi na kufanywa Idara inayojitegemea ilikuwa kuwa mdhibiti wa vyombo vya Habari. Ndio hiyo ofisi ya Maelezo. Jukumu hili ndilo limekuwa likifanywa sana.

Kuwa msemaji mkuu wa serikali wakati kila Wizara, Taasisi, Mashirika na Wakala ndani kuna wasemaji wao kunafanya Msemaji wa Serikali akose majukumu ya msingi kwenye eneo hilo. Sana sana anabaki kuwa MC kwenye shughuli za kitaifa.
 
MAMA SAMIA AMETUMIA VIGEZO GANI KUMRUDISHA KIDATA TRA WAKATI ALIKUWA NDO FAILURE PALE. JE HUYU THOBIAS RICHARD MWENYE UZOEFU WA SALES NDO UMEMPA TPA-SERIOUS? NADANHI SIKU YAKUAPISHA TUNATAKA MAELEZO.
ASANTE
Mie naona arudishe tu watu wale wale kama vipi kila mtu achukue chake basi maisha yaendelee...
Naona anarudisha wale watu waliotengemeza mianya ya kupiga madili...
 
Waziri ni msimamizi tu na kiongozi wa kisiasa zaidii, hapa hata mtu mwenye uwezo wa kawaida anaweza kuwa waziri.

Kwa upande wa katibu mkuu hapa sio kila mtu anaweza kuteuliwa. Unahitaji mtu mtaalamu wa wizara husika, it's based on seniority and experience. Mfumo wa utumishi wa umma tunaotumia ni British.

Endapo mwenye diploma ama degree ana uzoefu na uwezo kwa nini asiongoze wizara kama katibu mkuu? Hao waalimu wa vyuo wengi hawana field experience. Kuwa profesa chuoni ni rahisi sana ukiwa na kichwa kizuri ktk kuchapisha maandiko ktk fani yako hasa hasa ktk international journals ila ni vitu viwili tofauti kabisa na kuwa na uzoefu halisi na sekta husika. Unaweza kuwa profesa hata na miaka 30 tu ukiwa na kichwa kizuri ktk publish kazi za fani yako. Je, Unaweza kuwa katibu mkuu wa wizara na miaka 30? Umri huu sio rahisi mtu kuwa na uzoefu wa miaka 10.

Kwa upande wa wakuu wa mikoa sawa sawa tu na mawaziri hawa ni wasimamizi tu na viongozi wa kisiasa pia. Ila hao unaowachukulia poa makatibu tawala wa mikoa ni kazi zinazohitaji experience and seniority sio kila mtu anaweza kushika hizo nyadhifa zipo sawa sawa na makatibu wakuu au wakuu wa taasisi ni kazi za kiutendaji zaidi pia ni wasimamizi wa fedha zote zinazoingia ktk eneo lake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…